EPISODE 8: MAPENZI YA JINI LA MAJI Mwandishi: Dominick Chuwa Whatsapp: 0787325447 ........ILIPOISHIA......... Looo! Shikorobo ilibidi achomoe mnazi wake kwa mshutuko akamuinamia Ashura kwenye kichwa mida hii alikua kafunga macho kama mtu aliyepoteza fahamu au kuzimia.........SASA ENDELEA.... Japo alikua ni jini hata yeye alikua na moyo wa huruma na mshtuko kama binadamu wengine, kwa uwoga wa hali ya juu aliaziba pua za Ashura na kupuliza mdomo wake akimpa pumzi kama mtu aliyezama maji. Jitihada zake ziligonga ukuta baada ya kufanya kile kitendo mda mrefu bila mafaniko "Ashura! Ashura! Alimuita mikono ikitetemeka, kiasi kwamba aligusa mashavu yake akawa anazidi kuhlfia ile hali kwa sababu alikua ana baridi ile mbaya. "Amekufa nini? Au hii dawa waliyonipa ya kujibadili hairuhusu kujamiana binadamu?, hapana haiwezekani,"alijiuliza maswali na kujiJibu mwenyewe bila msaada wowote mida ile alikua kwenye kifua akisuukuma kwa viganja vyake haraka haraka. Zilipita dakika kadhaa akaona ile hali si kwamba kafa kwa sabau alipumua, ilionesha kazimia na dawa yake ya kumuamsha anaijua ni tofauti na kutumia maji. Kwa kuwa Ashura alikua uchi wa mnyama na kapoteza fahamu aliona sio vema atumie njia yake ya kumuasha aamke halafu ajikute yuko uchi. Kwa umakini mkubwa alimuosha sehemu za mwili alizochafuka kwa maji yaliyotiririka toka katika mto ule wa majini. Alipohakikisha usafi wa binti yule umekua mzuri na hana doa la uchafu mwilini mwake hasa sehemu zake za ikulu, alichukua kufuli la ashura akalishika vizuri nakuanza kumvalisha toka kwenye unyayo wa kigoli uile mpaka ilipotua nanga katika nyonga zake laini. Kiukweli Shikorobo alikua ni mwanaume mwenye kujiamini na jasiri kwa sababu nahisi angekua ni mwanaume wa sasa halafu mpenzi wake azimie katikati ya mechi kamleta gheto, ungekuta jamaa anakimbia geto na bukta bila kumsaidia mpenzi wake hata maji au kuvalisha nguo kama kitendo alichofanya Shikorobo. Alipomaliza kumvalisha kufuli kilichofata ni gauni lake akimvisha kama mtoto mchanga kwa utaratibu, bila mbwembwe. "Haya ngoja nikuamshe" alisemesha maneno hayo Shikorobo akiwa ndani ya maji nusu kisha alinyoosha mikono yake juu kama anaita kitu flani angani. Baada ya sekunde kama ishrini akiwa kanyoosha vile vile miti ya pale karibu iliamza kupuputisha majani yaliyokauka kwa ajili ya upepl mkali ulioanza kuvuma. Ule upepo ulisogea mpaka pale mtoni upepo ambao uliambatana na ka ubaridi cha kiaina Ukaanza kumpuliza Ashura kwa kasi ya ajabu mpaka gauni lake likaanza kufunuka. Zilikua ni nguvu za kijini alizotumia Shikorobo kuita upepo ule kwa sababu haukudumu ata dakika tano pale pale Ashura alikohoa akiwa anapepesa kope za macho yake. Shikorobo alipoona vile alitabasamu kisha alishusha mikono yake kliyokua bado kagandisha hewani na ule upepo ulipotea pale pale. Ashura akiwa karejesha fahamu zake kama alipokua awali. "mpen......zi bado uko?" Aliuliza Ashura kwa sauti ya uchovu kama katoka usingizi akiwa anataka kunyanyuka akisaidiwa na Shikorobo. "Nisinngeweza kuondoka bila kuona unanyanyuka tena" alijibu shikorbo kwa tabasamu na macho ya kumstai Ashura. Walikaa chini tena nakuanza kuelezeana kilichotokea japo kw aibu na Ashura hakuamini kile kwa sababau alisema ni UTAMU ndio ulioamfamya mpaka apoteze fahamu na kamwe hajawahi kuupata na siku hiyo alimuahidi Shikorobo ata iweje lazima afanye juhudi za kuwa nae milele ata kama ataenda kwwnye falme ya majini yani mpaka pale alikua kaoza bila kujua mpenzi wake siku hiyo ndio alipangiwa kuuliwa. "Ashura unasema kweli unaweza ukaja kwenye falme yetu ya chini ya maji ili uishi na mimi? aliuliza shikorobo baada ya Ashura kusema maneno kama yale. "Ndio niko tayari kwa lolote lakini sio kukukosa wewe Shikorobo" allijibu kwa msisitizo bila kuonesha utani wowote. Shikorobo alijikuta anambusu tena na furaha ya ajabu kwamba Lazima ataenda kuwaelezea zaidi a wake mpenzi mwanadamu aliyempata kakubali kuja mwenyewe kwenye falme ya majini kwa sababau aliwaambia kapata mpenzi binadamu lakini kuhusu ndoa hakuwaambia, hivyo leo ndio siku ya kwenda kuwaambia kwamba yule mpenzi binadamua kakubali kuolewa nae. Baada ya wote kuwa katika furaha Ashura aliona mda umeenda akaamua kunyanyuka na kuchota maji ili aondoke. Shikorobo alimtwisha ndoo baada ya kuchota maji yeye kisha akarudi kwenye lile jiwe akamuaga Ashura ambaye bado urembo wake ulionekana kila alipotembea. ASHURA aliondoka na shikorbo akatumbikia juu ya maji ili ajiande kurudi kwake kuwaelezea wazazi wake zile habari kabla hazijapoa. Akiwa kashatoka kabisa nje ya mto ukingoni mwa mto allikatiza njia yao ya kuelekea nyumbani Ashura ndoo yake ikiwa kichwani Bila kujua hili wala lile kumbe nyuma yake lile kundi la kwenda kumshambulia Shikorobo ndio liliwasili mda e wakina Juma,wazazi pamoja na rafiki wa juma. Maskini binti yule alimuacha mpenzi wake katika hali ya uzima asjijue kinachoenda kumtokea mda ule, na akiuliwa na ameoshaonjeshwa utamu hakika ataumia ila hakuna jinsi ni njama za wazazi wake. Hakushtuka chochote zaidi ya kuendelea kurudi nyumbani yeye alihofia kule nyumbani siku hiyo ndio atapigwa kabisa kwa sababu alichelewa kupita kiasi akiohofia wazazi wake bila kujua ndio kawaacha nyuma. ********* Kikosi cha watu wanne Juma alishika kisu kikali, mama Ashura alishika kibuyu cha dawa, baba Ashura aliyeshika bonge la rungu, na kijana makamo wa juma alishika panga kubwa dizaini anenda kichinja ng'ombe. Kwa usongo wa Shikorobo walifika eneo la mtoni wakiwa na nia ya kwenda kumshambulia au kupigana vita nae. Mda ule kwa bahati mbaya Shikorobo alikua ndio anajitumbukiza pole pole ndani ya maji akiwa ndio kafika kwenye mabega. Wakina juma walopofika kwenye mto walimuona, shikorbo akitaka kuzama kwa sauti ya juu na ya hasira baba yake alipayuka "Shambuliaa huyoooooo" kwa kujisahau walitoka wale watatu wanaume na silaha zao nakutumbikia kwenye maji kwenda kupigana wakimuacha mama Ashura nje ya maji alieyekuwa amebeba dawa. Shikorobo alishtuka kusikia sauti ile aliibuka tena kwa mara nyingine akageuka ile sauti inapotoke ndipo alipokutana na sura tatu za kazi kama wanajeshi na silaha za kutisha wakimfata yeye yani inaitwa tatu kwenye moja..........ITAENDELEA........

at 1:22 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top