JINA: NYOKA WA KUTUMWA SEHEMU YA 7 …………..ILIPOISHIA……………………… KIJANA 1: Jamani nini kimetokea hapa maana sielewi mbona mtego umefyatuka na hakuna kitu kilichonaswa. KIJNA 2: Hata mimi nana shangaa jambo hili, au kuna mtu ametuchezea. KIJNA 3: Nahisi maana tangu nianze kutega hii mitego sijawai kuona ikifyatuka nyenyewe bila kunasa kitu. KIJANA 4: labda kuna kitu kiligusa huu mtego . Kama vipi tutege tena alafu tukajifiche na tuangalie kama itatokea tena . Wakatega tena kisha wakaenda kujificha bila kujua kuwa walifanikiwa kumnasa wakiemtaka na kumtoa wenyewe kwenye mtego na kumuacha huru tena. Walipoenda kujificha tena, Yoka akarudi kwenye umbile lake ya nyoka na kurudi nyumbani kwake. ……………… ENDELEA………………….. Walikaa mda mrefu bila mafanikio yoyote na hatimae jioni ikaingia wakarudi mpaka kwa mfalme na kumpa taarifa hukusu kushindwa kwao kumpata nyoka. taarifa ile ilimuhuzunisha sana mfalme maana alitegemea mafanikio makubwa kutokana na wale watu walio wachagua kuwa hodari kwenye kazi kama zile. Lakini mmoja kati ya wale vijana aliongea kitu ambacho kiliwashangaza sana wenzake pamoja na mfalme. KIJANA: Lakini kuna kitu kinanishangaza kila nikitafakari, hivi ukili una uwezo wa kuufyatua ule mtego, alafu nimeshangazwa na kitu kimoja pale ambapo nilikuwa nimeuhifadhi sikuuona wakati tunatoa ule mtego. MFALME: Mh! Ukili sijawai kusikia ukifyatua mtego, au kuna mtu atakuwa anatuchezea mchezo hapa kijini, sasa nyie nendeni hili jambo nitalifikisha kwa wazee wa kijiji tutajua jinsi gani tufanye. Wale vijana wakaondoka na kurudi majumbani kwao huku kila mmoja akifikiria kuhusu ule ukili, mda mfupi mbele mfalme akaita wazee baadhi wenye cheo pale kijijini kisha akamtuma mlinzi wake mmoja aende akamuite mzee sube. Zikapita dakika kadhaa hatimae yule mlinzi akarudi akiwa ameongozana na mzee sube, mfalme alifurahi kuona vile maana alikuwa anampenda sana yule mzee bila kujua yeye ndie chanzo cha matatizo yote pale kijijini. Kikao kiaanza huku wale wazee wakiwa awajui nini wameitiwa hamala pale. MFALME: Wazee wangu nimewaita hapa kwa ajili ya kuwapa taarifa niliyoipata kutoka kwa wale vijana tuliowatuma kumtega nyoka, lakini kwa bahati mbaya hawakubahatika kumpata lakini kuna jambo wameniambia la kushangaza kidogo. Mfalme akaeleza kama alivyoambiwa na yule kijana na mwisho akawapa nafasi na wao watoe mawazo yao juu ya kile alichowaambia, ndipo mzee mmoja akaanza kuongea. MZEE: Mtukufu mfalme kutona na hiyo taarifa moja kwa moja inaonyesha kuna mtu anatuchezea kwahiyo hatuna budi kumtafuta mganga atakae wenza kutusaidia kututatulia hili tatizo. Mzee sube akamuangalia yule mzee kwa jicho Fulani la kuonyesha kuchukia kile alichokiongea lakini kwa bahati mzuri hakuna mtu ambae alimuona akiwa kwenye hiyo hali. MFALME: Kweli kabisa mzee wangu maana watu wamekuwa wakikichezea sana hiki kijiji chetu cha mbaka kwahiyo lazima tumtafute huyo mganga na ikiwezekana leo hii hii tumchague mganga na apewe taarifa yake ili kesho aje aianze kazi yake, Au unasemaje mzee Sebe unasemaje kuhusu wazo hili. { Aliuliza huku akimtazama mzee sube usoni na kumwachia nafasi ya kuongea } MZEE SUBE: Ni wazo zuri na hatuna budi kulifanya maana huyu nyoka sasa hivi amekuwa hatari na endapo tutamuacha aendelea kuzuru watu wa hiki kijiji tutajikuta wote tumepotea. Mfalme alifurahi sana kuona wote wamekubaliana jambo lile na ndipo akatoa nafasi ya kumpendekeza mganga ambae wao wanaona ataweza kusaidia kutokana na lile tatizo, mzee mmoja akasimama na kumtaja mganga aliehisi yeye kuwa anafaa kuifanya hiyo kazi. MZEE: Mtukufu mfalme kuna mganga mmoja anaitwa mzee Duba ambae tangu ujana wake amekuwa akiifanya hiyo kazi ya uganga na amesaidia watu wengi sana hapa kijijini na kwa sasa anapatika karibia na msitu wa dawa. Mfalme akawauliza wale wazee wengine kama kweli kile alichokisema mwenza, kila aliemuuliza aliitikia haraha lakini ilipofika zamu yam zee sube alisita kwa sekunde kadhaa kisha akakubali kuwa yule huyo mzee Duba anafaa kuifanya hiyo kazi. Baada ya wote kukubaliana mfalme akafunga ule mkutano na kuwaruhusu wale viongozi warudi majuimbani kwao ili kesho yake asubuhi wawai kufika kwa ajili ya kumpokea huyo mzee Duba maana yeye alikuwa hamfahamu. Wale wazee walipoondoka akatumwa kijana mmoja aende huko kwa huyo mganga akampe taarifa kuwa anahitajika kufika kwa mfalme kesho yake, kijana akafanya kama alivyo ambiwa akaanza safari ya kwenda huko karibu na msitu wa dawa kumfuata mganga. Sube alipofika nyumbani kwake akaingia moja kwa moja mpaka ndani bila kumwambia kitu chochote mke wake ambae kwa mda huo alikuwa amekaa nje na kumsababishia mawazo mengi, Haraka mke akainuka na kumfuata mumewe ili akajue nini tatizo mpaka awe kwenye ile hali na wakati sio kawaida yake. BIBI SUBE: Kulikoni mbona upo hivyo. MZEE SUBE: Mke wangu tupo kwenye wakati mgumu sana, usiku wa leo kuna kazi tunatakiwa tuifanye. BIBI SUBE: E ! kwani kimetokea nini huko kwa mfalme. { Aliuliza huku akiwa na uwoga } MZEE SUBE: Kuna mganga kachaguliwa kwa ajili ya kuja kualibu mambo yetu. Bibi sube aliposikia vile, akaanza kutetemeka huku akimrahumu mume wake juu ya wazo ambalo alilitoa ambalo sasa hivi limeanza kuwatia jamba jamba. BIBI SUBE: Heeee ! Sasa tutafanyaje si kuhumbuka huku mume wangu. Lakin mimi nilikuambia hiki tunachokifanya yatatukuta kama yaliyomkuta mzee SUI . MZEE SUBE: Mke wangu wala usiogope haiwezi kutokea kama kilachotokea kwa mzee sui na kila siku nakuambia kuwa mzee sui kilchofanya afe ni uzembe wake yeye pamoja na mwanae. Sasa sikiliza mganga aliechaguliwa ni yule mzee duba kwahiyo leo usiku inatakiwa twende tukapoteze uhai wake maana kama tukimuacha kweli yatatukuta kama ya mzee sui na ama. BIBI SUBE: Hivi kweli tutaweza kumuua yule mzee maana kaanza mda mrefu sana ile kazi na lazima katuzidi uwezo. MZEE SUBE: Hahahaha mke wangu unafurahisha sana. Mzee duba hawezi kufurukuta kwangu japokuwa ameanza zamani ile kazi ila mimi ni zaidi kwahiyo awezi kuzuia uchawi wetu hata siku moja. BIBI SUBE: Hapo sawa mume wangu maana roho yangu ilikuwa hipo juu. Kwa upande wa yule kijna ambae alitumwa aende kutoa taarifa kwa yule mganga kwa bahati mzuri akabahatika kumkuta yule mganga akiwa anatengeza dawa na wakati huo giza lilikuwa lishaanza kuingia. Alipokelewa vizuri sana na mzee Duba na baada ya kufahamiana akamueleza kilichompeleka pale, Mzee duba alifurahi sana kusikia amechaguliwa kuwa mganga anaetakiwa kutatua lile tatizo lililopo pale kijiji, akamuomba yule kijana ile siku walale pale alafu asubuhi na mapema waanze safari yao ya kwenda kwa mfalme. Wakati huo Duba alikuwa Hafahamu kitu chochote kinachoendelea juu yake. Masaa yalienda na hatimae mda wa kulala ukafika Duba akamuandalia yule kijana sehemu mzuri ya kupumzika, na yeye akaenda kulala sehemu yake, mda huo kwa upande wa sube na mke wao walikuwa wakijiandaa kwenda kuifanya kazi walio ikusudia kuifanya siku ile. Mda wa kazi ulipofika wakakusanya vitu vyao na kuweka kwenye ungo kisha na wao wakapanda na kusafiri mpaka nyumbani kwa Duba na kumkuta akiwa amelala fofofo. Walipofika wakamwaga unga huku wakiizunguka nyumba na mwisho wakashikana mikono na kuingia ndani kwa kutumia ukuta. Ghafla sura zao zikabadili na kuwa tofauti ambazo mtu yoyote isingekuwa rahisi kuwafahamu, Wakaanza kuimba na kucheza nyimbo zao za kichawi huku wakizunguka kitanda cha ukambaa alicholalia Duba, Walipomaliza wakamwamsha kwa mkitikisa mpaka alipozinduka kutoka usingizini. Duba alishtuka sana alipokutana uso kwa uso na wawili wale waliokuwa na sura za kutisha, akakurupuka pale kitandani na kuangukia chini. Wawili wale waliendelea kumfuata mpaka huku yeye akiwa anarudi nyuma nyuma, na mwisho akasimama na kukimbilia nje, Ghafla nje ya nyumba mulipo mwagiwa ule unga mkaanza kuwaka moto na kumfanya Duba ashindwe kuendelea kukimbilia mbali na pale. Akadondoka chini huku akitafuta wapi wale watu walipo, Ndipo sube na mke wakatokea pale pale alipokuwa ameanguka ndipo Duba akaanza kuwauliza maswali wawili wale huku kijasho kizito cha kujuta kikimtiririka. MGANGA: Kwani munataka nini kwangu kama kuna kitu munakiitaji niambieni mimi nitawapatia. Yule mganga baada ya kusema vile ndipo mzee sube akaanza kucheka kwa dharahu na kumjibu. MZEE SUBE: Hahahaha wewe si mganga ambae unataka ukaaribu mambo yangu. Sasa nimekuja kwa ajili ya kupambana, uwezo wako ndio utakufanya uendelee kuishi . Sube baada ya kujibu vile ndipo Duba akagungua kuwa ni mzee sube, maana walikuwa pamoja zamani kwenye shughuli zao za kichawi lakini baadae Duba akaacha kuloga watu na kuwa mgawa, chapokuwa nae ni mchawi. MGANGA: Nimekujua wewe sube na mimi nilijua tu lazima hipo siku utanifanyia kitu kama hiki maana umezoea kuwatesa wanakijiji. kama unataka kuniua niue tu ila endapo utaniacha nitasema ukwel kwa mfalme. Sube alichukia sana kusikia vile, ndipo akajibadirisha na kurudi kwenye sura yake ya kawaida na kusogea karibu na alipo Duba na kuanza kuongea. MZEE SUBE: Vizur sana kama umegundua mimi nani sasa kwa kuwa unajfanya jeuri basi leo ndio utakuwa mwisho wako wa kuonahuu ulimwengu, kamwe sitakuacha hai. MGANGA: Sawa wewe fanya utakalo lakini jua kuwa siku za mwizi ni arobaini hipo siku ukweli utajurikana tu hata kama utaniua. Sube akasimama akamkazia macho Duba ghafla damu zikaanza kumtoka puani mdomoni na masikioni, huku akiangaika kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayapata hatimae akakata roho. SEHEMU YA 8

at 1:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top