Home → simulizi
→ JINA: NYOKA WA KUTUMWA
SEHEMU YA 6
………………. Ilipoishia …………………………
MZEE.1: Mfalme tumekuja hata tunashida ya kuzungumza na wewe.
MFALME: kuweni huru wazee wangu mimi ninawasikiliza.
MZEE 2: Mtukufu mfalme sisi tumekuja hapa kwa ajil ya kuongelea kuhusu hili tatizo lilokumba hiki kijiji chetu cha mbaka kwasasa.
MFALME: Tatizo gan tena ?
MZEE 3: kuhusu huyu nyoka ambae amekuwa akisumba sana hapa kijijini kwetu.
MFALME: kweli huyu nyoka kwa sasa amekuwa tishio hapa kijiji kwetu ila mimi nimepata maelezo yote kuhusu huyu nyoka.
MZEE 2: Kwahiyo umeamua kufanya nini baada ya kujua kuhusu huyu nyoka.
Mfalme kabla ajajibu mara mzee sube akafika maana alipelekewa taarifa kuhusu kikao kilichopo kwa mfalme, mfalme baada ya kumuona mzee sube alijkuta na yeye akiwa anamtete yule nyoka.
……………….. Endlea ……………………………………
MFALME: KwelI huyu nyoka ni hatari sana ila hatakiwI kuwindwa maana atakuwepo hapa kwa mda tu na baadae ataondoka.
Maneno ya mfalme yaliwashangaza sana wale wazee maana wao walitarajia kuambiwa yule nyoka atafutwe na hauawe ila mfalme alisema kinyume kabisa na mawazo yao. Ila kwa upande wa mzee sube alifurahi sana kusikia mfalme akisema vile alijua moja kwa moja kafankiwa kuteka ufahamu wa mfalme. Wale wazee waliendelea kuongea huku mzee sube akiwa anawahudumia wagonjwa.
MZEE 1: Kwahiyo itabidi tuvumilie tu. angaliania mtukufu mfalme watu wanavyo umia ila kwa kuwa umeamua hivyo sawa sisi tumekulewa.
Wakamuaga mfalme na kuondoka zao huku wakiwa wamesononeka kutokana na jibu ambalo alikuwa ametoa mfalme. Siku hiyo mzee sube aliendea kufanya kaz yake na hatimae akamaliza na kurudi kwao na ile siku ikawa imepta. Siku kadhaa zilipita huku watu wakiwa wanaendelea kupata tabu na nyoka aitwae yoka ambae katumwa na mzee sube kwa ajili ya kijtafutia umaharufu pale kijijini kwake. Siku moja mchana kulikuwa na vijana kama watano wakiwa wanatembea wakielekea shambani kwao ghafla mmoja wao akang'atwa na yoka. Kitendo kile kiliwakasilisha sana wale vijana wengine na ndipo wakaanza kumkimbiza Yoka huku wakiwa wameshika fimbo na wengine panga pamoja na mawe. Vijana hao walijitahidi sana kumkimbiza lakini baada ya kumkaribia ghafla yoka akaingia kwenye kichaka Fulani, wote kwa pamoja wakakizunguka hiko ili nyoka asitoke sehemu ile na kuanza kuishambulia kwa kupiga mawe pamoja na zile fimbo walizobeba. walipomaliza kufanya hivyo mmoja kati yao akaanza kukatakata kile kichaka wakiamini wamefanikiwa kumuua yoka lakini kwa bahati mbaya waliambulia patupu. Walijiuliza mda gani nyoka ametoka maana hawakutegemea kuona kile walichokiona, lakini halikupatikana jibu zaidi ya kutazamana na kusikitika kumkosa adui wao mkubwa. Wakaondoka na wakarudi mpaka kwa yule mwenzao kisha wakamchukua na kumpeleka nyumbani kwa mzee sube kwa ajili ya kumfanyia matibabu, walipokelewa vizuri ndipo mzee sube akaanza kuwauliza tatizo japokuwa alikuwa anajua alifanya hivyo ikiwa kama kuwapumbaza na wasihisi kitu chochote kuhusu yeye na yule nyoka.
MZEE SUBE: Vijana huyu mwenzenu kapatwa na nini.
kijana mmoja akaanza kumsmulia jinsi ilivyokuwa.
KIJANA 1: Tulikuwa tunaenda shamban ila kwa bahati mbaya akatokea nyoka na kumbana mwenzetu, tukajitahidi kumkimbiza ili tumuuwe lakini kwa bahati aliingia kwenye kichaka na kutupotea kwa mzingra ya kutatanisha ndipo tukamchukua huyu mwenzetu na kumleta huku kwako kwa ajili ya kumfanyia matibabu.
Mzee sube alichukia sana aliposikia wale vijana walihitaji kumuua nyoka wake, akaingia ndani kuchukua dawa na kumpatia mgonjwa, Wale vijana walifurahi sana wakitegemea kumuona mwenzao akirudi kwenye hali yake ya kawaida. Mda mfupi wakielekea majumbani kwao hali ya mwenzao ikabadilika na kuwa mbaya zaidi ya mara ya kwanza, haraka waligeuza na kurudi nyumbani kwa Sube na kumkuta akiwa amekaa na mke wake, wakamueleza jinsi hali ya mwenzao ilivyobadilika, mda huo mgonjwa alikuwa amelazwa chini huku akipwitapwita kama kuku aliepigwa jiwe kichwani au kuchinjwa. akiwa kwenye hali ya kuangaika na maumizu makali ghafla alimuona nyoka mkubwa akiingia kwenye kichaka kilichokuwa karibu na nyumba ya mzee sube. Alitamani awaambie wenzake lakini kwa kuwa alikuwa mahututi alishindwa kuongea na kubaki akimuangalia Yoka kwa hasira mda mfupi mbele akakata roho, kumbe mzee sube aliwapa dawa tofauti ya kutibu sumu ya nyoka, alifaya hivyo ikiwa kama adhabu kutokana na kitendo walichokifanya cha kutaka kumuua Yoka. Jambo hilo liliwaumiza sana wale vijana na kuwa na hasiri ya kumtafuta yule nyoka kwa hudi na uvumba bila kujua kuwa mda ule alikuwa karibu yao. Wakamchukua yule mwenzao na kwenda kumzika kisha wakaenda mpaka kwa mfalme kwa ajili ya kuomba kufanya mkutano wa kijiji kizima kwa ajli ya kupanga mipango ya kumuangamiza yule nyoka. Walipofika wakamueleza shida yao na hatimae mfalme akawakubari ndipo ikapangwa siku rasmi ya kufanyika huo mkutano. Siku hiyo ilipofika watu walikusanyika kwa wingi nyumbani kwa mfalme maana kila mtu alipata taarifa ya kuwepo kwa hiko kikao na alichoshwa na matatizo wanayoyapata kutoka kwa huyo nyoka. Mda ulipofika kikao kikaanza huku viongozi wote wa kijiji wakiwemo bila kumsahau mzee sube, Mfalme akasimama kuanzisha mkutano rasmi.
MFALME: Ndugu wanakijiji cha mbaka tumekutana hapa kwa ajili ya kujadiri hili swala lilitupata ambalo limekuwa likitunyima raha pia limetufanya tusiishi kwa maani . Nahisi wote munajua nini tatizo lilipo hapa kijijini kwetu kwa sasa kwahiyo kuanzia sasa hivi nafungua mkutano rasmi na nani ruhusu mtu kutoa wazo pia na ruhusu mtu kupinga wazo ila kwa viongozi tu.
Mfalme akaa chini huku watu wakiwa wanampigia makofi kutokana na kile alichokiongea, mzee mmoja akasimama na kuanza kutoa mawazo yake.
MZEE: Mtukufu mfalme nina wazo moja kama litakuwa zuri naomba lifanyiwe kazi. Mimi ninaona bora huyu nyoka tumtengeneze mtego ambao utamnasa kama tulivyofanya kwa baadhi ya watutu hatari ambao walikuja hapa kijijini kwetu, hilo ndio wazo langu.
Mzee aliposema vile watu wote walipiga makofi mpaka na mzee sube mwenyewe, zamu za viongozi kukubali au kupina ikafika, kila kiongozi aliko mbele aliongea na kulikubali lile wazo mpaka mzee sube maana alikuwa anajua hakuna awezae kumtega Yoka akafanikiwa kumpata, lakini mke wake alishangaa kuona Sube akilikubali lile wazo maana yeye alikuwa afahamu nini mume wake aliwaza. Mtu mwingine akasimama kutoa wazo lake.
KIJANA: Mtukufu mfalme wazo langu ninaona bora ikifika usiku tuanze kumtafuta maana yeye uwa anadhuru sana usiku kuliko mchana kwahiyo inamaansha kuwa usiku ndio rahisi kumpata, hilo ndio wazo langu.
Mzee sube baada ya kusikia vile akasimama na kuanza kuipinga lile wazo la ya yule kijana maana aliona wakifanya hivyo itakuwa rahisi sana kumkamata yoka maana huwa anaenda mbali sana na eneo lake majira ya usiku kwahiyo wanaweza kumkimbiza na hatmae wakamkamata. Baadhi ya watu walishangaa kuona mzee sube amepinga lile wazo ila mfalme aliona kawaida maana alikuwa anamsikiliza sana mzee sube.
MFALME: Jamani wanakijiji huyu ndie tabibu wetu pia ni mzee wetu kwahiyo yeye anajua mambo mengi kuliko sisi ni vizuri endapo akisema kitu tumsikilize maana hata mimi nimeona hilo wazo sio zuri kwetu.
Vijana wengi walisikitika kusikia mfalme akiumuunga mzee sube, ndipo kijana mmoja akasimama na kuanza kutoa wazo lake.
KIJANA 2: Mtukufu mfalme pamoja na wanakijiji wote wazo langu naona tungepita kila sehemu kwenye kichaki tuviondoe maana tukifanya hivyo nyoka hatakuwa na sehemu ya kakaa na atakuwa anazunguka zungika na ndio itakuwa rahis kumuua.
Wazo la huyo kijana lilipendwa na kila mtu mahara pale mpaka mfalme mwenyewe lakini ilikuwa tofauti kwa mzee sube, maana hakupiga makofi kuonyesha kuunga mkono lile wazo wala kutabasamu jambo ambalo liliwashangaza sana viongozi wenzake. Mfalme akasimama na kumpongeza lile wazo lilitolewa.
MFALME: Kijana hongera sana kwa kutoa wazo zuri kiasi hiki nimefurahi sana na tutaanza kulifanyia kazi wazo lako ili tuone mafanikio yake.
Mfalme akaa na kupisha viongozi wengine waonge kuhu lile wazo, kila aliesimama alilipongeza na kushauri lianze kufanyiwa kazi wazo hilo lakini ilikuwa tofauti ilipofika zamu yam zee sube kutoa maoni yake juu ya wazo lile.
MZEE SUBE: Jaman mimi nilikuwa sijui kuwa vijana wa hiki kijiji chetu ni wajinga na wapumbavu kiasi hiki yani wanapitwa mawazo na wazee. Hivi unaonaje mtu aje nyumbani kwako kuaribu nyumba yako utamuacha kweli hata kama atakuwa na upanga lazama utajitahidi kadri uwezavyo kumzuia kufa hivyo hii ndio itakavyokuwa kwa hiyo siku mutakayo anza kuondoa hivyo vichaka . maana yule nyoka awezi kukubali kuona munaharibu nyumba yake kwahiyo ataanza kuwauma na hatimae mukapata madhara ya kujitakia.
Watu walibaki vivywa wazi maana hawakutegemea kusikia maneno yale kutoka kwa mzee sube, Kikoa kiliendelea na mwishowe wakaamua kufanya kama alivyosema mtu wa kwanza kutoa wazo, wakachaguliwa vijana shupavu mashujaa mahodari kwenye masuara ya utegaji mitego na kuwapa kazi na hatimae kikao kikafika mwisho.Siku ya pili ilipofika wale vijana waliochaguliwa kuifanya kazi wakachukua zana zao za kutengenezea mtego na kwenda nao sehemu ambayo ilisemekana huyo nyoka kufika mara kwa mara. Walitega huo mtego kisha wakamchukua mbuzi na kumuweka ikiwa kama chambo cha kumuitia nyoka, Walipomaliza wote wakaenda kujificha kusubilia nini kitatokea, lakini matumaini makubwa ya kufankiwa yakiwa juu yao, wakaa kimya wakisikiliza kwa makini ili wasikie pindi mtego ukifyatuka. Zilipita dakika kadhaa ghafla mbuzi ambae aliwekwa kwenye mtego akaanza kulia kwa sauti ya kuashiria amepatwa na tatizo, wale vijana wakaa vizuri huku wakiwa wameshika mapanga wakisubilia kusikia mtego ukifyatuka, sekunde kadhaa mbele mtego uliskika, haraka walitoka walipojificha na kuelekea kwenye mtego wao wakiwa na mawazo ya kumkuta nyoka akiwa amenasa kwenye mtego wao. Walishangaa kukuta mtego ukiwa umefyatuka huku yule mbuzi akiendelea kula majani, wakaukagua vizuri na kukuta ukili ukiwa umenasa kwenye mtegeo, wakautoa na kuutupa pembeni na kuanza kuongelea jambo lile.
KIJANA 1: Jamani nini kimetokea hapa maana sielewi mbona mtego umefyatuka na hakuna kitu kilichonaswa.
KIJNA 2: Hata mimi nana shangaa jambo hili, au kuna mtu ametuchezea.
KIJNA 3: Nahisi maana tangu nianze kutega hii mitego sijawai kuona ikifyatuka nyenyewe bila kunasa kitu.
KIJANA 4: labda kuna kitu kiligusa huu mtego . Kama vipi tutege tena alafu tukajifiche na tuangalie kama itatokea tena .
Wakatega tena kisha wakaenda kujificha bila kujua kuwa walifanikiwa kumnasa wakiemtaka na kumtoa wenyewe kwenye mtego na kumuacha huru tena. Walipoenda kujificha tena, Yoka akarudi kwenye umbile lake ya nyoka na kurudi nyumbani kwake.
SEHEMU YA 7
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: