Home → simulizi
→ Riwaya: SARAI
SEHEMU YA TISA(09)
***Ilipoishia***
ghafla aliona kuna pikipiki ikipita kwa mwendo wa kasi huku imembeba mwanamke kwenye kiti cha nyuma....baba sarai hakumtambua salome kwa sababu ilikuwa ni usiku...... hakujali aliendelea kuzipiga hatua kuelekea nyumbani kwake baada ya muda alifika.....akafungua mlango akazipiga hatua kuelekea chumbani.......
***Endelea***
alistaajabu kukuta mlango wa chumbani upo wazi, akaingia haraka upande wa ndani alipoangaza macho hakumuona salome , akajipa moyo huenda kaenda chooni kujisaidia akaweka ile mifuko miwili iliyokua na chipsi kuku juu ya meza kisha akajitupa kitandani kumsubiri salome, dakika zilizidi kusonga na hatimae ni dakika kumi sasa zimepita; wasiwasi ukaanza kumuingia baba sarai akaamua kutoka nje kuelekea chooni alipo ukaribia mlango aliita kwa mara kadhaa lakini salome hakuitika ,akaamua kuufungua mlango alistaajabu kutokumuona salome"mmmh! inamaana itakua kaenda wapi? bila kuchelewa baba sarai alizipiga hatua za haraka haraka kurudi chumbani akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani, alipofika chumbani alitazama pale lilipokua begi lenye pesa zake, macho yalimtoka akaanza kupiga mayowe...................."uwiiiiiiii, uwiiiiiiiii! jamani nimeimbiwa alisema maneno hayo huku machozi yakimtoka, akatimua mbio kutoka upande wa nje hakumuona salome alitembea kona zote za mitaa lakini hakufanikiwa kumpata bahati mbaya zaidi alikua hapafahamu ni wapi salome anapoishi baba sarai alikata tamaa akaamua kurudi nyumbani kwake, alipokua njiani alikutana na maaskari wakifanya doria kutokana na wasiwasi mkubwa aliokua nao sarai maaskari walihisi huenda ni muarifu ,wakaamua kumusimamisha baba sarai kisha mmoja kati ya maaskari hao akaanza kumuuliza maswali baba sarai"tunaomba utuoneshe kitambulisho chako cha uraia ama kitambulisho chako cha kazi....wakati huo baba sarai alikuwa kimya.. alikuwa asikilizi maswali aliyokuwa akiulizwa!!!akili yake ilikuwa inawaza kuhusu pesa zake...maaskari walimtilia masha baba sarai...wakamkamata na kumpeleka kituo cha polisi....
********************
upande mwingine alionekana salome akishuka kutoka kwenye bodaboda...huku amelibeba lile begi lililokuwa na pesa pamoja na baadhi ya nguo za baba sarai.. akamlipa dereva bodaboda kisha akaondoka zake kuelekea kwenye nyumba ya kulala wageni(Gest house) akakodi chumba akalipia pesa...
***************
Asubuhi palipokucha salome alidamka mapema akajiandaa kwenda kwenye kituo cha mabasi ili aende Dar es salaam....
kule kituo cha polisi alionekana baba sarai akiwa na huzuni kubwa aliwaza pesa zake....kila alichoulizwa yeye alijibu pesa zangu....maaskari waliamua kumuachia huru kwa kudhani huenda baba sarai anaugojwa wa akili....
alipoachiwa alitimua mbio mpaka kwenye saloon aliyokuwa anafanya kazi salome....alipokaribia kwa mbali aliona mlango wa saloon upo wazi akaongeza kasi ya kukimbia akapitiliza mpaka ndini...wateja waliokuwemo mule walimshangaa baba sarai....kisha msusi mmoja akauliza ""we kaka vipi kulikoni unaingia na viatu wakati unaona watu wote tumevua viatu mlangoni!!!!
baba sarai akaropoka""salome yuko wapi??
yule msusi akajibu salome gani??
baba sarai akadakia ""yule mwenye saloon hii.
yule msusi akajibu ""mimi ndio mwenye saloon hii...na salome ni mfanyakazi wangu lakini tangu Jana usiku hajarudi nyumbani.
baba sarai akadakia na kusema ""uuuwiiiii pesa zangu jamani nimeibiwa wale watu walizidi kumshangaa baba sarai kisha wakasema kwa pamoja""mjini shule jembe peleka kijijini..
kabla hawajamaliza kusema baba sarai alitimua mbio kwenda kushtaki polisi kuwa ameibiwa....
alipofika alianza kutoa maelezo yake....wale Maaskari waliangua kicheko kisha mmoja akasema""wewe si niyule mtu uliyekamatwa jana uzururaji??? askari mwingine akadakia "" mimi nilisema huyu ni chizi (mwehu) nyinyi mkasema tumkamate unaona sasa amekuja mwenyewe kudhihirisha kuwa ni mwehu....anasema jana usiku kaibiwa wakati tangu jana alilala hapa kituo cha polisi katoka asubuhi sasa kaibiwa saa ngapi!!!!!???
baba sarai alipojaribu kujieleza walimkatisha kauli na kumfukuza...baba sarai alitoka kituoni hapo huku akiwa amejishi kichwani....alizioiga hatua huku analia njia nzima mpaka akafika nyumbani kwake....
wakati huo huo salome alikuwa bado anajiandaa
alikuwa bado yupo bafuni anaoga katika hiyo nyumba ya kulala wageni.....sarai alijitokeza kisha akachukua lile begi na kitowekanalo kimiujiza na kutikomea kusikojulikana....salome alipomaliza kuoga alitoka bafuni kisha akaanza kuvaa nguo zake alipomaliza alifungu kabati ili alitoe begi aondoke zake...akafungua mlango wa kabati ..macho yakamtoka kwa mshangao!!!!! hakuliona begi lile akazipiga hatua za haraka haraka mpaka mlangoni....alipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo alijiuliza ni nani aliyetoa hilo begi ndani ya kabati!!!!alitafuta chumba kizima hakuliona begi hilo....akakata tamaa kwa sababu hayupo wa kumuuliza ...akaamua kufungua mlango na kutoka nje akaondoka zake kurudi nyumbani kwake...
************
Upande mwingine alionekana sarai kajitokeza ndani ya chumba cha baba yake na kuliweka begi pale lilipokuwa...kisha akatoweka kimiujiza
kule nyumbani kwa magesa alionekana akiwa katika hali ya mawazo alikata tamaa ya maisha alichoka kila siku yeye kuwa ni mtu wa kuletewa misaada ya chakula pamoja na mahitaji mengine....
siku ya leo aliamua kunywa sumu ya kuuwa panya...akachukua sumu hiyo na kuichanganya kwenye chakula
kisha akala chakula hicho..baada ya dakika moja kupita magesa alianza kuumwa na tumbo....akaanza kutokwa na povu mdomoni..
wakati huhuo yule mtu aliye mgonga na gari alikuwa njiani kuja kumjulia hali magesa alipofika alistuka kumkuta magea anagalagala chini huku baiskeli yake ikiwa imedondoka kando...alipomgeuza aliona mapovu yanamtoka magesa akamkimbiza haraka hospitali....walipofika muhimbili madaktari wakasema wamemchelewesha...tayari magesa alikuwa kakata roho muda mchache kabla hajafikishwa hospitali....
***************
upande mwingine alionekana baba sarai akizipiga hatua za taratibu mpaka akafika nyumbani kwake alipoingia chimbani alistahajabu kulikuta begi lake akafungua zipu harakaharaka akatazama upande wa mdani ya begi aliziona pesa zake...""mmh!! inamaana jana sikuangalia vizuri au nilikuwa nimechanganyikiwa!!!!!?? baba sarai hakujali akafunga zipu ya begi nakuliweka uvunguni mwa kitanda mara ghafla alisikia mtu akigonga hodi..
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ASANTENI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: