Home → simulizi
→ Riwaya: SARAI
SEHEMU YA NANE(08)
***Ilipoishia***
upande mwingine alionekana baba sarai akiwaza sana nini afanye ili heshma yake irudi kama zamani....aliamua kuuza nyumba yake..ili aondike na kuhama jiji la dar es salaam aende mikoani akanunue mashamba aanze kulima mazao ya chakula....
***Endelea***
akaandaa mpango wa safari akaamua aende kilosa kulima mpunga...alipofika kilosa alifikia gest akakaa hapo kwa muda wa mwezi mmoja huku akitafuta nyumba ya kupanga....alifanikiwa kuoata nyumba yenye vyumba viwili na sebule. akalipia kodi ya kukaa hapo mwaka mzima.....baba sarai alitafuta mashamba akanumua akaanza kulima...
sikumoja akiwa kwenye matembezi alimuona mwanamke mmoja aitwae SALOME aliyekuwa akifanya kazi kwenye saloon ya kike ....alivutiwa nae akahisi kumpenda.....aliamua kumfuata akajifanya anaulizia kama mtaa anaoishi salome kuna vyumba vya kupanga...salome alisema"" nitajaribu kuulizia nikipata nitakufahamisha niachie namba yako ya simu...baba sarai alikuwa badi hajanunu simu..ilibidi yeye ndio achukue namba ya salome....
salome alichukua karatasi na kalamu kisha akaandika namba yake ya simu na kumkabidhi baba sarai....
baba sarai alipotoka hapo alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye duka moja lililokuwa likiuza simu....akachagua simu kisha akalipia pesa na kuondoka zake...
baada ya siku mbili kupita baba sarai alimpigia simu salome kisha akajirambulisha...punde salome alimkumbuka....baba sarai alimuomba salome kuwa jioni waonane anataka wale chakula cha jioni pamoja sehemu yoyote aitakayo salome..
salome alikubali.. ..
ilipofika majira ya saa moja za usiku salome alidunga saloon na kumpigia baba sarai...wakakutana katika hoteli moja hapo mjini kilosa....walipomaliza kula chakula..walianza kunywa pombe...... baada ya lisaa limoja pombe zilianza kumkamta baba sarai .....alianza kumchombeza salome kwa maneno ya kimapenzi....salome alichanganyikiwa kuona baba sarai akiagiza bia anatoa noti za elfu kumi kumi tu alafu anamwambia muhudumu abaki na chenji...salime alianza kumtamani baba sarai kwa sababu ya pesa zake....aliamua kumkubalia ombi lake... wakaanzisha mahusiano ya kimapenzi..
sikumoja salome aliamua kutofungua saloon ilikuwa ni siku ya jumapili....aliamua kwenda nyumbani kwa baba sarai..alioofika alikaribishwa na baada ya muda walihamia chumbani....punde baba sarai alimuaga salome kuwa anakwenda kuoga kisha akatoka chumbani.....salome aliipo angaza angaza macho aliona begi likiwa wazi limejaa noti za shilingi ifu kumi kumi.....salome alioagawa akaandaa mpango wa kuziiba pesa zile akimbie nazo......
kabla hajazichukua alitoka nje ili aangalie kama baba sarai bado yumo bafuni au kashamaliza kuoga ili aibe pesa hizo. ile anatoka akakutana uso kwa uso na baba sari....salome alistuka huku macho yake yakionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.....kisha akasema """nilikuwa nataka nije huko bafuni nikuogeshe...baba sarai alitabasamu na kusema asante mpenzi usijali nimeshamaliza kuoga....siku nyingine utaniogesha...
waliingia chumbani wakkaanza kupiga stori huku salome akicheka kicheko cha mahaba...
ilipofika usiku salome alisema ""leo nitalala hapa nyumbani kwako baba sarai alifurahi sana wakawasha runinga(TV) kisha baba sarai akaweka CD kwenye deki na kuanza kutazama filamu ya kitanzania iitwayo NZITA....baada ya dakika kadhaa baba sarai alimuuliza salome """unajisikia kula chakula gani mpenzi???? salome alijibu kwa sauti ya kimahaba ""Chipsi kuku mpenzi.....baba sarai alinyanyuka kutoka kitandani akavaa suruali kisha akatoka nje ili akalete chakula hicho...kwa sababu mtaa aliokuwa akiishi hakuwepo mchoma chipsi hata mmoja hivyo alilazikmika kwenda mbali kidogo.....
wakatibaba sarai katoka salome alinyanyuka haraka na kuvaa nguo zake kisha akalichukua lile begi lililokuwa linapesa zote za nyumba aliyokuwa kaiuza baba sarai......salome alizipiga hatua za harakaharaka na kutokomea kusiko julikana....
************
uoande mwingine alionekana baba sarai akitoa noti mbili za shilingi elfu kumi kumi akamkabidhi yule mchoma chispi kisha akafungiwa kuki mzima na chipsi mbili.....akapoke na kuianza safari ya kurudi nyumbani kwake.....ghafla aliona kuna pikipiki ikipita kwa mwendo wa kasi huku imembeba mwanamke kwenye kiti cha nyuma....baba sarai hakumtambua salome kwa sababu ilikuwa ni usiku...... hakujali aliendelea kuzipiga hatua kuelekea nyumbani kwake baada ya muda alifika.....akafungua mlango akazipiga hatua kuelekea chumbani.......
ITAENDELEA......
usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua.
ASANTENI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: