Riwaya: SARAI SEHEMU YA SABA(07) ***Ilipoishia*** wakati huohuo alionekana sarai akiwa katika mlima mmoja.. ameketi juu ya jiwe huku akipuliza filimbi yake iliyokuwa imetengenezwa kwa mfupa wa binadamu....kisha akasimama... mara ghafla akatoweka kimiujiza... ***Endelea*** akatokomea kusikojulikana.... upamde mwingine walioneka wale wateja waliopeleka viatu vyao kwa ajili ya kusafishwa..walisubiri mpaka wakachoka walianza kuondika mmoja mmoja... *********** ule upande mwingine alionekana baba sarai akiwa sero mara ghafla aliona mlango ukifunguliwa bila kumuona mtu anaye ufungua baba sarai hakujali alihisu huenda mlango haukufungwa kwa ufunguo......punde alimuona askari akimfuata na kuondoka nae mpaka nje kabisa ya kituo cha polisi..na kumwambia aondoke zake...baba sarai alihisi askari huyo anamtania....akaanza kuzipiga hatua alipo ona askari yule hamjali..alitimua mbio....baba sarai alipokimbia hatua mbili aligeuka nyuma hakumuona askari yule.....baba sadai hakujali aliendelea kutimua mbio...alikimbia mpaka nyumbani kwake......alipofika alistahajabu kukuta watu wawili wame kaa nje ya mlango wake..alistuka sana alipotazama kwa makini aligundua kuwa ni meneja na muhudumu wa baa nyingine miingoni mwa baa alizokopa pombe... baba sarai alikatisha kona haraka akaingia kwenye uchochoro......akazipiga hatua za haraka haraka huku sura na macho yake yake yakionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.....akiwa njiani ghafla alimuona yule mtu aliyeleta viatu visafishwe baba sarai alichanganyikiwa akageuza shingo yake na kuangalia pembeni huku akionekana kama anashangaa kutazama kitu fulani....wakapishana...yule mtu alitaka kumuuliza lakini alisita..akadhani huenda kamfananisha na yule fundi viatu.....baba sarai aliendelea kuzipiga hatua alipokimaliza kichochoro mara ghafla alimuona yule mmiliki wa baa aliyempeleka kituo cha polisi. na kumfungulia mashtaka ya madai... baba sarai alizidi kuchanganyikiwa....akajiuliza moyoni ""ninamkosi gani mimi...ee mungu nimekukosea nini mbona nakutana na mitihani na misukosuko kila siku!!!!!!ghafla yule mmiliki wa baa alikutana na mtu aliyefahamiananae wakati huo sarai anamfatilia kwa nyuma lakini baba sarai hakuweza kumuona sarai kwa macho ya kawaida......baba sarai aliendelea kuzioiga hatua bila kujua ni wapi anaelekea......alijikuta katokezea ule mtaa aliokuwa anafanyia kazi ya kushona viatu alipotahamaki alistuka kuina yuoo eneo hilo akataka kukimbia lakini alipotazama ule upande ilipokuwa ofisi yake ya kushona viatu...hakuwaona wale watu waliokuwepo wakimsubiri...akaamua kuzipiga hatua za harakaharaka kuondoka eneo hilo na kutokomea kusikojulikana.... **************** ule upande mwinginealionekana magesa akiwa hospital ghafla simu ya mtalaka wake ikaita...akazipiga hatuakuelekea nje magesa alipojaribu kumuita alishindwa sauti ilikuwa chini sana kutokana na maumivu makaliupande wa ubavuni.....mtaraka wake alipotoka nje kuingea na simu hakurudi tena wodini.....hivyo aliondoka hata bila kuonana na mtalaka wake magesa....magesa alianza kulia kwa uchungu huku akimuomba mungu"""ee mungu nina mkosi gani mimi... magesa alilia sana.....kwa sababu hakuwa na msaada roho ilimuuma sana alipokuwa akiona wagonjwa wenzake waliolazwa wodi moja....wakikitembelewa na ndugu na jamaa zao...isipokuwa yeye...... *******BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA****** Magesa alipata nafuu akaruhusiwa kutoka hospitali....yule mtu aliyemgonga na gari alikuwa akimuhudumia magesa kipindi hicho chote pamoja na gharama za matibabu...alikuja na baiskeli ya walemavu na kumkabidhi magesa kisha akamuingiza ndani ya gari na kumpeleka nyumbani kwake...wakiwa njiani magesa alilia sana kila alipokuwa akiitazama miguu yake....alilia mpaka akamkufuru Mungu kwa kusema"" kwa nini umeniacha hai ni bora ungechukua roho yangu kuliko haya mateso ninayota...... ********** upande mwingine alionekana baba sarai akiwaza sana nini afanye ili heshma yake irudi kama zamani....aliamua kuuza nyumba yake..ili aondike na kuhama jiji la dar es salaam aende mikoani akanunue mashamba aanze kulima mazao ya chakula.... ITAENDELEA...... usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua. _sehemu ya nane(08) Jumatatu tutakutana hapa hapa endelea kuinjoy_ ASANTENI.

at 8:39 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top