Home → simulizi
→ Sitaki Tena - 01
(season 1)
Nakumbuka Levina mimi nilikuwa na miaka 12,wazazi wangu walikuwa wakinipenda
sana na walipenda kuniacha huru hata pale ninapokuwa nacheza na rafiki zangu michezo
mbalimbali,nilikuwa napenda sana kucheza michezo tofauti na wenzangu c unajua tena utoto,na mchezo mkubwa niliokuwa naupenda ni huu wa rede (ule wa kukwepa mpira unaporushiwa).
Siku hiyo nikiwa mimi na rafiki zangu tunacheza,sikuamini macho yangu na ni vigumu
kuamini mpaka sasa kwa kile nilichotenda kwani badala ya kuuokota mpira nirushe kwa ile
haraka niliyokuwa nayo ndani ya ule mchezo nilijikuta naokota jiwe bila kujitambua nilichokuwa
nimeokota huku nikidhani kuwa ni mpira na kumrushia Jeni na kwa bahati mbaya lilimpata Jeni
kichwani na kuzimia palepale.. Juhudi zilifanywa haraka haraka na majirani huku mimi nikiwa
pembeni cijui cha kufanya mchozi ukinitiririka huku kijasho chembamba kikipenyeza katika
paji la uso wangu kupitia shingoni huku lile jasho likichochea mkojo ulioanza kunitoka taratibu palepale huku nikitazama kinachoendelea..
"Panda na wewe twende.. Nimesema panda huko usikii.?"
Aliongea na mimi mama mmoja kwa ukali huku akinitolea mijicho kana kwamba labda alikuwa ni mtoto wake lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa ni mpita njia aliyekuwa shuhuda wa lile tukio.
Nilipanda taksi pamoja na wale majirani iliyokuwa imekodiwa haraka kwa ajili ya kumkimbiza
Jeni hospitali.. kadri tulivyokuwa tunakaribia hospitali ndivyo mapigo yangu ya moyo yalinienda kasi mithili ya yule mwanariadha wa jamaika anayeitwa 'Bolt'... Huku nikiomba miujiza yeyote itokee ili Jeni apone turudi nyumbani, niliendelea kulia tena kwa sauti ya juu huku kamasi likinitoka.. Tulipokaribia kufika hospitali nilisikia mama mmoja aliyekuwa
pembeni yangu akimshikilia Jeni..akitikisa kichwa huku akimwambia dereva apunguze mwendo kwani haina haja tena kuwahi huku akimsisitizia kuwa mtu waliyekuwa wakimuwaisha ameshapoteza maisha..
"Jeni amekufaaa.. Amekufaaa.. Hapana.. hapana.. Mama yangu weeee...mama..baaabaaa uko
wapi jamanii mama yangu weee..."
Nikazidisha kupaza sauti kwa kulia niliposikia yale maneno..
Sikuweza kuamini kama kweli Jeni amekufa mpaka nilipoona tunaelekea mochwari ndipo nilipoamini Jeni alikuwa tayari keshapoteza maisha kutokana na kupoteza damu nyingi zilizokuwa zikimtoka eneo la kichwani na puani.
"Umeshaua..? Ndio umeuwa naongea na wewe kinyago uliyefanya makusudi haya..!”
Aliongea yule mama..
"Sijau.. Kabla sijamalizia kujibu nikashangaa napigwa kofi kubwa la usoni mpaka nikajihisi
kizunguzungu, huku akiendelea kuniambia..
“tena ishia hapohapo mwanaidhaya mkubwa wewe na tunakupeleka polisi moja kwa moja mbwa we ukaozee huko huko ndio utanyoka...!"
Taarifa za mimi kufanya lile tukio tena kwa bahati mbaya lilitawanyika Mtaani kote na hakuna hata mmoja aliyeweza kuamini kwani taarifa hata zilipofikiwa wazazi wangu nao hawakuweza kuamini kilichonitokea walikuja pale kituoni japo kunitoa kwa dhamana lakini ilishindikana kwani huwa hakuna dhamana kwa kesi yoyote ya mauaji.. Nilishiwa nguvu,na kulegea viungo vyote na kusababisha kupoteza fahamu kutokana na kukataliwa dhamana..
BAADA YA SIKU (NNE).4
Sikuweza kupata hata lepe la usingizi takribani siku mbili kutokana na kulia sana,kichwa kiliniuma sana..nakumbuka ilikuwa asubuhi na mapema pale askari alipotuamrisha tupande gari la polisi kutoka pale kituo kidogo cha polisi kurasini na kuelekea kituo kikubwa cha polisi pale MSIMBAZI KARIAKOO.. Safari ilianzia kituo kidogo cha Kurasini nilipokuwa nimechanganywa na wenzangu niliowajua pale pale na wao waliletwa pale kwa makosa tofauti tofauti, huku tukikatiza Sheli ya BP mpaka raundi about ya Kamata,sehemu zote tulizopita bado machozi yalikuwa yakinitoka huku yakiandamana na mafua Makali yalionipata pale kurasini kituoni, kwikwi ilibana sana na haikuwa kwasababu ya kiu ya maji bali ilikuwa ni kwikwi ya kulia kwa mda mrefu..
"Embu nyamaza hukoo.. Haupo kwa baba yako wala mama yako..Tena unyamaze..??”
Aliongea kwa hasira askari mmoja alioonesha kukasirishwa na kitendo changu cha kulia mda
mrefu bila kunyamaza..
"Hivi we mtoto husikii..? Kwani sisi ndo tumekutumauue..?" aliendelea kunikalipia yule
askari. Mpaka tunaingia pale kituoni MSIMBAZI macho yalikuwa mekundu na yamenivimba sana huku sauti ikinikauka kutokana na kulia kwa mda mrefu..
*** ***
Tukiwa katika basi lenye namba PT 10319 ambalo lilikuwa likikatisha mitaa ya kariakoo likiwa linatokea kituo kikubwa MSIMBAZI huku nikiwa katika orodha ya mahabusu waliokuwa wamewekwa pale MSIMBAZI kituoni kuelekea mahakama kuu pale KISUTU kwa ajili ya kusikilizwa kesi yangu kwa mara ya kwanza. kila moja wetu akiwa amefungwa pingu mikononi .,
nywele pamoja na nguo zangu zilikuwa chafu sana kutokana na uchafu wa pale kituo cha Kurasini na msimbazi. Huku basi la polisi likiwa linakata kona ya kuingia mahakamani , nikiangaza huku na huku labda naweza kumuona hata mama au baba,ghafla nikamuona mama
kajifunika kanga upande mmoja wa paji la uso wake kuashiria kuwa alikuwa ameumia upande
mmoja wa uso wake,nilijikuta nikipigwa na afande.
"Embu tembea hukoo... Unashangaa shangaa nini? Kwani hujui kama hapa ni mahakamani...?"
Tukiwa mstari mmoja tulishuka na kuelekea kwenye vyumba ila mimi niliingizwa chumba maalumu kilichoandikwa maneno makubwa mlango wa kuingilia "CRIMINAL ONLY" kwa haraka
haraka sikuweza kutambua lile neno linamaana gani kwakuwa ndo kwanza nilikuwa niko form one ila niliweza kuambulia neno moja tu lililoandikwa "ONLY" kwani nilipenda sana kuangalia ile
tamthiliya ya kifilipino iliyokuwa inaitwa 'only you' nikijua inamaanisha 'Wewe Pekee..'sikuwa mbali na fikra zangu kwani kile chumba kilikuwa peke yake kwa ajili ya kesi za mauaji kama yangu ndo huwa zinasomwa hapa. Nikiwa na mawakili wangu nisiowafahamu ila niliamini tu baba ndo aliwatafuta kwani alikuwa akiongea nao kabla sijaingia mule ndani. Chumba kilikuwa kidogo sana na watu walimiminika wakiwa ni pamoja na majirani,ndugu na marafiki huku kesi ikitaka kuanzwa kusomwa niligeuka nyuma nikajikuta nakutana jicho na mama mmoja..kwa hasira na jazba niliokuwa nayo nikajikuta Natoa fyonyo kali na la kupaza sauti ya juu..Wote mle ndani wakawa kimya ghafla wakinitazama,
"xé@shh.. Mbea mkubwa we..!”
Kisha nikamtemea mate huku hasira zikinipanda kutokea miguuni kuelekea kichwani na
mikononi, nilijikuta nataka kumpiga lakini mikono yangu ilikuwa na pingu hivyo hasira ikazidi mara mbili huku nikihema kwa kasi ikiambatana na makamasi yaliokuwa yakinichilizika mithili ya umande unapokutana na majimaji au konokona anapokuwa anaachia kofia yake..nikanyanyua Mguu wangu wa kulia tayari kwa kumtupia mateke yule mtu..nikawa tayari nimeshathibitiwa.. hakuwa mwingine bali alikuwa ni yule mama tuliepanda naye taksi kumuwaisha Jeni hospitali yule aliyekuwa akinisema ovyo kwenye gari pia ndo alienipeleka
Kunikabidhi polisi..nikiwa naendelea kumtolea macho huku nimekunja uso wangu kwa hasira
mithili ya bi kidude akiwa jukwaani anaimba.. nilijikuta napokea vibao c kutoka kwa yule
mama bali alikuwa ni askari aliyekuwa akifuatilia tukio mule ndani.,
"Hata kesi haijaanza umeanza kuonyesha we nunda eenh... hatimaye hakimu aliingia Na lazima utaozea jela tu wewe.."
Maneno yale yalivuta hisia nyingi sana ndani ya kichwa changu,mwili ulininyong'onyea ghafla,niakanza kutetemeka japo nilikuwa mdogo kiumri lakini nikawa tayari nimeshakomaa kifikra na pia jasiri ndani ya mda mfupi..
******
Mda wa hakimu kuingia mule ndani ulifika,hakuwa mtu wa masihara hata kidogo kwani
aliingia haraka haraka na kuuliza jina langu kamili kisha akaandika andika pale kwenye kitabu
alichokuja nacho na kisha akaniambia kuwa inabidi nirudi tena ndani kwani kesi yangu bado ipo kwenye upelelezi hivyo nitarudishwa tena pale mahakamani baada ya wiki 3 au 4.. Nguvu zilizidi kunipotea,akili nayo ilishajichokea, Nilitoka pale kwa ghadhabu huku askari akiwa nyuma yangu.. nilikuwa na hasira na vitu vitatu, kwanza sijapata fursa ya kuongea na wazazi wangu kwa mda mrefu kwani kwenye kesi kama hizi mtuhumiwa huwa hana hata ruhusa ya kuongea na mtu yoyote, pili nilikuwa na hasira ya kuhairishwa kwa kesi yangu na tatu ni hasira ya yule mama aliojifanya yupo mstari wa mbele katika kunifuatilia kujua mwisho wangu..
"Ole wake siku nikitoka..?"
nilijikuta najisemea kimoyomoyo huku dukuduku likiwa limenijaa moyoni..
"Ipo siku tu.. Atanijua mimi ni nani..?"
nikapanda basi la polisi tayari kwa safari ya kurudishwa tena rumande..
INAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: