Riwaya: SARAI SEHEMU YA TANO(05) ***Ilipoishia*** walipomaliza kula mke wa magesa alimuta chumbani mme wake....akamwambia nataka nikupe pongezi mme wangu kabla sijaifungua hiyo bahasha yani hiyo inaonekana imejaa noti tu.....baada ya zawadi hii niliyokuandalia siku ya leo tukimaliza ndio nitaifungua bahasha hiyo....kisha mke wa magesa alijitupa kitandani....magesa alijua ni zawadi gani mkewe anataka kuumpa...magesa alimsogelea mkewe na kuanza kumpapasa maungo yake ya mwili.... ***Endelea*** baada ya kumaliza mke wa magesa alinyanyuka kutoka kitandani akaenda kuoga....baada ya muda alirudi....alipomaliza kujifuta maji akajifunga kanga kisha akaichukua ile bahasha....magesa alionekana kurabasamu huku akimtazama mkewe kwa macho ya matamanio....alipoifungua ile bahasha aliona makaratasi pamoja na magazeti...akahisi huenda magesa kaweka makaratasi hayo upande wa juu alipoyatoa makaratasi... magesa alistuka sana..mke wa magesa aliendelea kuyatoa makaratasi hayo...... alipoangalia vizuri aligundua kuwa hakuna pesa yoyote...mke wa magesa alikasirika sana akaanza kufoka....wakati huo magesa macho yalimtoka alikuwa kaganda kama kapigwa na shot ya umeme kisha akasimama na kuanza kuangua kilio...mke waagesa alianza kukusanya nguo zake na kuziweka kwenye begi kisha akakusanya nguo za watoto wake akaziweka kwenye mabegi akatoka kuelekea sebuleni...akawachukua watoto wake na kuondoka nao....magesa alibaki chumbani akiangua kilio..""uuuuuwii uesu na maria pesa zangu...hata kakuona mkewe alivyoondoka....mawazo yake yote yalikuwa juu ya pesa zake.... ******************* ule ulande mwingine baba sarai alionekana akiandaa mipango ya kufanya bihashara.....lakini ilipofika majira ya saamoja za usiku baba sarai alimuaga mkewe kisha akatoka...akaelekea baa akaanza kunywa pombe.....alianza kutoa maneno ya kejeri...akiwaambia wateja waliokuwa wakinywa pombe kwenye baa hiyo""nyinyi mbwa hamna pesa..mimi napesa.....aliyasema maneno hayo huku akiendelea kuagiza bia.... ilipofika mida ya saa tano za usiku..aliamua kurudi nyumbani...alipofika aligonga mlango kwa fujo..kitendo hicho kilimkera mke wake...lakini hakuwa na namna kwa sababu baba mwenyenyumba ndio karudi.......baba sarai alipoingia ndani alijitupa kwenye makochi akalala usingizi hapohapo.....""jamani mume wangu umepata pesa badala ufanyie mambo ya maana wewe umeenda kulewea pombe....mke wa baba sarai aliyasema maneno hayo huku akimsikitikia mumewe......akaamua kumuacha alale hapohapo sebuleni...... *************** asubuhi palipokucha baba sarai alidamka akajikuta kalala sebuleni....kutokana na kiburi cha zile pesa alizookota alinyanyuka na kwenda chumbani...alimkuta mke wake bado kalala..akaanza kimshushia kipigo""kwanink umenilaza sebuleni umeanza dharau ee???? alimpiga vibaya akampasua mdomo baada ya kumpiga ngumi za uso zisizokuwa naidadi..kisha akamfukuza mkewe.... ****BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA**** baba sarai alikuwa maarufu sana kuliko siku za nyuma...kila baa walimfahamu walimpa jina la mzee wa MUPE MURUKE jina hilo lilikuwa likajulikana kwa muda mfupi...baba sarai alikuwa akiingia baa aliwanunulia pombe watu waliomuita jina hilo...yani ukisema MUPE MURUKE basi unajipatia bia kumi....baba sarai alipita safa kila kona ya mitaa....hata ule mpango wake wa kuanzisha bihashara ukatoweka kwenye mawazo yake....saraalichukizwa sana kwa kitendo hicho... lakini akawa anasubiri aone mwisho wake utakuwa vipi..... baada ya miezi mitatu kupita pesa ilianza kupungua baba sarai akaanza kupagawa...alihisi kuchanganyikiwa alipokwenda kuangalia salio la pesa zilizobaki zilikuwa ni shilingi laki tatu pekee... akaanza kuwa anakunywa kwa bili...kwa sababu baa zote alizokuwa anakunywa zilimuamini...kila alipokuwa akifika anakunywa pombe anazotaka kisha anaondoka...alifanya hivyo baa nyingi...na baada ya mwezi mmoja kuisha alianza kudaiwa alipe madeni ya pombe alizokopa.... akaanza kujificha aliishi maisha ya kujifichaficha...hatimae hata zile laki tatu zilikwisha...alipokuja kutahamaki alikuwa hana hata mia.. *********** ule uoande mwinngine Magesa maisha yake yalikuwa magumu sana hata chakula kwake ikawa shida alimkumbuka mkewe...akaamua kumtafuta alifanikiwa kumpata lakini alikuta tayari kaolewa na mwanaume mwingine...magesa alichanganikiwa kutokana na msongo wa mawazo magesa alikuwa mwehu kabisa akaanza kuokota makopo barabarani... wale wawili walioshiriki na magesa kuichoma nyumba ya jeny...waliendelea kutaabika maisha yao yalikuwa magumu kila siku zilipozidi kusonga wake zao waliwakimbia kutokana na ugumu wa maisha kwa sababu walizoea kula vizuri na kulala pazuri...hivyo maisha yalipobadilika ghafla walishindwa kuvumilia....hatimae mmoja wao akaanza kupiga debe kwenye vituo vya daladala...kadri siku zilivyosonga akaanza kuwa mwizi...sikumoja alikwenda kuiba alivunja dirisha akaingia ndani lakini kabla hajaiba walimkamata...wananchi wenye hasira kali walimpiga na kumchoma moto..... Baba sarai aliamua kuhama mtaa akaikimbia nyumba yake alianza kazi ya kushona viatu.... sikumoja akiwa katika kazi hiyo ya kushona viatu alikuwa akitazama upande wa barabara kwa mbali aliona mtu....alipomtazama kwa umakini alimtambua mtu yule akanyanyuka ili asogee aone kwa ukaribu...wakati anazipiga hatua mara ghafla.. ITAENDELEA...... usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua. *Kesho nayo siku* ASANTENI.

at 7:07 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top