Home → simulizi
→ Riwaya: SARAI
SEHEMU YA SITA(06)
***Ilipoishia***
walimkamata...wananchi wenye hasira kali walimpiga na kumchoma moto.....
Baba sarai aliamua kuhama mtaa akaikimbia nyumba yake alianza kazi ya kushona viatu....
sikumoja akiwa katika kazi hiyo ya kushona viatu
alikuwa akitazama upande wa barabara kwa mbali aliona mtu....alipomtazama kwa umakini alimtambua mtu yule akanyanyuka ili asogee aone kwa ukaribu...wakati anazipiga hatua mara ghafla..
***Endelea***
Wakati anazipiga hatua mara ghafla alistahajabu kumuona Magesa amekuwa mwehu magesa alikuwa kabeba furushi lililojaa makolokolo ya kila aina yakiambatana na takataka.....baba sarai alistuka sana... kwani alikuwa akimfahamu magesa miaka mingi iliyopita...pia aliwahi kufanya nae kazi katika kampuni inayohusika na utengenezaji wa barabara hakujua kuwa nyumba aliyoijenga kisha aliyoijenga kisha akamtelekeza mkewe akiwa na mtoto mchanga.....magesa alikuwa ni mmona wapo kati ya watu waliohusika kuichoma nyumba hiyo....wakati anamtazama magesa mara ghafla magesa aliingia katikati ya barabara akagongwa na gari....magesa aliumia sana alivunjika miguu yote miwili ikang'oka palepale....wasamalia mwema walimuhurumia magesa wakamuwahisha hospital....hivyohivyo na kichaa chake(mwehu)
baba sarai macho yalimtoka huku akisikitika sana...wakati baba sarai akiendelea kustahajabu...wakati huohuo kunavibaka walipita na kuiba viatu alivyoachiwa kwa ajili ya kuvisafisha na kuvipaka rangi vilikuwa viatu pea tisa...baba sarai hakuweza kuwaona vibaka hao kwa sababu alikuwa amesimama mbali kidogo....
alipogeuka alihisi anaota ndoto za mchana kweupe huku akiwa macho wazi...alistuka sana baada ya kuona hakuna kiatu hata kimoja....
akaangaza angaza macho huku na kule.. hakuweza kumuona mtu yeyote aliyebeba viatu...
punde alikuja mtu moja kati ya wateja walioacha viatu vyao visafishwe na kupakwa rangi ya viatu...mtu yule alitoa noti ya shilingi elfu mbili ili amlipe baba sarai...lakini baba sarai aliipokea pesa ile kwa wasiwasi mkubwa akitazama huku na kule..kisha akasema ""ngoja nikatafute chenji...yule mteja aliamua kuketi ili amsubiri baba sarai....kumbe baba sarai hakwenda kutafuta chenji aliamua kuondoka kuelekea nyumbani kwake...
punde mteja wa pili alifika akaketi kumsubiri baba sarai kwa sababu aliambiwa fundi viatu katoka kidogo....punde mtu wa tatu na wa nne akaja...walikuja kila moja kwa nyakati tofauti....walikuja wote isipokuwa mtu mmoja...
****************
upande mwingine alionekana baba sarai akizipiga hatu za harakaharaka nusu akimbie....baba sarai alitembe huku akijikwaa hata kwenye mchanga..akiwa njiani mara ghafla alikutana na mmiliki wa baa ile aliyokopa pombe miezi miwili iliyopita....yule mtu alipomuona baba sarai alimkamata baba sarai ili amlipe pesa zake za vinywaji aina ya pombe...baba sarai alijaribu kujitetea.....lakini mtu huyo hakutaka kumsikiliza...akamkamata suruali..kamnyanyua juu juu(tanganyika jeki) mpaka kituo cha polisi...
baba sarai aliwekwa sero...kisha mtu yule akamuacha hapo kituo cha polisi na kuondoka zake...
******************
ule upande mwingine alionekana magesa katika chumba cha upasuaji madaktari walikata nyamanyama zilizokuwa zikining'inia miguuni..baada ya kuvinjika na kung'oka kabisa...
wakati huo magesa alikuwa kapoteza fahamu..alikuwa kafungwa bandeji mwili mzima kutokana na majeraha ya kuchubuka ngozi sehemu kubwa za mwili wake.....madakari walipomaliza kumfanyia upasuji...walimrudisha wodini.....wakati huohuo alionekana mke wa magesa akizipiga hatua kuelekea kwenye wodi ya wagonjwa waliopata ajali..mke wa magesa alikwenda kumuona mjomba wake aliye pata ajali kipindi anaendesha bodaboda....akiwa ndani ya wodi...ghafla magesa alizinduka akapata fahamu..alipofumbua macho kwa mbali alimuona mkewe aliyemuacha kisha akaolewa na mwanaume wingine..kutokana magesa alifirisika na kuwa na maisha magumu mpaka chakula ndani ya nyumba ilikuwa ni shida....kitendo cha kumuona mtalaka wake akili za magesa zikarudi kwenye uwezo wake wa kufikiri na kutambua jambo.... magesa akatoka katika hali ya ukichaa(mwehu) akawa na akili timamu kabisa...magesa alipojaribu kunyanyuka alihisi maumivu makali mwili mzima alipojaribu kunyanyumiguu hakuweza kuona miguu yake aligindia miguu yake yote miwili ilikuwa imekatwa...hakuweza kutambua chanzo ni nini..kwa sababu kipindi anagongwa na gari mpaka miguu yote miwili kivunjika na kung'oka alikuwa katika hali ya ukichaa(mwehu)
wakati huohuo alionekana sarai akiwa katika mlima mmoja.. ameketi juu ya jiwe huku akipuliza filimbi yake iliyokuwa imetengenezwa kwa mfupa wa binadamu....kisha akasimama... mara ghafla akatoweka kimiujiza...
ITAENDELEA......
usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua.
ASANTENI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: