Bikra yangu: 05 "Nimeshamuaga mama nimemwambia mida ya saa nane ntaenda kwa rafiki yangu". Nilimjibu vuai "Ok poa" alijibu na kukata simu. Nilifanya kazi zangu haraka ili utakapofika muda wa kuondoka muda tuliopanga na vuai niwe nimeshamaliza kazi zangu. Kama ilivyo ada nilimaliza kupika na tukala chakula cha mchana mimi, mama pamoja na mdogo wangu wakati huo baba akiwa ktk shughuli zake za kibihasha. Nilipo maliza kula sikutaka kupoteza muda moja kwa moja nilielekea chumbani kwetu kujiandaa kwenda kuoga. Nilienda kuoga huku nikikimbizana na muda kuwahi mihadi yetu na mtoto wa kishua. Kutokana na muda mrefu kuwa busy sikupata muda wa kushika simu hata kidogo. Nilipotafuta simu kuangalia saa tayari ilikuwa imeshafika saa nane na nusu. Wakati huo simu ilikuwa na sms sita na missed calls za kutosha zote zilitoka kwa vuai, sikuweza kusikia kwasababu nikiwa nyumbani huwa napenda kuondoa sauti kwenye simu yangu. Nilianza kusoma massage moja baada ya nyengine lakini zote zilionekana kuniuliza niko wapi na nyengine zikinielekeza ni wapi tutakutana. Wakati naendelea kusoma zile massage simu ilianza kuita, alikuwa ni vuai niliikata na kumtumia msg iliyosema "Njoo unichukue kwa bakadhir mi ndio namalizia kuvaa" kisha nikaituma. Baada ya dakika kadhaa alituma msg iliyosema "Tayari nimefika". Wakati huo mimi nikielekea alipokuwa amekaa mama na kumuaga. "Mi natoka mama" nilisema huku nikielekea kufungua mlango wa sebuleni. "Sawa usichelewe mwanangu si unamjua baba ako alivyo!!!!?" alisema mama na kuishia hapo. "Nitawahi mama" nilimjibu Haraka haraka niliwahi pale kwa bakadhir na kumkuta vuai akiwa maenuna . "vp nimechelewa eeeeh" nilijisemelesha. "Yes umechelewa sana na nilibakiza dakika chahe mi niondoke zangu" alisema vuai huku akiendelea kulalamika "tatizo letu sisi wa Afrika hatuwezi kwenda na muda" "Basi baba nitajitahidi kutumia muda vizuri" niliongea kwa utani. vuai aliwasha gari na tukaanza safari ila nilimsisitiza kwamba tuwahi kurudi kabla ya saa kumi na mbili jioni. "Ondoa shaka kuhusu hilo" sema vuai huku akiendesha gari kwa speed. Japo sikujua ni wapi napelekwa lakini tayari nilikuwa nimeshagundua gari inaelekea wapi. Haikuwa tofauti sana na mawazo yangu coz kile nilichokiwaza ndivyo kilivyokuwa, tulikuwa tukielekea stone town. Punde tulifika kwenye restaurant moja iliyojulikana kwa jina la Six degree iliyopo karibu na fukwe ya bahari. Sikuwa mgeni sana na maeneo yale kutokana na maswala ya utalii ninayosomea mara pengine huwa tunakuja practical kwenye jengo la African House liilopo karibu na hiyo restaurant. Aliitwa waitress na kuja kutusikiliza huduma tunayohitaji. Vuai aliniambia niagize chocho ninachojisikia kula lakini kutokana na kushiba ugali nyumbani ilinibidi nikatae chakula na kuagiza soda. "Aaaaaaaah!!!!!! Mambo gani hayo zuleiha utaagizaje soda bana wakati kuna vinywaji vingi tu" alisema vuai. "Mi nitakunywa soda tu inatosha" nilimwambia. "Basi agiza Red blue" alisema vuai "Haina kilevi?" nilimuulza "Haina" alijibu huku yeye akiagiza chakula na red wine aliyojulikana kwa jina la Rosee. Tulianza mazungumzo ya hapa na pale hasa hasa kujuana vizuri na kupiga baadhi ya stori za kimaisha, lakini katika mazungumzo ya vuai yalionekana kuelekea kwenye mahusiano kutokana na kuniuliza kwa umakini maish yangu ya kimahusiano yapoje. Kwakweli sikutaka kumficha kitu hata kimoja kuhusu maisha yangu nilimweleza ukweli kuhusu mfumo mzma wa maisha yangu na alionekana kunisifia sana hasa pale nilipo mwmbia sijawahi kukutana na mvulana yoyote kimwili japo haikuwa rahisi kwake kuamini hilo. Alinishauri sana kuhusu kuendelea kujitunza na kunisihi sana kuwa makini na vijana wa mjini. Wakati tukiendelea kuzungumza nilimuona vuai akiwa ameanza kulegeza jicho kidogo kidogo ila alionekana kuwa mchangamfu sana. Niligndua hiyo itakuwa wine imeanza kufanya kazi kidogo kidogo. Muda ulikuwa umeshakwenda sana ilikuwa imeshatimu saa kumi na mbili kasoro baada ya kuangalia saa yangu ktk simu, nianza kumsumbua vuai afanye haraka ili tuondoke na hata ikiwezekana aache hiyo wine yake ilikusudi niwahi nyumbani. Bahati nzuri hakuwa mbishi ktk hilo tulianza kuondoka ktk eneo hilo. Tuliingua ndani ya gari na kuanza safari ya kunirudisha nyumba , kipindi tupo kwenye gari ukimya ulitawala kwa takribani dakika tatu hivi ikanibidi nianzishe mazungumzo. "vuai mbona uongei? au nimekukera?" nilimuuliza "hapana , lakini nawaza mbali na kufahamiana baina ya mimi na wewe nahisi kuna kitu bado hujakifahamu kutoka kwangu" alisema vuai "kitu gani hicho?" nilimuuliza huku nikimtazama kuashiria umakini wa hali ya juu. Alikaa kimya kwa muda kisha akaniita jina langu. "zuleiha"..... "beeeeeee" niitika "Naomba nitoke nje ya mawazo yako kidogo kwa sasa coz najua hicho unachokiwaza hivi sasa si hiki ninachotaka kukwambia" alisema vuai. "we niambie tu usijali" nilimwambia "kwanza nashukuru kwa kunipa hii nafasi ya kutoka na wewe siku ya leo nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sijataamka neno AHSANTE huku nikimaanisha, kwasababu imekuwa ni fursa adhimu kwangu leo kutoka na binti mzuri kama wewe. Nimefurahishwa na kampani yako siku ya leo japo tumefahamiana kwa muda mfupi ila hukujali kutenga muda wako kwa ajili yangu siku ya leo. Ahsante sana Zuleiha. Lakini pia huu muda utakuwa ulipangwa nikwambie hiki ninachotaka kukwambia , zuleiha kama hutojali naomba uwe wangu yani namaanishe uwe mpenzi wangu, nina nia njema sana na wewe sihitaji kukuchezea hata kidogo, kama uliweza kujitunza kwa kipindi chote hicho basi na mimi nipo tayari kukutunza na kuulinda utu wako, nakuahidi.................. ........................................ nilipewa maneno ya kutosha na yenye kila ladha, kutokana na kuhaidiwa kuolewa taratibu nikajikuta nukimwambia.... "sawa ntakupa jibu" nilimwambia lakini nilikuwa tayari nimeshaanza kumelewa ila nilitaka tu nicheleweshe muda wa kusema NDIO NIMEKUBALI. Hazikupita siku mbili nilikuwa tayari nimeshamkubalia ombi lake, maisha ya mahusiano yakaanza japo sikuwa muenyeji sana kwenye mambo ya mapenzi ili kadri siku zinavyozidikwenda nikajifunza kuita hata baby coz kuna vitu nilikuwa naona aibu kabisa kuvifanya. Hadi ilifikia hatua vuai alikuwa ananilaumu niache mambo ya kitoto pindi akinibusu mi natema mate. Kiukweli vitu hivyo vilikuwa ni mateso makubwa kwangu, kuna kipindi sikutaka kabisa anishike hata mwili wangu. Lakini vuai alijitahidi kunifundisha hadi kuanza kuzoea maadhi ya vitu kidogo kidogo Nilikuwa ni mtu wa kutolewa kila weekend lakini vuai hakupata bahati ya kuona ha nguo ya ndani ninayovaa zaidi ya kuni_hug na kuni_kiss. Japo kuna kipimdi alikuwa ameanza kunichomekea habari zakufanya mapenzi, nilimpinga vikali huku nikimsisitizia swala hilo tutafanya hadi tukioana. Siku zilisonga mbele....... ilikuwa ni siku ya ijumaa saa 10 jioni kama kawaida nikisubiri my love vuai anifate na gari tuondoke siku hiyo nilichelewa kidogo kutoka chuo kutoka na mitiahani. Alipofika maeneo yale ya chuo alinipigia simu na kunielekeza mahali alipo nimfate ili anipeleke.......................... ITAENDELEA

at 4:40 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top