Bikra yangu 04. "Mambo zenu wakina dada, zuleiha ndio yupi hapa" aliuliza yule kaka "Ndio mimi hapa" alijibu rafiki yangu aliyejulikana kwa jina la salma "Ahaaa ninaujumbe wako kutoka kwa vuai" alisema yule kaka huku akionesha ishara ya kumuita salma pembeni kidogo ya maeneo tuliyokuwa tumekaa. Kutoka na yule kaka kutomfahamu zuleiha alijipa asilimia mia kuwa salma ndiye mtu aliyekusudiwa. "Mambo vp sista, jamaa kaniagiza nikwambie kwamba wakati wa lunch anaomba mue pamoja kama hutojali" alisema yule kaka. "Jamaaa!!!!!!!! Jamaa gani huyo"? Aliuliza salma kutoka na kutofahamu lolote lililokuwa likiendelea baina ya vuai na zuleiha "vuai" alijibu yule kaka huku akiendelea kusema "inamaana umfahamu mbona kaniambia jana ulimpigia simu!!!!!!? "Aaaaah okk mambo mengi kaka angu, basi sawa mwambie ntamcheki hiyo mida" salma aliuwa soo kiivyo ili asijulikane kuwa yeye sio zuleiha. "Basi poa jitahidi umcheki jamaa hiyo mida kama vp baadae" alisema yule kaka na kuondoka ktk eneo lile huku akiamini kuwa yule aliyekuwa akizungumza nae ndiye zuleiha. Salma alirudi pale tulipokuwa tumekaa na kuuchuna bila kusema kile alichoambiwa na yule kaka zaidi ya kujifanya anampondea yule kaka kwa kusema.......... "wakaka wengine bwana wanapenda kweli kusafiria nyota za wenzao.... Eti yule kaka anataka namba zangu huku akiamini mimi ndio zuleiha. "kwahiyo umempa"? Aliuliza mmoja kati ya wasichana waliyokuwepo pale. "weeee nimpe namba zangu za nini wakati alikuwa anahitaji za zuleiha". Alijibu salma wakati huo mimi nikiwa nimekaa kimya. .......................................................... Muda wa lunch ulipowadia sikuwa najisikia kabisa kula ikanilazimu nielekee kwenye bustani kwaajili ya kujisomea.Wakati huo rafiki zangu wakielekea canteen kupata msosi. Wakati nikiendelea kujisomea ghafra alikuja mmoja kati ya marafiki zangu aliyekuwa pamoja na wakina salma na kunambia "tumenunuliwa chakula na yule kaka aliyekupa lift jana ila amesikitika sana kwanini umekataa kwenda wakati alimtuma mtu akuletee ujumbe kwamba anahitaji muonane wakati wa lunch!!!!!!!!!? "Akaa!!! Mi sijapewa huo ujumbe na hata hivyo leo sijikii poa kabisa hata kama ningeenda sidhani kama ninge_enjoy hiyo lunch" nilimjibu yule rafiki yangu kisha nikamuuliza tena kwani wakina salma umewaacha wapi? Salma yupo na yule kaka canteen bado wanaendelea kula....................... Ilipofika muda wakutoka chuoni vuai akanipogia simu na kuniambia nimsubiri pale aliponikuta jana. Bila kusita nikamkubalia na kufanya hivyo alivyoniambia. Kama kawaida nikajisogeza pale nilipoambiwa nimsubiri. Punde ilikuja ile Nadia nyeusi iliyonibeba jana ila cha ajabu siku hiyo alikuwa aki_drive vuai mwenyewe. "zuleiha panda twendwe" alisema vuai Bila kupoteza muda nikafungua mlango wa nyuma nakutaka kuingia. "No no no no njoo ukae mbele bana leo tupo wenyewe usikae nyuma peke yako" alisema vuai huki akinisisitiza nikakae nae mbele. Nilitii wito na gari ikaanza mwendo taratiiiiibu tukiwa tunapiga stori mbili tatu moja kati ya mambo tuliyokuwa tukizungumza ni pamoja na kupewa lawama kwanini nilikataa kwenda kuonana nae. "Mbona mi sijapewa ujumbe wa kuonana na wewe!!!! Kwani ulimwagiza nani? Nilimuuliza vuai Kuna rafiki yangu nilimwagiza kwako aje kukwambia kwamba nahitaji kuonana na wewe wakati wa lunch" alisema vuai. "Nikakumbuka kwamba nikweli asubuhi kuna mtu alikuja pale bustanini tulipokuwa tumekaa na rafiki zangu lakini sikuongea nae mimi coz salma alimuwahi na kujfanya yeye ndio zuleiha". Ili kuonyesha kwamba sikupata ujumbe ilinibidi niendelee kukataa kwamba sijapewa ujumbe wowote. "Basi huyo jamaa itakuwa hakukufahamu vizuri, lakini poa hakuna kilichoharibika. Alisema vuai. Ukimya ukatawala kwa sekunde kadhaa huku nikiwa najiuliza kwanini vuai anaendesha gari taratibu kiasi hiki au ndio anajifunza nini!!!? Nilijiuliza kimoyo moyo bila kupata majibu. "zuleiha weekend hii unaweza ukapata muda twende somewhere hivi kuna kitu nataka kuzungumza na wewe kama hutojali". Alizungumza vuai. "Mmmh" hapana sidhani kama nitapata huo muda..... Kwani unataka kuzungumza nini? Si uzungumze hapa hapa, kunaulazima kwende huko unapotaka twende"? Nilimuuliza "Aaaaah no si lazima sana lakini ni muhimu kwenda na uwepo wako unahitajika" aliongea vuai akionekana kunisisitiza sana kwenda huko anapotaka. "Nitaangalia kama nitapata muda ila usinitegemee sana coz sidhani kama wazee wataniruhusu ila nitafanya kitu". Kutokana na vuai kunikazani juu ya swala lakwenda nae huko nisipo pajua ili bidi nimpe moyo kwa kusema hivyo. "Utafanya kitu gani zuleiha"? Aliuza vuai. "Nitaaga naenda kwa rafiki yangu lakini huyo rafii yangu wazazi wanamfahamu so itabidi nimpange kabisa. Kwani unataka twende huko siku gani "? Nilimuuliza "Nadhani itakuwa jumamosi" alijibu vuai "Basi sawa tutawasiliana basi lakini usinitegemee sana coz lolote laweza tokea". Nilimwambia "Nitaomba sana iwe kama tulivyopanga" alisema vuai. Nilifika maeneo ya nyumbani tukaagana na kila mtu akashika upande wake...................... Ilikuwa ni jumamosi asubuhi mida ya saa nne nilipokea simu kutoka kwa vuai akiniuliza kuhusu ile mipango tuliyopanga. "Nimeshamuaga mama nimemwambia mida ya saa nane ntaenda kwa rafiki yangu". Yalikuwa ni majibu ya zuleiha akimjibu vuai ktk simu................... ITAENDELEA

at 4:40 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top