Home → simulizi
→ Bikra yangu 03
Alikuwa ni Vuai akiniita akiwa ndani ya gari nyeusi aina ya nadia iliyosimama mbele yangu.
"Beeeeee" niliitika.
Unaelekea wapi? Aliuliza vuai
"Now naenda home kiembe samaki" nilimjibu
"Njoo twende kama hutojali coz sisi tunaelekea mbweni tutakupitisha kiembe samaki" alisema vuai.
Fasta sikupoteza muda nikaingia ndani ya gari , nikakaa siti ya nyuma, kiukweli gari ilikuwa ni nzuri sana kimuonekano nilikuwa nikitembeza macho huku na kule kulichunguza zaidi kwa muonekano haikuwa gari ya muda mrefu sana tangu imenunuliwa.
Taratibu safari ilianza kuelekea home huku nikiwa katika tafakuri kadha wa kadha juu ya maisha ya vuai. Hatukuweza kupiga stori nyingi sana kwa wakati ule zaidi ya kunitambulisha kwa dreva wao aliyejulikana kwa jina la Amour na mimi akanitambulisha kama rafiki yake.
Kipindi nikiendelea kujiwazia mambo yangu nilishtushwa na sauti ya dreva akiniuliza....
Unashuka wapi sista?
"Niache hapo kwenye hiyo shule ya kiembe samaki" nilimjibu
Baada ya sekunde kadhaa gari ilisima , nikaanza kushuka huku nikimuaga vuai na dreva wake.
Kwaherini jamani, vuai tutaonana kesho.
"poa" alijibu vuai na kuuliza kwani unakaa maeneo gani mtaa huu?
"Nakaa hapo kwa Bakadhir" nilimjibu
Basi sawa kama vipi tutaonana kesho. Aliongea vuai huku akijisachi ktk mfuko wa shati alilokuwa amevaa, alitoa noti mbili za shilingi elfu kumi zilizo ambatanishwa business card akanipatia na kumuamuru dreva waondoke.
"Ahsante vuai" nilisema huku gari ikianza mwendo kidogo kidogo.
Kabla sijafika nyumbani nilipitia dukani kununua vocha ya buku kwaajili ya kuanza mazungumzo na mtoto wakishua.
Nilifika nyumbani na kuanza shughuri zangu za kawaida kama ilivyo ada. Kama kawaida lilikuwa ni jukumu langu kuingia jikoni kila nitokapo chuo, nilifanya majukum yangu na kula chakula cha usiku huku nikivuta muda wa kuzungumza na vuai. Kipindi nikiendelea kuvuta muda wa kuzungumza nae kuna maswali niliyokuwa nikijiuliza "kwanini huyu mvulana kanikaa akilini kiasi hiki kuliko hata wavulana wote ambao walishawahi kunitamkia kwamba wananipenda?
Swali hilo halikuwa na majibu kabisa zaidi kujiandaa kuongea nae.
Ilikuwa ni saa nne za usiku baba na mama kuingia ktk chumba chao kulala, Mimi na mdogo wangu tukiwa bado tunaangalia tamthilia, lengo langu lilikuwa ni kumsubiri mdogo wangu aende kulala ili nitakapoanza kuzungumza nizungumze kwa amani.
Ilipofika saa nne na nusu tamthilia ilikuwa imeshaisha huku mdogo wangu akiwa ameshasinzia tayari. Nilizima tv na kumuamsha akalale chumbani, muda kidogo na mimi nikaelekea chumbani kwetu nikiwa na shauku ya kuongea na vuai.
"Hafadhali" nilijisemea baada ya kuingia chumbani na kumkuta mdogo wangu akiwa amelala fofofo.
Fasta nilifunga mlango na kukaa kitandani, nikatoa ile bussiness card niliyoiweka kwenye mkoba wangu. Nilianza kupiga moja ya namba kati ya zilizokuwa ktk kadi ile. Kwa bahati mbaya simu iliita bila mafanikio sikuishia hapo nikapiga tena lakini haikupokelewa pia, sikukata tamaa nikapiga tena hukunikijiwazia labda atakuwa amelala.
Wakati simu imeita sana kwa muda mrefu ghafra ikapokelewa.
"halloo" alisema vuai
"halloo mamboo"
"safi nani?" aliuliza
"mi zuleiha"
Okkkkk uko poa zuleiha? Mbona umepiga simu muda umekwenda sana? Aliendelea kuuliza tena vuai
"Sikuweza kukupia mapema coz nilikuwa karibu na wazazi lakini hata hivyo nilijua nikikupigia sahizi itakuwa muda mzuri wa kuongea na wewe " nilimjibu na kumuuliza "kwani ulikuwa umeshalala?
Yeah, leo nimelala mapema coz sipo sawa kama vipi tutaonana kesho au unasemaje mamie? Alisea vuai
"Sawa lakini nilikupigia tu ili uijue namba yangu, tutaongea kesho vizuri". Alisema zuleiha
"Ok poa mi nikutakie usiku mwema"
"nawe pia" nilimjibu na kukata simu.
Siku ya jumanne asubuhi na mapema nilifika chuo kama ilivyo kawaida. Wakati nikiwa katika bustani ya chuo pamoja na rafiki zangu tukibadilishana mawazo, alikuja kaka mmoja ktk eneo tulilouwa tumekaa japo sura yake haikuwa ngeni kwangu lakini hatukufahamina majina.
"Mambo zenu wakina dada, zuleiha ndio yupi hapa" aliuliza yule kaka
"Ndio mimi hapa" alijibu rafiki yangu aliyejulikana kwa jina la salma
"Ahaaa ninaujumbe wako kutoka kwa vuai" alisema yule kaka huku akionesha ishara ya...............
Itaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: