Home → simulizi
→ Bikra yangu 02
Kipindi nainama chini kumuokotea yule kaka simu yake, yule kaka aliniwahi na kunishika mkono huku akiniambia "usijali dada najua umenipamia kwa bahati mbaya ondoa hofu kuhusu hilo".
Nilipigwa na butwaa kwa Sekunde kadhaa huku nikitafakari tukio zima liliotokea pale, ilikuwa ningumu sana kuamini kama nimesamehewa kwa kile kilichotokea pale.
Alichofanya yule kaka ni kuokota simu yake na kuendelea na safari yake ya kuelekea canteen kupata lunch. Kipindi naendelea kupigwa na butwaa huku nikiwa na hali ya hofu juu ya kumsababishia hasara kaka wa watu likanijia wazo la kumfata na kumuomba radhi kwasababu sikufanya hivyo wakati wa tukio lile limetokea.
Sikutaka kupingana na mawazo yangu nilirudi canteen moja kwa moja hadi kwenye meza aliyokaa yule kaka, nilimkuta kaka wa watu yupo bize akibugia matonge ya wali na samaki aina ya changu.
Karibu tule dada" alisema yule kaka
"Ahsante nimetoka kula muda si mrefu" nilijibu huku nikivuta kiti nikae.
"Samahani kaka najua unakula lakini kwasababu ya muda naomba unipe fursa ya kunisikiliza kidogo" nilimwambia yule kaka huku nikiwa na hali ya wasi wasi.
"Usijali dada nakusikiliza vyema" alisema yule kaka huku akiendelea kutupia matonge mdomoni.
"Najua nimekupa hasara ya bila kutegemea muda huu, japo unafahamu nimekupush kwa bahati mbaya ila nahisi roho yangu imepoteza kabisa amani kuondoka eneo hili bila kukutaka radhi, nisamehe sana kaka angu kwa kukuharibia simu yako". Niliongea huku nikimtazama yule kaka aliyeonekana kuwa bize na msosi.
"Ondoa shaka sista wala usijali kuhusu hilo" alijibu yule kaka.
Kutokana na majibu ya yule kaka kuwa ya mkato sana japo hakunionyesha hali yoyote ya kukwazika na tukio lile nilihisi labda namsumbua wakati wa kula. Nilikaa kimya kidogo huku nikiendelea kujibaraguza pale huku nikitafuta njia za kuaga niondoke zangu pale wakati huo akimalizia kula.
Nilijikuta neno likinidondoka kinywani na kumuuliza "samahani kaka na wewe ni mwanafunzi wa chuo hiki?
"Yeah, nami pia nasoma hapa lakini sina muda sana hapa chuoni nimeanza masomo hivi karibuni, nachukua certificate of tour operator
ya miezi sita". Alijibu yule kaka.
Kwanini usichukue full corse? Niliuliza
Hapana, mi ni muajiriwa ktk kampuni kubwa ya utalii hapa unguja inayojulikana kwa jina la MPUTI ISLAND TOUR nilipata bahati ya kuajiriwa pale kwa kufanyiwa mipango na mzee wangu, sasa director wa kampuni alizungumza na father siku chache zilizopita na kumwambia inabidi nitafute cheti hata cha short corse kwasababu siku si nyingi utafanyika mchujo wa kupunguza wafanyakazi wasiokuwa na vyeti. Alieleza yule kaka.
Alaaa basi sawa mi nashukuru sana kwa kunisamehe na nimependa sana jinsi ulivyo mkarimu, ingekuwa ni wakaka wengine hapa leo sijui ingekuwaje, Nilijisemelesha
"Ah! usijali dada kawaida", alijibu
"Basi sawa mi naenda class now tutaonana baadae" nilisema huku nikiinuka kwenye kiti na kujiandaa kuondoka.
Kipindi naanza kuondaka ilisikika sauti ikiita "sista" niligeuka alikuwa ni yule kaka, alisogea na kuniambia tumeongea mengi lakini hatujafahamiana majina bado. Alisema yule kaka.
"Aaha mi naitwa zuleiha nipo mwaka wa pili ngazi ya diploma, nasoma mambo hayo hayo ya utalii, na wewe unaitwa nani"? Nilimuuliza
Akajibu mi naitwa Vuai.
Sawa ahsante vuai mi nawahi class tutaonana muda mwengine" nilimjibu na kuondoka kuelekea darasani.
Ilikuwa ni mida ya saa 10 alasiri natoka chuo pamoja na rafiki zangu, kwa mbali nilimuona vuai akiwa na rafiki zake nilitamani kumuita lakini kutokana na mazingira niliyolelewa ya kutozoeana na wavulana nikajikuta nikimpotezea.
Kipindi tukiendelea kusubiri daladala ktk eneo lile ilikuja gari aina ya nadia kumchukua vuai , "kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe ni mtoto wakishua ndio maana ilikuwa rahisi kunipotezea wakati nimempush na kudondosha simu yake!!!"
Wakati nikiendelea kutafari juu ya tukio lile lililotokea canteen na kujisemea mwenyewe kimoyo moyo nilishtushwa na sauti iliyosikika ikiniita "Zuleiha"
Alikuwa ni Vuai akiniita akiwa ndani ya gari nyeusi aina ya nadia iliyosimama mbele yangu.
"Beeeeee" niliitika............
ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: