Bikra yangu 01 Naitwa zuleiha ni mtoto wa kizanzibar mwenye umri wa miaka 19. Natoka ktk familia ya kawaida si yakitajiri wala si yakimasikini. Baba yangu ni mfanya bihashara ktk soko kubwa la hapa mjini unguja maarufu kama darajani, mama yangu ni mama wa nyumbani. Mimi ni mtoto wa kwanza ktk familia yenye watoto wawili. , Wazazi watu walibahatika kupata wototo wawili tu na wote wakike ambao ni mimi na mdogo wangu mwenye umri wa miaka 13. Nilifanikiwa kupata elimu ya chuo ngazi ya diploma ktk chuo cha maruhubi kilichopo hapa mjini unguja, nilikuwa nikichukuwa taaluma ya utalii. Ktk maisha yangu ya shule toka elimu ya msingi hadi sekondari nilifanikiwa kutunza bikra yangu hadi nilipo ingia chuo. Kutokana na uzuri wangu nilijitahidi sana kupambana na vishawishi vya wanaume wa kila rika wengine wenye umri zaidi ya baba yangu, wote walikuwa wakinihitaji kimapenzi na wengine walithubutu kwenda hadi kwa wazazi wangu kwa lengo la kunichumbia. Mbali na uzuri wangu wazazi wangu walikuwa wakorofi sana na wenye itikadi kali kupita kiasi. Walitulea ktk mazingira hayo lengo lao hawakutaka watuone tukiharibikiwa kimaisha au kimasomo. Mbali na wazee wetu kuwa watata juu ya mambo hayo, lakini pia tamaduni zetu za kizanzibar ni lazima uolewe ukiwa na bikra yako. Msichana akiolewa akiwa na bikra yake hiyo ni heshima kubwa kwa wazazi na familia nzima kwa ujumla. Kwa upande mwegine kwa waowaji tamaduni hizo zimejengeka vibaya huku wakiamini kuoa mwanamke asiye na bikra ni sawa na kuingiza mkosi ndani ya familia au kama msichana atapata bahati yakuolewa bila brika ajue ataenda kuwa mke wapili. Wazazi wangu walipinga vikali fedheha ya kuzarauliwa kwa kushindwa kutulea vyema, ndio maana walizisha ukali maradufu pindi walipogundua nipevuka (kuvunja ungo). Hawakutaka hata siku moja niongozane na kijana yoyote yule awe wa mtaani kwetu au hata chuoni waliamini hakuna urafiki baina ya msichana na mvulana. Maisha yangu ya chuo yalikuwa mazuri na yenye amani huku nikiendelea kupambana na changamoto za kimapenzi , ilikuwa ni nadra sana siku kupita bila kutongozwa na zaidi ya wavulana wawili. Nilikuwa ni mwenye msimamo mkali sana juu ya maswala ya kimapenzi sikutaka hata kusikia mvulana akinitamkia kuwa ananipenda, hiyo ilinifanya nianze kuitwa majina ya ajabu ajabu pale chuoni. Baadhi ya majina niliyokuwa nikiitwa ni BINTI MARINGO, MTOTO WA OSAMA NA mengine mengi kama hayo. hali hiyo ilwafanya hata marafiki zangu waanze kunitenga kwasababu wao wote walikuwa na wapenzi wao. Ilikuwa ni jumatatu tulivu iliyokuwa na furaha kwa upande wangu, nikiwa ktk maeneo ya chuo mnamo mida ya saa saba nilielekea kupata chakula ktk canteen ya chuo, nilipata chakula na kuanza kuondoka ktk maeneo hayo ya canteen kipindi nimefika mlangoni nikielekea nje huku nikichezea simu yangu nilimpamia kaka mmoja alikuwa akiingia canteen kupata chakula na yeye akiwa anachezea simu. Kwa bahati mbaya simu ya yule kaka ilidondoka na kupsuka kioo, binafsi niliwaza kumlipa lakini nilishtuka sana nilipoambia jina la ile simu na thamani yake , ilikuwa samsung galaxy note 6, kutokana simu ile kuvishwa kava nilijua uwenda itakuwa tecno L8 plus yenye garama ya laki mbili, kumbe ilikuwa ni simu yenye thamani zaidi ya laki saba. Kipindi nainama chini kumuokotea yule kaka simu yake, yule kaka aliniwahi na kunishika mkono huku akiniambia............... ITAENDELEA

at 4:39 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top