Bikira yangu:13 "Zuleiha habatri yako"? Ile nageuka kumtambua aliyenisalimia ni nani, kumbe alikuwa ni vuai ktk viunga vile vya kupandia boti za kuelekea kisiwani. Sikutaka kabisa kuongea nae kitu chochote na wala sikutaka asogee karibu yangu. Nilivyoshuka tu nilimwambia mahmoud tuondoke ktk eneo lile, lakini vuai alionekana kunifata kwa kasi huku akiniita kwa sauti. "Kwani huyo ni nani"? Aliuliza mahmoud baada ya kuona kero za vuai zinazidi. "We tuondoke tu nitakwambia ila kwasasa sihitaji kabisa kuonana na huyo kaka" nilimwambia mahmoud. Ilimlazimu mahmoud na yeye aongeze mwendo baada ya kuona ninatembea kwa kasi. Kutokana na kero za vuai kukithiri ilinilazimu nisimame kumsikiliza alichokuwa akikihitaji kwangu. "Haya sema shida yako" nilimwambia kwa hasira huku mahmoud akiwa anashangaa bila kutambua kinachoendelea. "Tafadhali naomba unisiskilize zuleiha" alisema vuai. "Ni kitu gani kinachokufanya unifate mbio mbio tena mbele za watu kama unanidai? Nilimuuliza kwa hasira. Mahmoud alikuwa kimya akinishangaa kinachoendelea baina ya mimi na vuai huku akitutaka tuongee taratibu ilikusudi watu wasikusanyike kwaajili yetu. "Kwanini umekuwa mtu wa aina hiyo? Kwanini umekuwa mtu mwenye roho ngumu kiasi hicho? Ni kosa gani kubwa ambalo nililotenda kwako ambalo halina msamaha? Hebu usiwe mtu wa aina hiyo, rudisha moyo wako nyuma na ukumbuke hata kidogo umuhimu wangu kwako. Sipendi niwe adui kwako, ni makosa mangapi umetenda na mungu amekusamehe? Lakini kwanini hutaki kutoa msamaha wako kwangu. Najua kuwa unanichukia tena sana tu, ila kama Mungu alimuumba mwanaadamu si mkamilifu basi kuna kila sababu za kuepo neno msamaha.......... Aliongea maneno hayo vuai huku akionekana kuhitaji msamaha wangu. "Zuleiha hakuna kosa kubwa lisilosameheka kama Mungu anasamehe kwanini wewe usisamehe, hebu jaribu kurudisha moyo wako nyuma". Alisema mahmoud bila kujua chanzo cha tatizo ni nini. "Mi nilishamsamehe ila kwa sasa sihitaji usumbufu kutoka kwake, sitaki kabisa anizoee. Niliongea kwa hasira kisha nikaanza kuondoka, mahmoud ikabidi anifate. "Zuleiha, zuleiha, zuleiha" vuai aliita bila mafanikio........................... Mawasiliano na mahmoud yakawa makubwa kwa kiasi chake huku mahmoud akiamini kwamba mimi ndio mke wake mtarajiwa. Binafsi sikutaka kuliweka hilo akilini mwangu kutokana na kutokidhi vigezo vya mke aliyekuwa akimuhitajiwa mahmoud. Mbali na hilo pia sikutaka kumtia mahmoud akili mwangu kutokana na kuhisi atakuwa na tabia kama za vuai yani kwa kifupi nilianza kupoteza uwaminifu kwa wanaume wote ila sikudhihirisha hilo kwa mahmoud. Siku zilizidi kwenda huku mahmoid akinipa faraja ya kuandaa mipango ya harusi yetu ila bado nilikuwa siamini kabisa, nilichokuwa nikikifanya ni kumpa moyo kwamba na mimi nasubiri kwa hamu kuingia mdani ya ndoa. Siku moja mahmoud alinipigia simu na kunieleza anataka tuzungumze mipango ya kuleta wazee wake nyumbani kwetu, nilimuitikia lakini nikamwambia sidhani kama nitakuwa na muda wa kuonana naye labda tuongee kwenye simu, hii ilitokana na hofu niliyokuwa nayo juu ya wanaume wa aina kama ya vuai. Aliniomba sana nakunisisitiza tuonane hata kama itakuwa barabarani tu itatosha, sikuwa na budi kumkatalia ikanilazimu nipange ratiba zangu kisha nikaonane nae. Tuliongea mengi sana huku akinihakikishia kwamba anamalengo na mimi na nikaanza kuamini hilo baada ya kuniambia kesho atawaambia wazazi wake waje nyumbani kwetu. Nilianza kuamini ila bado nilikuwa na hofu juu ya kigezo kimoja tu alichokuwa akikihitaji na ndicho kilikuwa kipaumbele chake. Japo kuna wakati nilijipa moyo kwakuwa nimeingiliwa mara moja tu kimwili huwenda bikira yangu haikutolewa kisawa sawa. Nilimkubalia ombi lake la kuja nyumbani kwetu ila sikutaka waje kesho kwasababu sikuwa nimewaambia wazazi wangu. "Mahmoud wacha nikazungumze na wazazi kuhusu hilo kisha nitakupigia simu kukujuza siku mtakayokuja". Nilimwambia mahmoud. Nilifanikkwa kumwambia mama kuhusu swala hilo japo ilikuwa ni ngumu kumueleza lakini ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na mimi nilikuwa nimeshaanza kuingiwa na tamaa na hamu ya ndoa. Baada ya kumshirikisha mama jambo hilo naye akamwambia baba, baba alililpokea vyema na wakapanga siku ya kuwaiita wazazi wake na mahmoud waje nyumbanini kwetu. Baada ya siku mbili wazee wake na mahmoud walikuja nyumbani kuleta mahari na kupanga mikakati ya siku ya ndoa kwasababu hawakutaka swala hilo lichukue muda mrefu. Walimaliza kikao cha mipango yao bila shida na tayari wakapanga tarehe maalumu ya siku ya ndoa. Kutokana na ndoa ilipangwa kufanyika wiki mbili zijazo ilinilazimu nikaombe ruhusa kazini ya mwezi mmoja ili nipate muda mzuri wa kujianda kwaajili ya jambo hilo......................... ITAENDELEA

at 4:43 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top