Bikira yangu:12 "Nina mwezi sasa nipo huku na tayari nimeshaanza bihashara zangu mwenyewe, ilimlazimu mzee anipatie na mtaji kabisa ili nikifika huku nianze kufanya bihashara." Alisema mahmoud kisha nikamuuliza tena. "Kwahiyo huyo mchumba unayemtafuta umeshampata? "Hapana, ila nahisi yupo njiani, kama sikumpata leo basi hata kesho nitampata kwa uwezo wa mungu." Alisema mahmoud "Unajua kwenye kufanya uchaguzi wa mtu wa kumuoa unatakiwa uwe makini sana, usije ukakurupuka then baadae ukajilaumu, sijui kama unalijua hilo." Nilimuuliza tena mahmoud. "Yeah, nalijua hilo ndio maana kwenye uchunguzi wa kumtafuta wa kumuoa natembea na vigezo vya msichana ninaye muhitaji kichwani mwangu, kama nitampata ambae kidogo amevikaribia vingezo ninavyovihitaji basi huyo ndio atakuwa mke wangu, japo ni ngumu sana kumpata mwanamke aliyekamilika kwa sifa ninazozitaka." alisema na kukaakimya. "Ni kweli, kwani wewe unataka msichana aliye na sifa zip!."? Nilimuuliza tena. "Kwanza kabisa awe mcha mungu, awe mwenye huruma na upendo kwa watu wote, awe mwenye heshima bila kuzingatia rika hapa namaanisha amuheshimu mkubwa na mdogo, uzuri pia ni sehemu ya vitu ninavyo hitaji, laki uzuri huo utakuwa bora zaidi kama bado atakuwa na usichana wake yaani hakuwahi kuchezewa hata siku moja na hilo ninalizingatia sana. Alisema mahmoud, lakini moyo wangu ulipasuka sana baada ya kusikia kwamba bikra ni kitu anachokizingatia kwenye utafutaji wa msichana amtakae. Nilianza kujihisi mwenye bahati mbaya coz fikra zangu zilinituma kwamba wanaume wote watakuwa wanazingatia vigezo kama hivyo nilijihisi kama mtu nisiye na thamani, moyo uliniuma ghafla nikaanza kumfikiria vuai kwa ubaya alionitendea. Nilitamani kulia lakini nilijikaza coz sikutaka mahmoud ajue mauvu niliyonayo. Nikaanza kujitafakari mwenyewe kwamba siku ikitokea mwanaume kanipenda then asinikute na sifa ya kuwa na usichana wangu sijui itakuwaje. Na istoshe kipindi hicho nilikuwa tayari nimeshaanza kuitamani sana ndoa, nilihisi muda wa kuolewa umefika lakini kila nikijiuliza ni nani atakaenioa? swali langu halipati majibu kabisa. Niliumia sana baada ya kutafakari hayo, machozi yalikuwa yameshafika mlangoni yakisubiri kutoka tu. Ghafla mahmoud akanikatisha mawazo yangu kwa kuniita........ "Zuleiha, zuleIHA, ZULEIHA vipi mbona umekuwa hivyo, tatizo nini? Au nimekukwaza ktk mazungumzao yangu, labda nimeongea vibaya kuna kitu hujapenda? aliniuliza mahmoud. "Hapana kuna kitu nimekumbuka tu ndio maana nimekuwa hivi, ila ondoa shaka kuhusu mimi, nipo ok". Nilimaliza kwa kumjibu hivyo lakini kimuenekano sikuwa poa hata kidogo. Mahmoud akaniuliza tena swali la kunichoma moyo wangu...... "Hivi zuu unafikiria nini kuhusu ndoa? inamaana hadi hapo ulipofika bado hujaamua kuolewa!!!? Nikacheka kicheko cha uwongo kisha nikamwambia.............. "Muda wangu wa kuolewa umefika lakini siku hizi wanaume hawaoi". Nilisema kiutan utani japo ilikuwa inanikeleketa. "Aaaaaaaaaah No sio wote , kuna watu wapo tayari kuoa muda wowote kuanzia hivi sasa lakini na wao wanasema hivyo hivyo kama unavyosema wewe." Sikusema tena kitu kingine nilianza kuhisi kuchoka na mazungumzo yale ikanilazimu kumwambia mahmoud muda wangu wa kururdi home ndio huu. "Sawa hakuna shida tujiandae tuondoke" . Alisema huku tukiinuka mahali tulipokuwa tumekaa. "Waite wenzetu tuondoke" . Nilimwambia mahmoud ila cha ajabu pale tulipowaona mwanzo walipokuwa wamekaa hawakuwepo wameshaondoka. "Haa wale hutowaweza, wamechezeana pale wakaamshana vilivyolala then wameondoka kurudi hotelini. Alisema "Wewe umejuaje"? Nilimuuliza "omy alinitumia msg wakati tupo hapa hapa kwamba wanarudi hotelini kufanya yao". Alisema mahmoud "Ok, basi sisi tuondoke" nilimwambia. wakati tunaondoka nikamsikia mahmoud akisema........ "Zuu vp na sisi tukiwa couple kama wenzetu huoni kama inapendeza?" alisema japo ilikuwa kiutani utani lakini kama ilibeba ujumbe wenye kumaanisha. "Mmmh! Kwasasa tafuta kwanza mwenye vigezo unavyo vitaka" Nilimjibu. "Mbona nimeshampata muda mrefu sana, yani nimempata tangu tunaanza safari ya kuja huku yani kilichobaki ni kwenda kwao tu". Alisema mahmoud. "Alaaa kumbe upempata? Sasa mimi wa nini tena?" nilimuuliza. Wakati tukizungumza hayo yote tulikuwa tukitembea kuelekea kwenye usafiri wa kuturudisha nyumbani. Mara nikashangaa mwenzangu kanishika mkono jambo ambalo hakuwahi kulifanya tangu tumeonana ikanilazimu nisimame na kumgeukia kisha nikamuuliza........ "Tatizo nini mahmoud"? Nilimuuliza "Zuleiha wewe ndio msichana mwenye sifa na vigezo ninavyo vitaka tafadhali naomba uwe mke wangu, naomba nikuoe, naomba unikubalie ili nijione mwenye bahati, naomba uniambie ni siku gani niwatume wazee wangu waje kwenu? Alisema maneno hayo kisha akaa kimya akisubiri jibu kutoka kwangu. Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nikamwambia........ "Samahani mahmoud naomba unipe muda. "sawa mie kesho nitakupigia simu kukukumbushia swala hilo" aliongea na kunishika mkono na kuanza kuondoka. Nilikuwa naogopa sana wakati amenishika mkono coz tayari aibu ya kimapenzi ilikuwa imeshaanza kuniingia, hisia zangu zikawa tofauti na mwanzo tulivyokuja. Sikuongea tena kitu chochote hadi tulipopanda boti, japo alijitahidi kunisemesha vitu tofauti tofauti lakini sikuweza kumjibu ipaswavyo kwasababu ya haya nilizokuwa nazo. Wakati nipo kwenye boti mara mawazo yangu yakaelekea kwa vuai nikaanza kumkumbuka vuai, kwa visa vyake, utani wake na mambo kibao kuhusu yeye, ila kila nikikumbuka tukio alilonifanyia moyo unaniuma sana na mara pengine nikaanza kumlinganisha mahmoud na vuai, nikihisi kabisa huyu anaweza akawa kama vuai... Nilishtushwa na sauti ya mahmoud akiniambia..... "zuu tumefuka mbona huinuki? Nikasimama haraka haraka na kuanza kutelemka ktk boti ile. Wakati natelemka nilisikia sauti tofauti na ya mahmoud ikinisemasha....... "Zuleiha habatri yako"? Ile nageuka kumtambua aliyenisalimia ni nani, kumbe alikuwa ni vuai ktk viunga vile vya kupandia boti............... ITAENDELEA

at 4:43 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top