Home → simulizi
→ Bikira Yangu :11
Siku moja nipo kazini ktk majukumu yangu ya kila siku nilitumiwa email na mgeni mmoja akihitaji nimfanyie arrangement za spice tour, nilifanya hivyo na akaniambia angependa sana uwepo wangu kwenye hiyo tour weekend ijayo yani alihitaji sana kampani kutoka kwangu.
Ilikuwa ngumu sana kumkubalia kutokana na ratiba zangu zitakuwa zimenibana mbali na ratiba kuwa taiti lakini pia nikitaka siku hiyo niwepo nyumbani na ndugu zangu.
Aliniomba kadiri awezavyo, nikajikuta nikimkubalia kwa masharti mapesi ya muda. Tulipanga mikakati yote, ni wapi safari yetu itakapo anzia na kumalizikia, na tukakubaliana kwamba tunakutana maeneo ya kazini kuwasababu yeye hakuwa anajua sehemu nyingi sana za hapa mjini unguja kutokana na ugeni wake.
Jumamosi ikafiaka, nikajiandaa kama kawaida na kuelea ktk maeneo ya kazini kwetu hapo ndipo tulipopanga kukutana. Baada ya kufika eneo lile nilimpigia simu ili kujua ni sehemu gani alipo. Na akanijibu nimsubiri kwa dakika kama kadhas atakuwa tayari amefika.
Nilimsubiri ndani ya dakika chache akawa amefika eneo hilo na tayari kwa kuanza safari, wakati tukiwa tunatembea taratibu kuelekea kwenye usafiri yule mgeni aliejulikana kwa jina la mahmoud, alisema kuna rafiki yake yupo sehemu inabidi tukampitie. Nilihitaji kufahamu mahali alipo rafiki yake huyo, na akanambiwa kwamba yupo hotel ya jirani kutoka ktk hoteli niliyokuwa nikifanyia kazi.
Kabla hatujafika katika hoteli hiyo bahati nzuri huyo rafiki yake na mahmoud alikuwa anakuja mahali tulipo sisi, ila aliongozana na msichana mwenye asili ya kiarabu.
Tuliungana pamoja na safari ikaanza kuelekea ktk kisiwa kimoja kilichopo hapa unguja kilichojulikana kwa jina la prison iland. Kufika katika kisiwa hicho ni lazima tukodi boti ndogo zinazofanya kazi ya kuvusha watu wanao hitaji kwenda ktk kisiwa hicho.
Tulifika salama na tukaanza matembezi ya hapa na pale huku tukipata historia fupi ya kisiwa hicho kutoka kwa waenyeji mahali hapo, lakini baada ya muda kidogo wale wenzetu wawili ambao ni rafiki yake na mahmoud na yule msichana mwenye asili ya kiarabu walitoweka ghafla kusiko julikana. Nilimuuliza mahmoud...........
"Hawa wenzetu wako wapi"?
"Usihofu kuhusu hilo hao ni mtu na mpenzi wake, huyo msichana ametoka oman kaja kwa mpenzi wake ambaye ni huyo rafiki yangu anayejulikana kwa jina la omar, ni mwenyeji wa hapa hapa unguja". Mahmoud alieleza kwa kifupi baada ya kutaka kufahamu wawili wale walipo alekea. Lakini pia kama sikuamini hivi niliposikia mahmoud ameniambia kwamba yule binti yule ametoka oman kwaajili ya mwanaume, ikanilazimu nimuulize tena.......
"Inamaana huyo dada katoka oman hadi huku kumfata huyo rafiki yako tu!!!!?"
"Ndio, si unajua mapenzi tena yalivyo na nguvu alafu istoshe huyo msichana kwao anabanwa sana na wazee wake, sasa ameona akimwambia omar amfate oman anaweza akauliwa coz wazee wa binti huyo ni wakorofi sana na wanauwezo mkubwa kifedha kutokana na bihashara ya mafuta". Alisema mahmoud wakati huo tukiwa tunatembea sehemu mbali mbali ktk kisiwa kile.
Nilishangaa kidogo kusikia taarifa ya binti yule wa kioman na kujisemea kimoyo moyo kwamba kuna watu wanapenda.
Baada ya muda kidogo tukiwa kwenye matembezi yetu tulifika katika sehemu iliyoonekana kuwa nzuri zaidi, ilikuwa ni bustani nzuri iliyokolea ukijani na minazi iliyoruhu upepo mwanana kutoka baharini, mahmoud aliniomba tupumzike ktk eneo lile lililo onekana kuwa na watu wachache sana tena kila mtu na mpenzi wake.
Nasi tukakaa ktk eneo lile ila kwa mbaali tukawaona wale wenzetu wakiwa kwenye mahaba mazito ila wao hawakutuona sisi. Kitendo cha kukaa pale ndio ikawa nafasi pekee ya kupata fursa ya kujuana na mahmoud kwa uzuri zaidi, tuliongea mengi sana na kila mmoja alijitambulisha kwa mwenzie na mahmoud alikuwa mtu wakwanza kutaka kunifahamu mimi.............
Nilimueleza background yangu kwa kiasi chake, ila alionekana hasa ni mtu mwenye kuhitaji sana kufahamu maisha yangu ya kimahusiano. Sikutaka afahamu lolote kuhusu maisha yangu ya mahusiano coz nilikuwa nikikumbuka liletukio nililofanyiwa na vuai roho yangu iliniuma sana, japo nilimuongopea kwa kumwambia nilikuwa na mchumba lakini hakufanikiwa kunioa na wala hakuwahi kufanya jambo lolote ktk mwili wangu. Na kumsisitizia kwamba mimi bado nipo kama nilivyo zaliwa.
Baada ya kumueleza hayo mahmoud naye akanieleza historia yake fupi kuhusu maisha yake..............
"Zuleiha, mimi nimezaliwa hapa hapa unguja, baba na mama yangu ni watu wa hapa hapa, lakini kwa sasa wapo dubai, mzee aliamua tuhame kutokana na bihashara zake zipo dubai, aliona itakuwa ngumu kuacha familia yake hapa then yeye akaishi huko, ikamlazimu ahamishe familia nzima , wakati huo nilikuwa darasa la sita. Tangu tumehamishia maisha yetu dubai kutoka kipindi hicho ndio nimearudi tena zanzibar hivi sasa" Alisema mahmoud kisha akaendelea tena.
"Kilichonifanya nirudi hapa zanzibar ni kutokana na wazee kutaka kunitafutia mchumba huko huko dubai, nilikataa hayo mawazo yao na nikawaambia kwamba maisha yangu nataka yawe Zanzibar na huko ndipo nitakapo tafutia msichana wa kumuoa. Ilikuwa ni ngumu sana mzee kukubali lakini ilimlazimu afanye hivyo kutokana mimi mwenyewe ndio nimeshaamua." Alisema mahmoud kisha nikamuuliza tena.......
"Unamuda gani tangu umetoka huko dubai?
"Nina mwezi sasa nipo huku na tayari nimeshaanza bihashara zangu mwenyewe, ilimlazimu mzee anipatie na mtaji kabisa ili nikifika huku nianze kufanya bihashara.............................
ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: