Bikira Yangu :10 kipindi nafika chumbani tu vuai alipiga simu lakini sikutaka kuipokea, akapiga tena sikupokea , nilifanya hivyo zaidi ya mara nne alipo piga kwa mara ya tano ilinilazimu kuipokea na mazungumzo yalikuwa hivi. "Hallo" alisema vuai "Nakusikia" nilimwambia "Najua nimekukosea sana zuleiha mpenzi wangu, najua hutaki kabisa kusikia chochote kutoka kwangu, najua nafsi yako imekata tamaa kabisa juu ya mapenzi yangu, najua utaniweka kwenye kundi la wanaume wabaya wasio na huruma tena wauwaji. Yote hayo nahisi nafsi yako ndivyo inavyofikiri, sitaki kupingana na fikra zako wacha nizipe asilimia zote kuwa mimi naweza nikawa katika makundi ya wanaume wa aina hiyo". Alisama vuai kisha akaendelea tena "Naogopa kumsingizia shetani kwamba amenipitia kufanya yote niliyokufanyia ila kitu ninachotaka kukuweka wazi ni kwamba nimefanya hayo kwa lengo moja tu, nalo ni kuokoa penzi langu kwako, ni ngumu sana kwa sasa kunielewa kwamba nilitaka kuokoa penzi langu kwako kivipi, ila ninacho amini mimi ni kwamba japo nimepata nafasi ya kufanya tendo hilo bila ridhaa yako nahisi mawazo yangu ya kuwa na wewe daima yatatawala kwenye akili yako". Alisema vuai kisha akaendelea tena "Zuleiha mamie sasa ninaweza nikaamini kwamba utakuwa wangu wa maisha japo si kwa asilimia zote mia moja, ila ninachoomba mawazo yako yawe sawa na yangu. Nimeshindwa kuvumilia kufanya hivyo hadi tutakapofunga ndoa kwa kuhofia kukukosa kwa kuolewa na mwanaume mwengine. Zuu my love mi nipo tayari kwa lolote kwako tafathali niambie ni lini niwatume wazee wangu waje kwenu?" vuai aliongea kisha akamalizia kwa kuniuliza swali hilo. Kwakweli nilishindwa hata ni mjibu nini kwakuwa kipindi anazungumza yote hayo nilikuwa nalia kupita kiasi, sikutaka kabisa kuamini uwongo wake ila nilihisi hizo zitakuwa ni njia za kutaka kunichezea zaidi mwili wangu. "Vuai naomba unisikilize kwa makini sana, kuanzia leo sitaki unitambue kama mpenzi wako, sitaki unifatilie, sitaki mazoea na wewe. Wewe ni muuwaji kama umeweza kuniwekea madawa kwenye kinywaji kisha ukanibaka unadhani naweza nikakuamini kama unataka kunioa? Huna malengo yoyote na mimi ulichokuwa ukikitafuta kwangu umekipata, tafadhali sana naomba uwachane na mimi kabla hili swala halijawa kubwa zaidi". Niliongea kwa hasira na machungu ya hali ya juu huku machozi yakimiminika, sikuishia hapo nikaendelea tena. "Zawaidi uliyonipa ya kunibaka inatosha sana nadhani ilikuwa ni dhamira yako ya kulipiza kisasi cha kukudondoshea simu yako, hongera kwa kufuzu hilo lakini kaa ukijua kuna leo na kesho, leo umenifanyia mimi hivyo kunasiku utamfanyia mwengine ambae hatokubaliana na ufira'uni wako. Mungu atanilipia insha'allah. Nilimaliza kuongea na kukata simu, moyo ulikuwa unaniuma sana nilitamani nipige kelele lakini sikuweza kufanya hivyo kwa kuhofia wazazi wangu. Punde kidogo nikasikia mlango wa chumbani kwetu unafunguliwa, alikuwa ni mdogo wangu anakuja kulala, nilijifunika shuka gubi gubi na kugeukia ukutani ili asigundue chochote kuhusu mimi. "Dada usiku mwema" alinambia mdogo wangu sikuweza kumjibu kwa kuhofia kigugumizi cha uchungu na hasira labda atafahamu kwamba nilikuwa nalia. Nae akajifunika shuka akalala. Kukawa kimya kwa dakika kadhaa mara simu yangu ikaanza kuita tena nilipoishika kuitazama alikuwa ni vuai nilikata na kuizima kabisa................................ Siku mpya ikawajia ilikuwa ni jumamosi, niliamka kufanya shughuri zangu kama kawaida lakini kwa bahati mbaya mama alianza kuwa na wasi wasi na mimi coz sikuwa kama nilivyozoeleka, mama aliniita........ "Zuleiha hebu njoo hapa, wewe unatatzio gani mbona upo hivyo mwanangu, tangu asubuhi umeamka nauona kabisa haupo sawa, tatizo nini mwanangu?" Mama aliniiuliza. Sikuwa na jibu zadi ya kumwambia "Najisikia vibaya, tumbo linaniuma tangu jana usiku" "La kawaida au?" Aliuliza tena mama "Hapana" nilijibu Nilivyojibu hivyo mama akajiongeza litakuwa tumbo la Hedhi, kisha akaniambia baadae nitaenda kukuchumia majani flani hivi kwa mama choro uyachemshe unywe huwa yanatuliza maumivu" Nikaitikia "Sawa mama" ila kimoyo moyo nikajisemea laiti mama angejua sidhani kama angejisumbua kwenda huko kutafuta hiyo dawa. Weekend iliisha japo haikuwa poa sana kwa upande wangu, jumatatu niliingia chuo kama kawaida, sikutaka kabisa kuwasha simu yangu. Lakini ilipofika muda wa lunch ilinilazimu niwashe, nilipo washa tu punde simu ikaingia alikuwa ni vuai, sikupokea mara muda kidogo zilianza kuingia msg nyingi sana za kuniomba msamaha, sikujali meseji zake nikazima tena simu. wakati natoka chuo vuai alinifata na gari kama kawaida , alinisubiri kwenye sehemu aliozoea kunikuta, nilipoiyona gari ya vuai sikutaka kabisa kuikaribia wala kuonana nae, nikapitia nji nyengine kwemda nyumbani. Nilijitahidi kumkimbia vuai kwa takribani mwezi mmoja na namba ya simu nikabadili. vuai alifanya kazi ya kuwatuma marafiki zangu kila kukicha ila sikutaka kabisa kuwapa nafasi ya kunieleza kuhusu vuai. Siku zikaenda mazoea na vuai yakapotea kwa kiasi fulani Mara nikahitimu masomo yangu, nikaingia mtaani rasmi nikiwa si mwanafunzi tena, nikawa nafanya kazi ya ku_apply kazi sehemu mbali mbali. Kwa uwezo wa mungu nikafanikiwa kupata kazi ktk hotel iiyojulikana kwa jina la Double tree iliyopo mjini unguja. Niliajiriwa kama Reservation ktk hotel hiyo. Siku moja nipo kazi ktk majukumu yangu nilitumiwa email na mgeni mmoja akihitaji nimfanyie arrangement za spice tour nilifanya hivyo na akaniambia angependa sana uwepo wangu kwenye hiyo tour weekend ijayo yani alihitaji sana kampani kutoka kwangu........................................................ ITAENDELEA

at 4:42 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top