Home → simulizi
→ Bikira yangu:14
Walimaliza kikao cha mipango ya harusi bila shida na tayari wakapanga tarehe maalumu ya siku ya ndoa. Kutokana na ndoa ilipangwa kufanyika wiki mbili zijazo ilinilazimu nikaombe ruhusa kazini ya mwezi mmoja ili nipate muda mzuri wa kujianda kwaajili ya jambo hilo.
Nilifanikiwa kupata ruhusa na bila kupoteza muda nikaanza kutawa, yani kwa kipindi hicho kilichobaki kabla ya ndoa yangu nilikuwa nakaa ndani tu.
Kwa muda wote niliokuepo ndani kuna muda nilimfikiria sana vuai hadi kufikia hatua ya kutaka kumtafuta ila kilichokuwa kikinizuia ni kukosa namba zake za simu, lakini pia kuna muda nilijilaumu kwanini nimedanganya, hivi ikatokea mahmoud akanikuta sina hiyo bikira ni maamuzi gani atachukua. Mbali na mawazo yangu hayo nilijipa moyo kwamba mungu ndiye muweza wa yote hivyo namuachia yeye kila jambo.
Kadiri siku zilivyokuwa zikizidi kukatika ndipo hofu ilikuwa inachukua nafasi kwa kiasi kikubwa sana, kuna muda niliwaza kumshirikisha mama juu ya hilo labda angenisaidia lakini sikuweza kutokana na kuhofia fedheha.
Siku zikakatika yani terehe ya kuifikia ndoa ikawa ipo karibu. Siku mbili kabla ya ndoa yangu mama alinifata na kuniuliza baadhi ya maswali................
"Zuleiha mwanangu unakwenda kuolewa lakini ninachokuomba nijue kitu kimoja tu kutoka kwako, mwanangu mimi na baba yako tumekulea ktk misingi mizuri kabisa na hatukutaka hata siku moja tupate fedheha ya kushindwa kukulea vyema na ndio maana tulijitahidi kufanya kila namna ujue zuri na baya ili usije ukafanya vitu kwa kushawishiwa bila kujua, mwanangu hebu niambie hadi umefikia hatua hii unauhakika hukuwahi kucheza michezo ya ajabu? Aliuliza mama
"Michezo ya ajabu!!!! Ndio michezo gani hiyo mama? Nilimuuliza
"Hapa namaanisha kwamba hukuwahi kuingiliwa kimwili na mwanaume yoyote? Aliuliza tena mama.
Kabla sijamjibu nilishtuka kidogo kusikia hivyo ikanibidi nikae kimya kwanza kwa dakika kadhaa. Kisha nikajawa na hofu ila sikutaka kumwambia mama ukweli nilichomjibu ni kwamba.....
"Ondoa shaka kuhusu mimi mama angu kila kitu kipo sawa, sijawahi kufanyiwa chochote kibaya". nilimjibu na kukaa kimya.
"Nimefurahi sana mwanangu kusikia hivyo na hilo ndilo tulilotegea kutoka kwako. Alisema mam
Siku moja kabla ya ndoa, kungwi wangu alikuja nyumbani asubuhi na mapema kabla ajaanza kufanya lolote aliniita ktk chumba fulani hivi. Kwa akili ya haraka haraka mi nilijua anataka kunifundisha mambo yanayohusu ndoa ila cha ajabu akaanza kuniuliza swali aliloniuliza mama siku moja iliyopita.
"Binti unauhakika hujawahi kuingiliwa kimwili tangu umezaliwa? Kwasababu mi nakuuliza hivi nataka kujua, na kama utakuwa uliingiliwa tunaweza tukakusaidia kwa namna moja au nyengine. Alisema kungwi
Nilijawa na hofu baada ya kusikia tena swali hilo, yani nilibakiza asimia chache sana kukubali kwamba nilishawahi kuingiliwa kimwili. Nilitamani kulia ila nikazuga kama ilivyo kawaida yangu
"Hapaana sijawahi kufanywa jambo lolote". Nilijibu na kukaa kimya.
"Sawa binti, kama ni hivyo hongera sana". Alimaliza kwa kusema hivyo.
Siku ya ndoa ikawadia, ndoa ilifungiwa nyumbani kwetu, watu walikula vyakula vya kutosha na kufurahia, harusi ilikuwa kubwa kiasi chake.
Baada ya pirika nzima za harusi, ilikuwa imeshatimia saa moja kasoro jioni, ndugu kutoka upande wa kwao mahmoud walikuja na magari kibao kuja kunichukua nikaanze maisha rasmi ya ndoa. Nilikusanyiwa kila kilicho changu ile hali wazee wakiamini kuolewa ni jambo jema na si busara baada ya siku kadhaa nirudi tena nyumbani kwetu.
Nilipewa wosia wa kila namna na ndugu zangu, jamaa pamoja na rafiki zangu, wote walinisisitiza kuhusu maisha ya ndoa, na walinitaka niwe mvumilivu kwa kila jambo.
Tulifika kwao na mahmoud, nibadilisha nguo na kuvalishwa gauni jengine lililoandaliwa kwaajili ya honeymoon, kwakweli gauni lile lilimvutia kila mmoja aliyefika mahala pale. tuliingia ndani ya gari kwaajili ya kuelekea hoteli moja iliyojulikana kwa jina la sea clif iliyopo nje kidogo ya mji wa unguja, tulifika na kupokelewa vyema na wahudumu wa hoteli hiyo na moja kwa moja tukapelekwa kwenye chumba maalumu kilichoandaliwa kwaajili yetu.
Usiku wa kwanza wa fungate uligubikwa na vitu vingi sana. Tulipofika chumbani mahmoud alinisogelea kwa mahaba karibu yangu na kunibeba kuniweka kitandani, wakati huo nilikuwa naona haibu sana..............................
ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: