Home → simulizi
→ STORI TAMU MALKIA WA JELA SEHEMU 03
*🅱 professional love*
....................................
Alipofika mama yake alishangaa kuona akiwa analia na kuamua kumwuuliza ni kitu Gan ambacho kimemsibu
"Kulikon tena tiyar mmesha udhiana huko maana hamkawii mnakuwa Kama watoto wadogo....Haya kafufanyaje mwenzio ?
"Mama BEN Leo wakunifanyia mie hiv kweli mama
"Sasa usiponieleza Mimi sintojua nikusaidiaje hebu nambie moja kwa moja nini tatzo
"Mama BEN kila siku Ana amka saa kum na moja na kusema ratba ya kazn imebadilika kwakuwa naamin tunapendana nikaamn itakuwa kweli sikutaka kumwuuliza DAVID kumbe ananiongopea Mimi na kwenda kulala na wanawake wengine gest mama" Aliangua kilio
"Hebu nyamaza kwanza usilie haya yote umeyataka Mimi na mama yako mdogo tulikwambia BEN hakufai mtoto ukang'ang'ana unayaona sasa anayokufanyia sasa basi nataka uachane nae na kuanzia Leo urud nyumban
"Eeeh mama siwez kurud nyumban mama ile ni nyumba yangu isitoshe BEN ni Mme wangu Nina ndoa nae
"Mmh! Kumbe umekuja kunijarbu siyo Kama unampenda umeijia nini hapa ungejua hilo simngeyamaliza nilivo simpend Mimi huyo mwenzio nilijua atakusumbua nanitahakikisha unaachana nae "
LINDA aliamua kunyanyuka na kurud chumban kwake
BEN baada ya kufika nyumban hakuweza kukuta mtu na geti likiwa limefungwa ilimbid aondoke na kuelekea kazn
Baada ya siku kadhaa kupita ilimbid LINDA aweze kukutana na DAVID na kuweza kuongea nae
"Shemej Kama nilivokuambia BEN amebadilka mno sijui n kwanini simwelew inafikia hatua ananiongopea ofisn mnaingia saa kum na mbili anaamka saa kum
"Shem ulifanya vbaya kuto kuniuliza BEN nimchelewaj mmoja mzur tu pale ofisn kila mtu anamjua yupo pale kwaajil yangu ni kweli amebadilika inafikia hatua hata naona aibu nikiwa Kama mtu wa karibu niliyemtafutia kazi pale
"Shemeji nadhan unajua ni kias Gan ninavyompenda nilikuwa nikigombana na mama pamoja na mamdogo kwaajili ya BEN ili tu niweze kuwa naye hatiamye tumefunga ndoa nyumba yangu nimeamua kuandika jina lake halafu Leo kweli inafikia kunilpiza haya
"Shem mim nitapanga muda niongee nae Kama atashindwa kubadilika siyo sir nitashindwa nimteteaje maana hata kazn watamwondoa
"Ukiongea nae utakuwa umenisaidia sana anayonifanyia mpk najutia maamuz yangu
"Usijali Shem atabadilika tu
"Nakutegemea Sana Shemeji yangu nisaidie
Katika maeneo ya nyumban BEN akiwa seburen anakunywa Soda huku akitazama TV alinyanyuka Mara moja na kuelekea chumban kufuata kitu TABU akawa ameingia ndan alipokuta ile soda mezan alimimina kwenye glass aliokuwa ananywea BEN na kuanza kunywa huku amesimama akiwa ana pepesa macho kwenye mazingira ya pale seburen Muda huo huo akawa anaingia LINDA akaweza kumkuta TABU pale seburen
"Wewe ni nan naunatafuta nini nyumban kwangu "Aliuliza LINDA
"Hhahahaa pole kumbe bado unakibarua Eeh .....hujanijua Mimi ningependa nikuulize wewe "TABU alimjibu kwa dharau
Ilimbid LINDA aanze kupaza saut akimwita BEN ,BEN alitoka hajui kinachoendelea huku na CD ya movie mkonon ambayo alikuwa ameifuata Alipofika seburen alishangaa kumkuta TABU tena akiwa amebebelea ile glass ya soda aliyokuwa akiitumia
"BEN kweli umenichoka hukumbuki fadhira zangu niligombana na mama angu kwaajili yako Nyumba yangu nimefuta jina langu nikaandika lako kumbe hukumbuki nilipokutoa BEN "Aliongea kwa uchungu huku machozi yakimtoka
"TABU umeijia nini hapa ?
"Kwani kunatatzo kumtembelea Mume wangu
"Unasema nni ?
"Unamsikia BEN umenichoka kias hiki umeamua kuniletea mpk mwanamke ndan kweli BEN shukran ya punda..........
"Na haya ndo mateke "Alimjibu TABU huku akionesha kujiamn na kumnyali mbele ya BEN
"We malaya Naomba utoke "Aliongea LINDA kwa sauti ya juu
"Hahaha wakunitoa itakiwa wewe hapa sitoki nitaondoka nikitaka "
"TABU siuende "BEN aljaribu kumwambia akitegemea ataondoka LINDA alisogea mpk mezan na kunyanyua ile chupa ya soda na kutaka kumpiga nayo TABU ,BEN aliwahi kuzuia na kujikuta ikimpata kichwan ile chupa na kuanguka chin LINDA alibaki ameshkilia kipande cha chupa mkononi alikitupa chin na kujitazama mikono yake
BEN damu nyingi zilikuwa zikimvuja kichwan pamoja na puan
TABU alivyoona vile aliamua kuweka glass mezan na kukimbilia nje
LINDA taratibu alisogea alipokuwa ameangukia BEN na kupiga magoti kisha kumwinamia kifuani huku akimtikisa aamke na kilio cha uchungu kikimtoka kilichoambatana na kwikwi Mara ghafla TABU anarud akiwa na polisi "Huyo hapo Afande Mwuuaji "Aliongea TABU mbele ya wale Polisi
Polisi walitoa silaha na kumnyooshea LINDA huku wakimtaka anyanyuke kisha ageuke nyuma kisha afande akatoa pingu na kumvisha na kuweza kuondoka nae kuelekea kituon huku afande mwingine akiwasiliana na askar wenzie kwaajili ya usafiri wa kuubebea mwili wa BEN
LINDA alimaliza kumsimulia chanzo kilichompelekea kuwemo mule ndani "Pole Sana LINDA wanaume siyo watu wazur hata kidogo tukio langu halitofautian na lako hata kidogo "aliongea PENDO na kuanza kumsimulia
Ilikuwa siku moja jion kuna rafiki yangu wa kike aliyeitwa DINA tulipendana Sana siku moja nikiwa sina hili wala lile mida ya saa kumi na mbili jion DINA alikuja nyumban kwangu huku akionekana ni mtu aliyekuja anakimbia nilipojarbu kumwuuliza akanambia amemwona GEOFREY ambaye ni bwana wangu anaingia Hotel na msichana "mh! Utakuwa umemfananisha GEOFREY Hana tabia hyo halafu yuko safar tangu juz " nilimwambia DINA lakin DINA alinisisitiza niweze kwenda nae na kushuhudia kwa macho Moyo wangu ulikuwa mgumu kumwamin bado niliamin GEOFREY alikuwa safarn huenda amemfananisha "PENDO najua ila twende kwanza Kama siyo yeye nitakulipa gharama za usumbufu "Aliongea DINA "DINA we nisumbue tu ole wako "Nilimwambia maneno hayo Kisha nikatoka nae na kwenda kuingia ndan ya gari na kuelekea maeneo ya Hotel alipomwona akiingia GEOFREY nilipofika nilipaki gar kwa pemben na kushuka kwenda kujarbu kuulizia Reception "Dada samahn kuna mgen wangu anaitwa GEOFREY ninatakiwa kuonana nae sijui yupo"Nilimwuuliza yule mdada aliyekuepo pale reception "Aam tuna wagen wengi Sana sasa sijui huyo unayemwuulizia anaitwa GEOFREY nan ?"
"Anaitwa GEOFREY JONAS " Yule Dada aliangalia kwenye kitabu cha list ya wagen aliowapokea
"OK ila Ana mgen tiyar halafu hakuniachia maagizo yoyote kama kuna mtu atakuja"aliongea yule Dada wa Reception "Dada sisi niwafanya biashara tu hata huyo aliyanae ni mfanyabiashara mwenzetu pia "Nilijarbu kumwongopea ili nipate nafas ya kwenda kumshudia kwa macho yangu "Mfanyabiashara Dada labda utakuwa umekosea tu jina au mgen nliyenae majina yamefanana na huyo mtu wako aliyeko hapa yupo na mkewe Leo siku ya tatu sasa unaponambia hivo kwamba n mfanyabiashara mwenzie nashindwa kujua nikusaidiaje " Maneno aliyonambia huyo Dada nilimtizama DINA pemben huku nikijifikiria nitumie njia ipi "Mmh! Saw a ila samahan kwa kukuongopea Mimi n Dada yake sikupenda ujue hilo na GEOFREY alishanipigia Sana simu kuniomba nije kumwona ila kutokana na kazi nyng nikawa sipat muda ikashindikana na hapa nimetoka kazn nikaona acha nionane nae then niende nyumban"Nilijiumauma kwa kuunda maneno ya uongo "Kama ni hivyo bas ngoja nimpigie simu "
"Aa haina haja Dada huniamin "Nilimwuuliza yule Dada "Hapana ila ndo kaz yangu kumtaarifu mteja hili Kama anajua ujio wako kuna watu wengine hawapend usumbufu "Alinambia yule Dada "usijali Bwana "PENDO alitoa noti ya Elfu kumi na kumpatia "Sawa nenda namba 124 " DINA alipotaka kuongozana na Mimi yule Dada aliomba niende mwenyewe kwa kuwa si taratibu za Hotel yao Nilipandisha ngaz mpk sehemu iliyokuwa na vyumba vimepangana nikaanza kuangalia kila mlango kuipata namba 124 na kuweza kuupata Nilishusha pumzi na kutaka kubisha hodi nilikuwa nikisita sita nikajikaza na kuamua kubisha Nikasubr kwa mda kidogo akatoka mwanamke na kuja kunifungulia mlango yule Dada alikuwa amejifunga taulo "Samahan Dada sijui unashida gan maana hatujaagiza kitu chochote huenda umekosea chumba"Aliongea yule Dada baada ya kufungua mlango Nilimpush na kuingia ndan kwa nguvu na kumkuta GEOFREY akiwa amevalia boksa
_______________
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: