Home → simulizi
→ CHOMEZO MALKIA WA JELA SEHEMU YA NNE
By
*B professional love*
SEHEMU YA NNE
..................................
Baada ya kuniona pale ghafla alistuka na kuvuta shuka na kujifunika gubigubi Nilisogea huku nikiwa nimejawa na hasira kisha kulivuta lile shuka na kulitupa chini "Unajificha nini GEOFREY naona safar yako nzur nimeipenda Sana hapa ndo safarin ? "Niliongea maneno yake huku kifua kikiwa kimenibana kwa hasira "PENDO nisamehe Baby shetan kanipitia "Aliongea GEOFREY huku akijibana bana pale kitandani Yule msichana alisogea karbu Nam "we Dada vipi mbona mnapenda kuharbu starehe za watu we huyu unamjua au Umalaya tu " aliongea yule Dada nilijikuta napatwa na hasira na kumsukuma na kumgeukia GEOFREY kutaka anambie kwanini kaniongopea Mara ikasikika kelele ya saut ambayo haikutokea mbali nasi nilipogeuka alikuwa ni yule Dada baada ya kumsukuma alienda kujigonga ukutani na kuumia sehemu ya kichwan kelele zile zilipenya mpk nje ya chumba kile ikawastua mpk watu waliokuwemo ndan ya hotel ile DINA na yule Dada wa Reception waliamua kuja moja kwa moja mpk ndan ya chumba tulichokuepo na kukuta yule Dada akiwa chin kaegemea ukutan huku michiliz ya damu ikitiririka ukutan GEOFREY alitumia nafas ile na kuweza kupenya na kukimbia akiwa amevalia boksa Dada wa reception alibak akitetemeka PENDO alimwomba rafiki yake DINA simu na kuweza kuwapigia polisi na kujisalimisha mikonon mwao
"Mmmh ! Pole Sana PENDO ila lako linaonekana kubwa kuliko langu "Alisema LINDA katika maeneo ya kule Gerezan NYANZARA alipostuka usingizin alishangaa kuona LINDA hayupo kwa kuwa alimtenga na PENDO na kumweka karbu na alipokuwa amelala alinyanyuka na kuangalia alipokuwa PENDO nae hakuweza kumwona alifuata kamba yake na kuanza kuzunguka akiwatafuta na kuweza kuwakuta wakiwa wamejificha wakiongea aliwaamuru wamfuate huku wakiwa wanatembea kwa magoti mpk kwa askar wasimamiz wa Gereza hilo na kuweza kuhadhibiwa na kupewa adhabu ya kufyeka nyasi usiku kucha huku wakilindwa na askar hakuna kula wala kulala mom adhabu yao itakapoisha
Kula wala kulala mpaka watakapokuwa wameimaliza adhabu yao lakin askar baada ya kuona kuwa wamechoka Sana na muda umekwenda aliamua kuondoka nao na kuwarudisha ndan ya gereza baada ya kupambazuka wafungwa wengine wakiwa wameshaamka LINDA na PENDO walikuwa bado wamelala kutokana na adhabu ya Jana pamoja na njaa NYANZARA alisogea mpka walipokuwa wamelala na kuwakurupua waamke haraka na kwenda kuchukua chakula walipochukua Kama kawaida yao walienda kujitenga pemben "PENDO maisha ya hapa yamenishinda nataman leo kesho nijifie nikapimzike tu " Huku vichozi vyembamba vikimlenga machon "LINDA utazoea tu hakun a jinsi kila mtu alikuja Kama ulivo wewe ila wameshazoea na kuona ni hali ya kawaida tu "
"PENDO itakuwa ngumu sisi wakulala njaa tunafanyishwa kaz mpk usiku wa manane tunampepea binadam mwenzetu asiumwe mbu kweli hii haki ?"
"Mmh! Hii mbona ni kawaida ndo maana nakwambia utazoea tu taratibu hakuna namna "
"Kwann huyu NYANZARA anakuwa mkatiri kiasi hiki hajui sisi n wasichana wenzie "
"Usimwazie we vumilia haya yote yana mwisho wake
Baada ya Miez kadhaa kupita LINDA akiwa anafagia fagia eneo la nje ya ofisi ya Askari alitoka askari mmoja umri wake ulikuwa umekwenda kwenda aliyejulikana kwa jina la Afande MUGA na kuweza kusogea pale alipokuwa akifagia fagia LINDA ,,LINDA akiwa hana hili wala lile akawa anaendelea kufagia bila ya kujua kwa nyuma yake kuna mtu Afande MUGA alikuwa akiangalia maungo ya nyuma ya msichana LINDA na kuamua kumsogelea na kumshika LINDA alistuka na kuinuka kumtazama "Binti unafanya usafi " Aliuloza Afande
LINDA aliitikia kwa kutikisa kichwa Afande MUGA aliangaza huku na kule alipoona hakuna askar yeyote yule Alisogea na kumshika LINDA pegan LINDA alimtoa mkono na kurud nyuma "Usiogope Nataka kukusaidia na Kama utakubal nitakacho kwambia utaishi kwa aman Sana humu ndan utakula vizur tofauti na wenzako "
LINDA alikuwa akimtizama Askar yule kwa woga huku akionekana kutetemeka
"Skia Binti kwanza unaitwa nan ?
"LI...LINDA "
"Unajina zur sina Sasa akili yako itakuokoa Nataka uwe mpenzi wangu nahii iwe siri yetu hakuna hatakae jua yoyote yule hapo utaish kwa aman na utakula vizur "
Kabla hawajamaliza kuongea alitokea PENDO
"LINDA fikiria "Aliongea Afande na kuondoka
PENDO alibakia akishangaa bila kujua ni kipi kilikuwa kikiendelea Kati ya askar na LINDA
"LINDA vipi kuna usalama hapa "
"Ndiyo hakuna kitu "
NYANZARA akiwa kwa mbali aliweza kuwaona wakiwa wamesimama pale aliweza kuwafuata na kuwaomba waondoke haraka eneo lile
Muda wa usiku wakiwa ndan ya gereza LINDA alionekana kufikiria Sana maneno aliyoambiwa na yule askar alipokuwa akifanya usaf aliingia katika mawazo mazito juu ya jambo lile PENDO alipomwangalia alimwona hayupo sawa alinyanyuka mahala alipokuwa amekaa na kumsogelea LINDA
"LINDA?!" Alijaribu kumwita lakin LINDA hakuonekana kuwepo eneo hilo PENDO alijarbu kuweka mkono wake mbele ya uso wa LINDA na kuchezesha vidole vyake kujarbu kuona Kama atafanya chochote lakn bado alionekana kuwa na mawazo Aliamua kumshika began na kumtikisa ndipo LINDA akastuka na kujikuta akiropoka "Usinifanyie ivoo"
"Mmh ! LINDA Una nini ?" Aliuliza PENDO "MH! hakuna kitu nimekumbuka Sana uraiani nimemkumbuka mama yangu PENDO "
"Hapana siyo kweli LINDA kuna kitu unanificha "
"PENDO hakuna nitakachoweza kukuficha ni kweli " NYANZARA alipowaona aliwafuata pale walipo "Ni Mara ngapi nawaambia sitaki mkae pamoja " Aliongea NYANZARA kwa saut ya ukali "lakini ............" Alitaka kuongea PENDO lakin NYANZARA alimzuia "Sasa Leo hamto Lala Mtanipepea Mbu mpk asubuh haya nyanyuken " PENDO alinyanyuka haraka pale chini ila LINDA akawa bado amekaa akionesha kukaid amri ile "Wewe ndo mbishi siyo umesha kuwa " Aliongea NYANZARA "Mim nimechoka kila siku sisi Nimechoka mm sifanyi nahitaji kupumzika Kama wewe " LINDA alijibu huku machoz yakim mwagika "Oooooh! Sasa Utakula jeur yako kumbe hunijui vizur Eeeh Huwa huna tabia ya kuuliza wenzio Mimi amri yangu huwa haikaidiwi hata Mara moja utafanya nachokitaka PENDO rudi ukae "
"Ahsanteee" alisema PENDO na kurud kukaa "Binti nyanyuka hapo " NYANZARA aliongea kwa sauti ya juu Wafungwa wenzao walibaki wakiangalia ni kipi kitafuata baada ya LINDA kukaid amri ile NYANZARA aliinama na kumshika mkono kisha kumvuta anyanyuke kwa lazima na kumsukuma mahala ambapo huwa analala kisha kumpatia cha kujipepelea na kumwamrisha afuate Kama alivyoambiwa LINDA alikitupa kile cha kujipepelea NYANZARA alimshika na kuanza kumpiga huku akitaka mtu yeyote asisogee na kuamua ugomvi ule mpaka pale atakapoona inatosha PENDO roho ilimwuuma Sana kwa kile kitendo kilichotokea ila hakuwa na namna ya kufanya kumwokoa rafiki yake LINDA
_______________
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: