STORI; MALKIA WA JELA SEHEMU YA KWANZA .............................................. *🅱 professional love* Kwenye maisha ya kila siku katika ufanyaji wa maamuz ya ufanyaji wa jambo fulan una ulazima wa uhitaji wa ushaur kutoka kwa mtu mmoja wa karibu nawe Ila unapoamua kujichukulia maamuz yako na kufanya jambo baya kwa kunufaisha/kujinufaisha baadae unapokuja kuona madhara yake ndipo uona umuhimu wa kutaka ushaur toka kwa wenzako ikiwa tayar umeshachelewa kwan "NGOMA INAPOVUUMA SAANA MWISHO WAKE HUISHIA KUPASUKA" LINDA ni msichana mrembo aliyebarikiwa kwenye kila idara ikiwemo mvuto pamoja na umbo lake lililowavutia watu wengi mtaani kwao ila kwa bahat mbaya anakuja kupata kesi ya kumwuua mpenzi wake bila kukusudia na mahakama kuamua kumhukumu kifungo cha miaka mitatu jela kutumikia kifungo hicho cha kuua bila ya kukusudia ndan ya Gereza la wanawake LINDA siku ya kwanza anaingia ndani ya Gereza ilimpa wakat mgumu Sana kuyazoea mazingira muda mwingi alijitenga peke yake huku akilia na kujutia makosa yake Kwa kawaida kila gereza lazima utakutana na mtu ambaye usimama Kama kiongozi ndan ya gereza aliyejulikana kwa jina la NYAMPALA ,Kuna binti aliyeitwa NYANZARA ndiye aliyekuwa akiliongoza gereza lile Kama Nyampala Aliutumia udhaifu wa LINDA kwa kuwa alikuwa ni mgen na kumfanyia baadh ya kaz zilizokuwa zikiendeshwa ikiwemo usaf ndan ya gereza na ufyekaj wa nyasi katika maeneo ya nje ya gerezan LINDA alikuwa akiumia Sana moyon na kushindwa kufanya lolote kwa kuwa tiyar limeshatokea Adhabu yake kubwa ndan ya gereza lile iliyokuwa inamfanya alie kila wakat ni majira ya usiku anapotakiwa kukesha macho na kumpepea NYANZARA asiumwe na mbu kuna wakat alishindwa kujizuia na kujikuta akipitiwa na usingiz na kujikuta akiambulia kipigo toka kwa NYANZARA Siku moja wakiwa wamejipanga wanachukua chakula LINDA baada ya kupata chakula chake alisogea na kwenda kukaa peke yake chini ya mti Kuna mfungwa mwenzie baada ya kumwona LINDA amekaa peke yake aliamua kubeba chakula chake na kumfuata alipokuwa amekaa "Habar yako Dada ? Alimsalimia yule Dada ilikujua hali yake "Nzur tu .... Yule Dada aliamua kukaa chin ili waweze kuongea "Nimekuona umekaa hapa muda mrefu unaonekana mnyonge wakat wote ....Unaliaa ..Uchangamki ....Bado hujazoea mpka Leo "Mmmh! Nashindwa kujizuia .. Maisha ya huku ni magumu sijazoea "Ipo siku utazoea tu acha kuwaza changamka Mimi naomba niwe rafiki yako "Saw a "Akatabasamu "Nafurah kukubali hili Aam naitwa PENDO sijui wewe mwenzangu ? "Mimi naitwa LINDA "Woow! Jina zur Sana "Nashukuru Hata lako pia "Kwani Dada wewe hasa kilichokufanya uingie humu ndani ni kitu gani ? "PENDO we acha tu sitaki hata kukumbuka Wakat wakiendelea kuongea NYANZARA aliwafuata na kuanza kuwapiga na kuwataka waondoke haraka na kwenda kujumuika na wenzao kufanya kazi LINDA pamoja na PENDO walinyanyuka na kukimbia kujiunga na wenzao kabla hawajafika mbali Sahan zao walizokuwa wanalia walizisahau NYANZARA aliamua kumrudsha LINDA na kumtaka arudie zile sahan haraka LINDA alirud kuchukua sahan "Mlikuwa mnamwachia nan awatolee okota haraka utokee " Aliongea NYANZARA kwa saut ya ukali LINDA aliinama na kuziokota zile sahan kisha kuondoka huku akikimbia Baada ya wiki moja kupita wakiwa wanafyeka nyas katika eneo la nje ya gereza wakati huo NYANZARA alikuwa amejilaza kidogo kwa pemben chin ya mti wakiwa wanaendelea kufyeka nyasi PENDO alimfuata alipokuwa LINDA "Wewe PENDO umeijia nini hapa huogopi ? "Amelala hawez kuamka sahv yule "Angalia Mimi namwogopa Kama nini sitak matatzo "Hapana bhana usiogope ... Sasa sikia siku ile hatukumaliza kuongea haukuniambia ni nini kimekupelekea uwepo hapa "PENDO siku nyingine Leo haitowezekana acha tufanye kaz kwanza "LINDAA watu wote hawa unafikir hapa hapata isha na hata pakiisha hatuach kufyeka Leo wala kesho "Mmh haya tutakaa kwa wapi Walitafuta sehem nzur ya kuweza kukaa ambayo hawatoweza kuonekana kwa haraka na kuanza kuongea "PENDO unajua tangu nimeingia humu umejitolea kuwa mtu wangu wa karbu mno tena mapema "Unajua LINDA Mara nyingi watu wakiletwa huku hukosa furaha kabisa na kupoteza Raman nzima ya maisha ila unapokuwa na rafiki hautaman hata kutoka "Kwani wewe Una mda gani tangu uingie humu ? "Nina mwaka wa tatu sasa Bado miaka yangu minne mbele niweze kumaliza kifungo changu "Eeeeeeh! Miaka minne na umeshamaliza miaka mitatu humu humu ndan "Ndiyo mbona nimeshaona kawaida vipi wewe mwenzangu "Mingi..Miaka mitatu "Ha! Hyo mingi Mbona midogo je ungekuwa Mimi ....Tuachane na hayo niambie kilochotufanya tuje hapa kuongea "Mmh! PENDO Wanaume siyo watu wazur hata kidogo kuna mwanaume nilitokea kumpenda Sana lakin alichokuja kunifanyia sinto sahau mpk natoka humu LINDA alianza kumsimulia Ikiwa ni mida ya saa kumi na mbili asubuh LINDA akiwa usingizn anajarbu kupeleka mkono wake pemben akijarbu kupapasa papasa na kukuta hakuna anachokitafuta anastuka na kufumbua macho kuhakikisha na kukuta mumewe BENSON hayupo kitandan alijinyoosha huku akipiga mihayo na kujirekebisha rekebisha nywele zake kwa mikono akaamua kutoka kitandan na kusogea mpk kwenye kioo cha kwenye dressing table na kuanza kujiangalia alipoona yupo sawa alisogea mpk karibu na mlango akitaka kuufungua muda huo huo BENSON akawa amefungua na kuingia chumban "Baby ulikuwa wapi ? "Nilienda kazn Mara moja kulikuwa na dharura "Uliamka sa ngapi mbona sikukusikia "Sikutaka kukusumbua nimeamka usiku Sana "Ungeniaga bwana ya Mungu mengi unaweza kupatwa na tatzo "Sorry! siku nyingine nitafanya hvo nilijua ntakusumbua

at 11:04 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top