Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA ISHIRINI.
“Catherine siku uliyoondoka ndani ya begi lako uliacha kitabu chako cha kumbu kumbu, niliweza kusoma matukio yote ambayo uliwahi kukutana nayo hapa shuleni.
Nilijua kwamba ulibakwa na Maloya, nilijua kwamba uhusiki na kifo cha Candy ingawa mwanzo nilikuwa nikikutilia hofu, nilijua jinsi ulivyokuwa na wakati mgumu sana kwa ajili yangu.
Mambo mengi sana hukutaka niyajue lakini kupitia kitabu chako kile niliweza kuyafahamu nilijua hata mpango wako wa kutaka kupoteza mawasiliano na mimi kisa ikiwa ni ule ujauzito.
Vyote hivyo vilikuwepo ndani ya kitabu chako cha kumbukumbu.”
Niliinamisha uso,
“Baada ya muda tulitangaziwa kwamba unatafutwa na polisi, mwalimu alikuwa akipenda sana kutuletea habari zinazohusiana na kesi ya Candy na hadi mwisho nilipata taarifa kwamba umekamatwa Dar na umeletwa huku Mwanza na kufunguliwa kesi, moyoni mwangu niliumia sana niliazimia kukusaidia kwa namna yoyote ile.
Nilifanya mawasiliano na mama yangu mkubwa Happiness ambaye ni mama yake na Martha.”
Moyo ulinipasuka paa, sikuwa najua kitu hiko.
“Niliongea naye nilimwelezea kila kitu nikampatia na kile kitabu chako cha kumbukumbu, aliguswa sana na shida zako na aliamua kukusaidia.”
“Tunashukuru mungu kwamba kila kitu kilienda sawa na Mungu alionekana na hatimaye leo umeachiliwa huru.
Lakini kilichonipa furaha kabisa ni kwamba ujauzito haukuwa ni wa Maloya ulikuwa ni wa kwangu, sorry Candy kwa kukatisha masomo yako.”
“Naomba nikupe kitu ambacho kinawakilisha ombi langu langu la msamaha kwako aliongea kwa uzuni na kwa sauti ya kilio.”
Niliinama tu nilishindwa la kusema.
Niliziba macho yangu na kiganja changu nikibaki nimejiinamia,
“Catherine” aliniita Martin,
“will you marry me?”
Nilitoa kiganja kilichokuwa kimefunika macho yangu
“Say whaaat!!” Alikuwa ameshikilia pete ambayo ilionekana imenakshiwa na madini ilionekana kuwa pete ya thamani sana.
“Yes” aliongea kwa kunong’ona.
Machozi yalinitoka upya, nilimtizama baba yangu alikuwa akilia, shangazi yangu naye pia.
“Yes Martin niko tayari”, nilijibu kwa sauti ya upole.
Alipiga magoti na kunivalisha pete ile kidoleni kwangu ilikuwa ni furaha kubwa kwangu na si kwangu peke yangu bali kwa wote.
“Catherine” wakili Happiness aliniita,
“baada ya dhiki huja faraja” alisema.
“Niwatakie maisha mema ila naitwa Happiness Lutabenza niliolewa miaka kadhaa iliyopita na Denis Lutabenza na kufanikiwa kupata mtoto mmoja tu Martha kabla mume wangu hajafariki. Nampenda sana mwanangu Martin kwa sababu yupo karibu nasi hasa na binti yangu nah ii ni sababu niliamua kukusaidia kwa nguvu zote yani IN THE NAME OF LOVE.” Hapo alicheka.
Nilishituka sana Martin alikuwa akiitwa Martin Lutabenza.
“Martin ni mtoto wa mdogo wa marehemu mume wangu, David Lutabenza.”
Tuliachia tabasamu wote.
Ulikuwa mwanzo wa maisha ya furaha.
Nampenda sana mume wangu Martin maisha yangu yote.
>>>>>>>>>>>>>>>>>> MWISHO<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
Napenda kuwashukuru watu wote ambao mlikuwa pamoja namI tangu mwanzo wa hii hadithi hadi hapa tumefikia mwisho.
Mungu azidi kuwabariki sana natumaini kwamba kuna kitu mmekipata, yani hamkutumia muda wenu bure mmesoma na mmepata kitu.
Lengo kubwa la kuandika hadithi hii ni kwamba kuna vitu nilikuwa nataka mvione.
Watoto wana ndoto nzuri lakini wazazi ndiyo chanzo cha kufeli kwa ndoto za wanafunzi na za watoto wengi.
Inatia huzuni sana,
Tunazaa watoto kwa sababu tunataka kuwa wazazi, lakini mara zote wazazi wengi sana wanakimbia majukumu ya kuwa wazazi.
Watoto wana mahitaji mengi sana.
Ili mtoto aweze kufikia ndoto zake mzazi anahitajika kujitoa kwa hali na mali, ili mtoto huyo aweze kufanikiwa.
Watoto wengi sana wakiharibikiwa mara zote tumekuwa tukiwatupia lawama huku tukiangalia sababu chache tu ambazo zinaonekana lakini tukiacha sisi wenyewe wazazi tunashindwa kujibebesha lawama kwamba sisi ndio tunahusika katika namna zote.
Hata hivyo lawama kubwa nazipeleka kwao wazazi kwasababu wao wanahusika
Watoto wanahitaji muda,
Wanahitaji mtu wa kuwajali,
Wanahitaji mapenzi,
Wanahitaji kuongozwa,
Wanahitaji ulinzi,
Wanahitaji maombi,
Wanahitaji kupata muda wa kupumzisha akili,
Wanahitaji kuchanganyika na watu,
Wanahitaji kusikilizwa,
Wanahitaji uhuru,
Wanahitaji amani na kujifunza.
Watoto wakipata hayo yote ni vigumu sana kwa mtoto kupoteza ndoto zake maana mtoto huyo atakuwa anajitambua kwa sababu tayari ana mahitaji yake yote ya msingi.
Kama wazazi tumekuwa tukifikiria kwamba watoto wanahitaji mavazi, elimu, malazi na chakula basi.
Lakini hayo yote hayatoshi na ndiyo maana ndoto za watoto waliowengi zinaishia njiani.
Watoto wanakuhitaji sana mzazi.
*Mwisho*
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: