Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA TISA.
Haikuhitaji kuambiwa wala kuelezewa mtoto huyu alikuwa kama pacha, hakika alifanana sana na Martin
“Mungu wangu kumbe hii mimba ilikuwa ni ya Martin mtoto kafanana na Martin kheeeh! ni pacha wake kabisa” nilishangaa nesi aligundua mshangao niliokuwa nao
“vipi”
“aanh, mwanangu ni mzuri”,
“yeah umezaa mtoto mzuri sana hongera”, niliachia tabasamu.
Moyo wangu ulijawa na furaha ambayo siwezi kuielezea.
“Mungu hatimaye umeufariji moyo wangu nikurudishie nini mimi nikurudishie nini kiwe sawa na fadhli zako Jehova” nilijikuta nikisali.
Nilisali si kidogo, nilimshukuru Mungu kwa yote ambayo yaliwahi kutokea katika maisha yangu hatimaye mungu umenipa faraja ya milele mwanangu mpenzi.
Nilishindwa cha kuongea ilikuwa ni furaha isiyo na kipimo.
Hatimaye baba, wakili Happiness pamoja na shangazi yangu waliruhusiwa kuja kuniona pamoja na ndugu wa wakili Happiness walifurahi kumuona mtoto huyu mzuri,
“mtoto mzuri sana huyu wa kiume”
Ilikuwa ni furaha isiyo kipimo.
Wakili Happiness alikuja kwa tabasamu,
“unapenda mwanao aitwe nani”, niliachia tu kicheko,
“bado sijafikiria kuhusu hilo” nilimwambia
“naomba mimi nimpe jina.” Alisema
Nilicheka “sawa”
“Nitampa jina kwa wakati wake”,
“nitashukuru.”
Tuliruhusiwa kuondoka hospitalini hapo baada ya kila kitu kukaa sawa.
Baada ya siku kadhaa kupita, baba alishauri apewe jina la muda wakati wakili Happiness akiandaa jina lake.
Mwanangu aliitwa Blessing hakika alikuwa ni Baraka kwangu na kwa maisha yangu.
Kesi yangu mahakamani iliendelea, hatimaye siku ya hukumu ilifika nilisimama kizimbani nikitetemeka sana.
Mwanangu alikuwa amebebwa na wakili Happiness machozi yakinitiririka wakati huo wakili Happiness alikuwa na furaha wakati wote.
“Anafurahi nini wakati hukumu haijatolewa nikifungwa je?” nilisema
Akili yangu haikutuliai kabisa,
“ee Mungu naomba usinitenganishe na mwanangu naomba unipe muda wa kumlea nampenda sana mwanangu.”
Hatimaye muda wa hukumu ulifika, hakimu alisimama kwa ajili ya kutoa hukumu,
“kutokana na ushahidi kutoka pande zote mbili, mahakama imeamua kwamba Catherine Kindamba kuwa hana hatia kwa kuwa hakuhusika na kifo cha Candy, ila Candy alifariki baada ya kushikwa na kizunguzungu na kisha kudondoka na kujingonga ukutani hivyo basi mahakama inapenda kumwachilia huru Catherine Kindamba kuanzia sasa”, nilijikuta nikipiga magoti kizimbani nilisali nilishukuru.
Baba alishindwa kujizuia aliachia machozi kwa pamoja wote walikuja kizimbani na kunitoa na kisha kunikumbatia kwa furaha.
Watu wengi walikuwa wakifatilia kesi yangu siku hiyo nilimwona mwalimu mkuu wa Hanspop Academy Mr. Maige alikuja kunipa hongera
“hongera sana Cathe wewe ni msichana Shujaa sana.”
Nilishindwa kujizuia machozi yalinitoka nilitamani kumuulizia kuhusu Martin lakini sikuwa na shaka kwamba alikuwa ameisha maliza shule kwa wakati huo.
“Asante mwalimu”
“Nashukuru ingawa umepoteza nafasi ya kusoma lakini naamini kwamba kuna siku itajirudia tena, endelea kujipa moyo Mungu yupo pamoja nawe” aliongea kwa upole sana mwalimu Maige na kisha kupotea machoni pangu.
Nilibaki tu machozi yakinitiririka.
“Tulilia kwa furaha mimi pamoja na familia yangu mpya nilimkumbatia mwanangu Bless.
“Catherine” niligeuka na kutizama, wakili Happiness alikuwa akiniita,
“mtoto wako ataitwa Comfort” akimaanisha faraja
Niliachia tabasamu,
“jina zuri sana nimelipenda nahisi nitakuwa na furaha sana kuitwa mama Comfort”, ila mwisho wa yote baba yake atakuja kuamua jina la mwisho mwanae ambalo atapewa.
Maneno yake yalinifariji sana ingawa sikuwa najua ni namna gani ningekutana na Martin, nilirejea nyumbani.
Watu wote waliingia ndani wakili Happiness aliniita
“nimekuandalia zawadi kubwa sana binti yangu, wewe ni sawa na mwanangu. Naomba uipokee zawadi yangu” nilicheka,
“mama” nilijizoeza kumwita mama.
“niambie mwanangu”
“mimi ndiyo ninapaswa kukupa wewe zawadi mama umenifanyia mambo mengi sana”,
“hapana haya mambo yote yasingefanyika hupaswi kunipa zawadi mimi kama unataka kutoa zawadi ipeleke kanisani nimefanya haya yote IN THE NAME OF LOVE”,
“IN THE NAME OF LOVE” nilijiuliza anamanisha nini?
“Sawa nipo tayari kupokea hiyo zawadi yako” aliachia tabasamu
“naomba nikuzibe macho ili usiione. Iwe surprise kwako” alimalizia,
“hasa.. mama nimebeba mtoto si tutajikwaa tudondoke jamani”
“Hamna mimi nitakuongoza”, aliongea kwa utani kama kawaida yake,
Nilicheka tu,
Aliniziba macho na kuniongoza sikujua hata tunaelekea wapi, baada ya kutembea hatua chache hatimaye tulifika ambapo tulipaswa kufika, alinifumbua macho.
Sikuitaka kuamini nilichokiona mbele yangu.
Martin na Martha walikuwa wamesimama mbele yangu walikuwa wamependeza sana Martin wangu alizidi kuwa mzuri na hakika alionekana mbaba nyuso zao zilijawa na tabasamu.
Nilishindwa kujizuia machozi yalinitoka
“Martin” sauti iligoma kutoka,
Martin alilia alijongea polepole hadi nilipokuwa nimesimama,
“Cathe mwanamke wa maisha yangu.”
Alinikumbatia kwa nguvu zote huku akilia,
Furaha iligeuka vilio kila mtu alitokwa na machozi.
Martin alimchukua mwanangu na kumbeba
“my first born” aliongea kwa sauti ya chini.
“Nakupenda sana Catherine”, alisema Martin.
“Nakupenda Martin” nilijibu.
Nilishindwa kuelewa mazingira yaliyokuwepo mahali hapo.
Martin alianza kujielezea.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: