RIWAYA: HIGH SCHOOL 😋😋😋😋😋😋😋 SEHEMU YA SABA. Nilikosa nguvu ya kufanya kitu chochote nilianza kulia upya niliumia sana na kitu alichokifanya baba yangu, furaha yangu ilikuwa imetoweka kabisa kiukweli nilimchukia sana baba yangu, alikuwa ni zaidi ya shetani kwangu, kwa upande mwingine niliilaumu nafsi yangu kwa kusababisha kifo cha mama yangu nilijiona sina thamani tena nililia na nafsi yangu. “Nisamehe mama nisamehe kwa kusababisha kifo chako popote ulipo mama naomba unisikie naomba unisamehe mama yangu”, nililia sana. Maisha yaliendelea ingawa kiakili nilikuwa siko sawa, taaluma yangu ilishuka sana wala sikujali katika hilo niliishi tu ili mradi siku zisogee mbele. Maisha yangu yalibadilika kwa kiasi kikubwa nilikuwa nina hasira muda wote hata hivyo sikupenda tena kuonewa nilipanga mtu yoyote atakaye nifanyia kitu chochote nitalipiza kisasi kisasi kilitawala ndani ya moyo, wangu mtu wa kwanza niliye muwazia alikuwa ni baba, “lazima nitakaporudi nyumbani nilipizie kwa kifo cha mama” nilisema, Niliwaza kumlipizia Candy endapo angenifanyia tukio lolote lile. Sikumhofia tena Maloya, sikuhofia kupigwa kwasababu nilishakuwa sugu nilipigwa sana, sikuogopa kufanya tukio lolote lile kwa kuhofia adhabu au kutangazwa mbele za watu, nilijikuta nimekuwa sugu sikuogopa chochote adhabu kwa upande wangu zilizidi mara nyingi. Maloya alikuwa alinisingizia mambo mbalimbali, nilikuwa nikipokea adhabu mara kwa mara kutoka kwa Maloya kwa makosa ya kusingiziwa nilifanya tu sikuwa nahisi chochote katika moyo wangu. Candy alizidi kunionea kutokana na kwamba yeye alikuwa ni kiongozi mara kwa mara alikuwa akinisingizia makosa na kupewa adhabu, niliona kawaida tu na mara nyingi nilimdharau sikusita kumwonesha dharau kila tulipokutana naye sikulihofia tena kundi lake, chuki zao na dharau zao kwangu zilikuwa ni kawaida sana maisha yangu yaliendelea vizuri na hata ufaulu wangu ulianza kuongezeka. Mawasiliano na baba yalipungua, mara kwa mara alikuwa anajaribu kunitafuta lakini sikuweza kuitikia simu zake alipokuwa akipiga simu ofisini nilipoitwa kwa ajili ya kuongea naye nilikataa, Martin alikuwa akinionea huruma sana kutokana na adhabu nilizokuwa nikipata pale shule, siku yake alinitafta “Cathe sijakuona mda mrefu sana” Nilitabasamu nikamwambia “niko busy sana” “Busy busy na nini aliuliza?” “Jamani kwani hapa shuleni tunafanya nini, niko busy na kusoma” alicheka kisha akaniangalia kwa muda nilijisikia aibu. “Aaaah yaah niko busy na kusoma sasa hivi sitaki kukutwa na matukio yoyote yale ya ajabu”, “uamuzi mzuri sana kwa maana ufaulu ulikuwa umeshuka sana” alisema. “Cathe najisikia vibaya sana kwa ajili yako mara nyingi nakuona katika adhabu inaniumiza sana”, nilitoa tabasamu jepesi kisha nikamwangalia usoni “Marti usijali kuhusu yote haya ninachoangalia sasa ni kufanya kile kitu ambacho kimenileta hapa shuleni kwa sababu hilo ndio lililokuwa tamani la mama yangu na ameondoka kabla sijalitimiza ni lazima nilitimize ili hata uko alipo apumzike kwa amani”, aliniangalia sana kana kwamba sio mimi niliyekuwa nikiongea hivyo, “Cathe umeongea kitu kizuri sana lakini hujui kuwa hizo adhabu zinaweza zikakuathiri kisaikolojia na kimasomo pia?” “Martin siwezi kuruhusu kitu chochote kikaniharibu tena najua kwamba nikiwa mpole nikiwa mkali haya matukio kwangu ndiyo yameshakuwa yangu na hayawezi kuondoka vyovyote vile niwavyo lazima yatanijia siwezi kuyakimbia siwezi kumkimbia Candy siwezi kumkimbia Maloya siwezi kuikimbia shule nitaendelea kupambana hivyo hivyo” niliongea. Alifurahi sana alinivuta na kunikumbatia nililihisi joto lake tulibaki tumekumbatiana kama dakika mbili hivi ilikuwa ni wakati mzuri sana kwangu ambao sikuwahi kuwa nao katika maisha yangu yaliyopita, tuliachiana huku tukitweta, aliachia tabasamu na mimi pia, “uwe na wakati mwema Cathe” alisema na kuondoka. Tukio hilo liligoma kufutika katika akili yangu kabisa kila mara nilikuwa nikifikiria liwazo kutoka kwa Martin, nilihisi nampenda sana Martin. Huyu mkaka niliwaza na kisha nikatabasamu na kuondoka eneo hilo na kuelekea bwenini. Nilipofika bwenini nilipanda kitandani kwangu nikiwa na tabasamu hatimaye katika maisha yangu nimepata liwazo mtu ambaye anaweza akarejesha furaha yangu katika mazingira magumu kama haya, nilifikiria. Niamua kwenda kumwambia wakati tutakapokutana tena baada ya kufikia uamuzi huo nilikuwa nikitabasamu kila wakati, ulipofika wakati wa kuhudhuria kipindi cha dini alikuwepo pia, aliimba vizuri sana moyo wangu ulijawa na furaha na amani tele kila mara nilikuwa nikimwangalia. Tulipotoka kwenye kipindi nilienda nilimshika mkono tukaongozana darasani alikuwa na furaha sana. Tulipofika darasani nilimwambia “Martin baada ya hapa nilikuwa nahitaji kuongea na wewe”, aliachia tabasamu. “usijali bibie” aliongea kwa sauti yake tamu, kisha akaendelea kusoma na mimi nikachukua madaftari yangu na kuanza kusoma. Baada ya muda wa prepare kuisha wanafunzi walianza kutoka madarasani na kuondoka, aliniangalia kisha akanibinyia jicho nikaachia tabasamu tu. Mara baada ya watu wote kutoka alinigeukia na kunitazama “haya niambie bibie”, alisema nilitabasamu alitabasamu pia “Martin” niliita kwa sauti nzuri ya kike, “Naam” “unajisikiaje tunavyoonewa kwa kosa lisilo la kwetu?” “Hamuna mtu ambaye angeweza kujisikia vizuri Cathe kila mtu lazima angeumia na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu” aliniambia. “Pole” nilisema. “Na naomba nisamehe kwa kuwa chanzo cha mambo haya yote kutokea kwa upande wako.” “Usijali Cathe hata mimi pia napaswa kusema sorry kwako kwasababu hata mimi ni chanzo cha haya yote kutokea kwako.” “Aaah kwahiyo kila mtu amwombe msamaha mwenzie si ndiyo?” nilisema. “Mmmh” alicheka “Ndio nisamehe pia na mimi”, Tulicheka wote kwa pamoja. Cathe” aliniita. Nilimwangalia, nilishindwa kumtizama moja kwa moja machoni, “Uliniambia kuna kitu unataka kuniambia nakusikia na utakapomaliza kuniambia unachotaka kuniambia na mimi kuna kitu nataka nikwambie.” “Asa kwanini hukuniambia toka saa zile?” nilimuuliza “Kimenijia ghafla” alisema na kisha akacheka. Na mi nikacheka pia “Ok Martin mara zote huwa najisikia vibaya sana kusemwa au kuhukumiwa kwa kosa ambalo kweli sijalifanya na najua kabisa kwamba sijafanya” “Ni kweli inaumiza” alisema Martin kwa utulivu, “Martin sorry kama nitakukwaza kwa nitakacho kwambia” nilimwambia. “Lakini nimeona kwamba tusiache ibaki midomoni kwa watu nataka iwe kweli kwasababu wewe ni mzuri kwangu” aliniangalia sana, “Cathe are you serious?” “Nataka kuwa na uhusiano na wewe.” “Ngoja na mimi nikwambie ambacho ninatakanikwambie” alisema Martin. <<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA >>>>>>>>>>>>>>>>>

at 11:06 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top