Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA SITA.
“Mama yako mpenzi amefariki dunia” aliongea baba kwa sauti iliyochanganyika na kilio,
“Say whaaat?” niliongea kwa mshituko sana.
“Ni hivyo mwanangu, kazi ya mola haina makosa” Machozi yalinichuruzika mfululizo huku mdomo ukitetemeka nilishindwa kuongea neno lolote.
“Cathe” baba aliinita kwa utulivu,
Nilishindwa kuendelea
Aliongea,
“pamoja na hayo yote nasikitika kukwambia kwamba hutoweza kuhudhuria mazishi yake kwa maana anazikwa leo.”
Maneno hayo yalinishingaza nilipata ujasiri wa kuongea,
“baba kwanini sipaswi kuudhuria mazishi ya mama yangu, ina maanisha mama amefariki na siwezi kuona sura yake ya mwisho kwanini sikupewa taarifa mapema baba kwanini lakini?”
Niliongea kwa sauti kubwa ya kilio,
“Hapana mwanangu hatuna jinsi mama yako hawezi kuendelea kukaa tena naomba unielewe endelea kusoma utakuja wakati wa arobaini yake” aliongea baba.
Niliangua kilio kikubwa hatukuweza kusikilizana tena, baba alikata simu.
Nililia, niliona duniani niko peke yangu nilihisi nimetengwa mbali na dunia sikuwa sawa na viumbe wengine roho iliniuma kuliko kawaida sikuwahi kuhisi maumivu makali moyoni kama nilivyoyahisi kwa wakati huo, nililia sana sikuwa na nguvu ya kunyanyuka.
Mwalimu alinionea huruma alininyanyua akanikokota kuelekea bwenini wakati tuko njiani tulipishana na Martin , Martin alikuwa amekonda sana nilimtazama huku nikilia kwa sauti mwalimu aliniongoza mpaka bwenini akaanza kunifariji kwa maneno mazuri, hii ni njia ya kila mmoja wetu kila mtu atapita kila nafsi itaonja mauti jipe moyo Cathe. Nililia sikuwa namsikiliza alikuwa anaongea nini wala sikutamani kusikia alichokuwa akiongea, kwanini baba asinipe taarifa na kuhudhuria msiba mapema kwanini? Nililia huku nikiwaza hayo yote, nilishindwa kupata majibu.
Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilikuja kushituka ilikuwa ni asubuhi siku ya pili roho iliniuma sana, sikuweza kunyanyuka kuelekea darasani nilibaki nimejilaza tu chumbani.
Nikiwa nimezama kwenye fikra huku nikidondokwa na machozi nilihisi mlango wa chumba chetu umefunguliwa nilijuwa ni Candy, cha kushangaza alikuwa ni Martin, nilipomuona machozi mfululizo yalianza kunidondoka, Martin alijongea kitandani nilipokuwa nimelala akanikumbatia,
“Cathe pole”, alioongea kwa upole.
Nilishindwa kuongea
“pole sana yote ni mambo ya kidunia usijali mungu yupo pamoja nawe” aliendelea kunifariji na kunitia moyo,
Nilijitahidi kurudia katika hali yangu ya kawaida ingawa kwa kiasi fulani nilishindwa baada ya muda alitoka kwa sababu aliingia kwa makosa.
Dunia sasa imeniacha peke yangu mama ambaye nilikuwa nikimtegemea na nikimpenda kuliko watu wote ndio huyo ameniacha nililia sana kwa kweli. Baada ya muda kupita nilirejea katika hali yangu ya kawaida lakini haikuwa kawaida kama kawaida nilikonda nilipungua mara zote nilikuwa mwenye huzuni machozi yakinidodoka, sikupennda kujiunga na watu katika makundi nilipenda kukaa peke yangu. Sikupenda kula chakula nilikula pale tu niliposikia njaa.
Usiku iliniwia vigumu sana kupata usingizi kila nilipolala sura ya mama yangu ilinijia, sikuwa na wakati hata wa wakusoma kila niliposoma machozi yalinibubujika nilipenda kusoma ili nitimize ndoto zangu.
Kutimia kwa ndoto zangu ilikuwa ni furaha ya mama yangu, sasa mama yangu hayupo ninasoma kwa ajili ya nani?
Nilikata tamaa ya kusoma nilikata tamaa ya kuishi.
Walimu walijitahidi sana kunifariji, na kunipa nasaha mbalimbali. Haikusaidia kitu.
Martin naye hakuacha kunihusia kwamba hayo yote ni mambo ya dunia yapasa kujipa moyo.
Ilikuwa ni siku ya jumanne asubuhi, tukiwa kwenye mkusanyiko jina langu liliitwa mbele kiukweli saikolojia yangu haikuwa vizuri kabisa nilijuwa tu tayari nina kesi nyingine hapo shuleni nilikuwa tayari kwa kila kitu, hata kama nikiambiwa kwamba leo nimefukuzwa shule ningepokea kwa kawaida kabisa, nilishachoshwa na mambo yaliyokuwa yakinikuta, nilijongea mbele kiunyonge zaidi. Shule nzima walinyamaza kimya, wakitegemea kusikia ni tukio gani tena nimelifanya. Maana nilishazoelekea kuwa mtu wa matukio hapo shuleni. Nilipanda mpaka mbele. Mwalimu alichomoa barua na kunikabidhi nilibaki nimeshangaa imetoaka wapi, nilijiuliza.
Nilirudi huku nikiwa na mshawasha wa kuifungua barua ili nione ni nini kilichoandikwa ndani yake nilifika darasani hata sikukaa sana nilinyenyuka na kuelekea bwenini nikaifungua barua hiyo na kuanza kuisoma.
Nilichokutana nacho kilichoandikwa kwenye hiyo arua kilinifanya nilie upya.
Kiliibua huzuni na simanzi ndani ya moyo wangu.
Kiliuua kabisa tumaini langu na furaha yangu.
Matumaini yangu ya kuwa na furaha yalikatizwa na barua ile, ilikuwa ni barua kutoka kwa mama yangu.
“Kwako mwanagu mpendwa na wa pekee naandika barua hii kwa huzuni nyingi nikijua kuwa sitaweza kukuona tena wewe ni kipenzi cha moyo wangu Cathe mama yako anakupenda sana na siku zote nilitamani ufike pale ambapo ulitaka kufikia, najua unajua tumaini langu kwako kuwa natamani utimize ndoto zako lakini, moyo wangu unaumia sana kujuwa kwamba utatimiza ndoto zako ingawa sitoshuhudia naomba ujipe moyo mama yako natangulia na wewe utafata, mpendwa wangu ujaposoma barua hii sitaki ujenge chuki yoyote na mtu yoyote bali uzidishe upendo, mwanangu kilichokupeleka shuleni ndicho unachotakiwa kukizingatia usiangaike na vitu ambavyo siyo lengo lako wala la kwetu sisi kama wazazi wako kukufikisha shuleni, soma sana mwanangu. Wala usisahau kumkumbuka mungu wako kwa maana ndiye atakuwa kiongozi wa maisha yako mwanangu napenda ujue hiki kitu nitakuwa na furaha sana endapo barua hii itakufikia na kuifungua na kuisoma.
Mwanangu Cathe, nilipokuzaa wewe ukiwa na miezi minne tu nilikuwa na ujauzito mwingine baba yako alinishawishi kuutoa ingawa nilikataa aliniambia kwamba sitakupa muda wa wewe kukua vizuri kama nitakuwa na ujauzito mwingine baaada ya ushawishi wa muda mrefu nilikubali kuitoa hiyo mimba ambayo ilikuwa ni ya mdogo wako, nilifanikiwa kuitoa lakini ilitoka vibaya, iliharabu mfuko wangu wa uzazi.
Baada ya muda, nilianza kusikia maumivu ya tumbo yasiyoisha nilipoenda hospitali niliambiwa mfuko wangu wa uzazi umeharibika haufai tena. Hivyo napaswa kutolewa. Hapo ndipo nilopohakikishiwa kuwa mgumba maisha yangu yote, baba yako alibadilika sana kila mara tulikuwa tukizozana kwasababu alikuwa anataka kupata mtoto mwingine aliniambia endapo sitaweza kumpatia mtoto mwingine basi ataenda kuzaa nje ya ndoa, niliumia sana kwa maana sio mimi niliyetaka kutoa ujauzito bali ni yeye aliyeniamasisha sikuwa na jinsi nilivumilia hayo yote huku nikiweka juhudi kuomba mwanangu.
Cathe tukio lililotokea shuleni kwako ingawa sina imani kama ni kweli umefanya hivyo lilimkasirisha sana baba yako, mara zote alijuwa kwamba mimi ni mtu wako wa karibu sana kuliko yeye, kwa maana hiyo kosa lolote wewe ambalo ukifanya lawama zote nilibeba mimi, nashukuru katika kipindi chote katika uhai wangu nilibeba majukumu yangu sawasawa na hata sasa naelekea mwisho wa maisha yangu nimekupigania wewe kama mtoto wangu na naamini utafika sehemu ambayo unatamani kufika baba yako alinipiga sana kwa kosa lako ulilolifanya shuleni.
Na baada ya hapo aliondoka hadi ninapoandika waraka huu sijui yuko wapi, nahisi maumivu makali mwilini na hakuna mtu wa kunisaidia. Sitamani tena kuendelea kuishi katika mateso kiasi hiki acha tu nife mwanangu. Nilimwomba tu kijana wa hapo jirani anisaidie kukutumia hii barua ili mwanangu ujue baba yako ni mtu wa aina gani. Sio kwamba umchukie bali umpende na kuishi naye vizuri katika tabia aliyokuwa nayo baba yako ni mkatili sana, mwanangu naona nafsi yangu haina mda mrefu sana nitakufa wakati wowote ule.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kutimiza ndoto zako usiache kusomea kile unachokipenda mkumbuke sana mungu usiache kusali kila unapoingiakatika tatizo lolote, mimi ni mama yako mpendwa nakutakia maisha mema binti yangu”.
Nilijikuta nimekaa sakafuni bila kujua.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>>
*Mwendelezo njoo inbox*
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: