Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA NANE.
Niliishiwa nguvu mwili mzima ulikuwa ukitetemeka nikiwaza Martin anataka kuniambia nini? Akili yangu hakutulia niliwaza sana nimewezaje leo kumwambia mwanaume kuwa nakupenda kitu ambacho sikuwahi kufikiria katika maisha yangu. Akili yangu haikuwa sawa kabisa,
“Cathe” sauti yake ilinitoa kwenye wimbi la mawazo,
niliongea kwa kitetemeshi, “nakusikia martin”.
“Mawazo yetu yanafanana”, nilibaki namshangaa nisijue akimaanisha nini
“una maana gani Martin?” nilimuuliza.
Alivuta pumzi ndefu na kisha kuishusha
“ulichokuwa unakiwaza ndicho kilichokuwa akilini mwangu” alisema.
Sentensi yake fupi ilitosha kuufanya moyo wangu ujae na furaha sana niliruka kwa furaha na kumkumbatia. Kila mtu akiwa na furaha moyoni mwake na huo ndio mwanzo wa mahusiano kati yangu na Martin, tulipendana sana huku tukishirikiana katika mambo mbalimbali pale shuleni, alikuwa mshauri wangu mkubwa na pia tulishirikiana kimasomo ili kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri katika mitihani yetu. Ukizingatia wakati huo tulikuwa tumebakiza wiki chache tu kufanya mitihani yetu ya muhula wa pili.
Candy mahusiano yetu yalimuumiza sana, Candy na kundi lake, alizidi kunipa adhabu mbalimbali lakini sikujali kwakuwa kwa wakati huo hakuwa akinionea tena.
Mahusiano yetu yalizidi kustawi ingawa ndani ya nafsi yangu sikuwa na amani, kisasi juu ya baba kilinisumbua sana mara zote nilitamani kumlipizia kisasi. Niliwaza sana nitakapoporudi nyumbani lazima nilipize kisasi kwa baba haiwezekani kuniulia mama yangu,
“haiwezekani baba lazima ulipe damu ya mama yangu”, niliwaza.
Martin alikuwa akinishauri sana kuhusu swala la kulipiza kisasi,
“achana nayo yamesha pita hata ukilipiza kisasi mama yako hatoweza kurudi mwache msamehe baba” alikuwa akinishauri.
Nilifanya kama namwelewa ingawa nafsi yangu ilikataa kabisa kuendana na mawazo yake lazima nikalipize kisasi nilisema.
Tulifanikiwa kufanya mitihani yetu ya mwisho na kufaulu kwa ufaulu mzuri kabisa.
Tulirudi nyumbani mimi na Martin tulikuwa tukitokea Dar es salaam. Candy alikuwa akitokea Arusha hivyo naye alielekea kwao ingawa kwa masikitiko sana alikuwa akiumia sana kumpoteza Martin.
Wakati wa likizo tulitumia muda mwingi sana kuwa pamoja mara nyingi tuliongozana sehemu mbalimbali za burudani. Nilipata amani na furaha sana moyoni mwangu kuwa pembeni ya Martin wazo langu la kulipiza kisasi bado nilikuwa nalo.
Mara nyingi baba hakuwepo nyumbani nilikuwa nabaki peke yangu, toka nimerudi likizo baba alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani na akiwahi sana kuondoka alikuwa marachche sana nilikutana na baba yangu na hakuwa katika hali ya kawaida.
Kila mara nilikuwa nikimshangaa jinsi alivyo baba alivyobadilika sana. Nilipanga lazima tu nilipize kisasi kwa namna yoyote ile ingawa hadi wakati huo sikuwa naijua ni kwa namna gani nitalipiza kisasi siwezi kumuua baba yangu nilisema.
Muda mwingi niliutumia kuwa na Martin na wakati huo niliweza kupoteza usichana wangu. Martin aliniingiza katika dunia ya mapenzi sikujali kuhusu hilo ingawa mama yangu alikuwa akinihusia sana kuhusu kujitunza sikuona umuhimu wowote kwasababu mama yangu mwenyewe hakuwepo duniani niliona ni kawaida.
Mapenzi kati yetu yalizidi kuongezeka hata hivyo akili yangu ilikuwa ikifikiria vitu vingine kabisa. Muda ulienda na wakati wa kurudi shuleni ulikaribia.
Nilichelea kuona kwamba sijafanya kisasi kwa baba yangu niliamua kwa muda huo mchache lazima niwe nimefanya kitu, kama kawaida yake baba alichelewa sana kurudi nyumbani na aliwahi kuondoka asubuhi.
Alipotoka tu nilinyatia hadi chumbani kwake, nilipoingia nilishangaa kukuta baba hafungi chumba chake siku hizi. Nilikuwa naogopa sana kuingia chumbani kwa baba yangu enzi za uwepo wa mama. Mara zote sikuruhusiwa kuingia bila ruhusa maalumu niliingia mara chache sana. Nilikuwa nikitetemeka mno kuingia chumbani kwa baba. Mazingira niliyokutana nayo pale chumbani yalinishtua sana, palikuwa ni pachafu kana kwamba haishi mtu.
“Nahisi toka mama amefariki hiki chumba hakijawahi kufanyiwa usafi”, niliwaza.
Nilipofika katikati ya chumba nikasimama,
“nafanya nini humu sasa?” Nikajiuliza,
“humu ndio nimekuja kulipiza kisasi kwa baba yangu?” Nilibaki nimesimama nisijue nini cha kufanya. Ghafla nikaijiwa na wazo la ghafla nikaenda kwenye droo ya baba yangu na kuanza kufungua fungua droo moja baada ya nyingine.
Nilikuwa nafungua tu nisijue nini natafuta. Katika kupekua pekua nilikutana na vyeti vya hospitali vingi, moyo wangu ulinishawishi kuviangalia,
“aaaah! mimi si nimekuja kwaajili ya kulipiza kisasi? Hivi vyeti vya nini? Mimi naachana navyo bwana” nilijiwazia, upande wa pili nafsi yangu iliniambia nivifuatilie. Nikaviweka kitandani kisha nikaanza kukagua kimoja baada ya kingine. Moyo wangu ulizimia cheti cha kwanza kukiona kilikuwa ni cha marehemu mama yangu. Ilikuwa ni ripoti ya daktari kuhusiana na kifo chake ambayo sikuwa na shaka kuwa haikusomwa siku ya msiba wake. Mama yangu alikufa kwa stroke (kiharusi). Na hii imetokana na kupasuka kwa mirija yake ya damu kutokana na kipigo kikali alichokipokea kutoka kwa baba. Hadi kufikia mwisho ripoti ya daktari machozi yalikuwa yakinitoka huku mwili mzima ukitetemeka. Nilijawa na hasira mara mbili yake nilitamani baba awepo karibu yangu nichukue hata kisu nimchome aondoke mbele ya macho yangu sikumpenda kabisa. Nikasimama ili niondoke nikagundua kuna vyeti vingine ambavyo vimebakia hapo chini nilivichukua huku mikono ikitetemeka na kuanza kuvisoma,
“mungu wangu!” Nilisema.
Vilikuwa ni vyeti vya baba yangu kutoka katika hospital maarufu sana hapa mjini. Vilikuwa vikionesha kwamba baba yangu yupo katika hatua za mwanzo za kansa ya ini na hii imetokana na ukweli kwamba baba yangu alikuwa mlevi kupindukia hasa mara baada ya kifo cha mama.
Nililia sana ni sawa nilikuwa nikimchukia baba yangu lakini kujua kwamba baba yangu ana kansa ya ini na asingekuwa na maisha marefu iliniuma sana wazo la kisasi lilipotea kabisa katika moyo wangu
“kwanini mimi? Kwa nini matatizo hayaniishi?” nililia mno.
“Baba ukiondoka nitabaki na nani sasa?”
Nilitoka chumbani kwa baba nikawa nimenyong’eya nilijutia kiherehere change kutaka kulipiza kisasi bora nisingejua nililia siku nzima sikutaka hata kuongea na Martin na mtu mwingine yoyote nilijifungia chumbani siku nzima.
Nilikuja kusituka ni asubuhi yake Martin alikuwa amekuja nyumbani alikuta mlango uko wazi akaingia moja kwa moja hadi chumbani kwangu,
“Cathe kwanini hupokei simu yangu wala hujibu meseji zangu?” Aliniuliza,
“Hapana hamna kitu” nilisema
“Kuna tatizo? kama lipo naomba niambie” aliniuliza.
“Hapana hakuna tatizo lolote”
Sikupenda ajue.
Tulishinda wote hadi ilipofika jioni. Jioni baba aliporejea alitukuta na Martin mara nyingi alizoea kutukuta na Martin nyumbani, alisalimia pasipo uchangamfu na kupitiliza chumbani kwake. Sikuweza kupata muda wa kuongea na baba muda mwingi alikuwa akinikwepa.
Wakati wa kurudi shuleni ulipofika nilirudi shuleni kinyonge sana Marti alikuwa akiniuliza mara kwa mara kwa nini umepoteza uchangamfu wako Cathe aliniuliza.
“Hapana usijali” ilisema
Ingawa hata ndani ya nafsi sikuona kama nipi kawaida nilihisi nina kitu ndani yangu sikujua ni kitu gani.
Nilirudi shuleni nikiwa na unyonge sana
Safari hii Candy alikuwa amenipania sana sikuogopa kitu.
Martin alizidi kunipenda na tulizidi kudhijirisha uhusiano wetu haikuwa siri tene pale shuleni.
Tatizo na lenye kuumiza kuliko yote lilijitokeza.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: