RIWAYA: HIGH SCHOOL SEHEMU YA TISA. Chuki ya Candy ilizidi juu yangu pamoja na faraja niliyokuwa naipata kutoka kwa wanafunzi na kwa baadhi ya marafiki zangu, Martin akiwa mmoja wapo haikutosha kunifanya nisiogope, niliingiwa na woga sana kwa sababu alikuwa akinitisha mara kwa mara nilipokea meseji za vitisho kutoka kwake mara nyingi akiniambia kwamba atanifanyia kitu kibaya, nilianza kuogopa sana. Martin aliweza kunitia moyo na mara nyingi alikuwa akinisisitizia kuwa makini, nilijaribu kujiweka busy na masomo na kumtoa Candy katika akili yangu, sikutaka kurudia makosa niliyoyafanya hapo kabla, nilitamani kufanya vizuri katika mitihani yangu ya mwisho hivyo sikupaswa kurudi nyuma tena. Siku moja niliitwa ofisini kwa mwalimu Maloya niliogopa sana kwenda ingawa sikuwa na jinsi kila nilipokuwa nikipiga hatua moyo wangu ulikuwa mzito nafsi ilinishauri sana nisiende ingawa upande mwingine uliniambie niende laiti ningejua nisingeusikiliza upande huu. Nilipiga hatua zangu za kinyonge hadi ofisini kwa Maloya nilipoingia hakunikaribisha kama ilivyokuwa siku zote, niliingia na kubaki nimesimama, “shikamoo mwalimu” nilimsalimia hakunijibu “nimeitikia wito” nilimwambia bila kujali jinsi ambavyo alikuwa amechukia, alisimama “karibu binti mrembo, mrembo ambaye unajisikia unajiona mzuri kuliko wote hapa shuleni” aliongea kwa dharau, Unamaanisha nini mwalimu “Hivi we unafikiri ni mzuri sana kiasi cha kinikatalia mimi?, wasichana wenzio wazuri wazuri kabisa kama wakina Candy hawaringi kama unavyoringa wewe, wewe ni nani hasa?” Nilishindwa kumwelewa. Akili ilianza kuniambia kuwa tukio baya litatokea, miguu iliniwia mizito sana kuondoka , nilitamani kukimbia lakini nguvu zilinishia. “Wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kunishinda mimi alaaa!” Alisema na kusogea pale nilipokuwa, nilisimama kujizatiti kwa ajili ya kile kilichokuwa mbele yangu. Alikuja hadi mbele yangu akasonya kisha akinipita alielekea mlangoni nilijua alikuwa akienda kuchukua fimbo kwa ajili ya kuniadhibu . Adhabu nilishazizoea nilikuw tayari aniadhibu, maloya alifika mlangoni na kujifanya kama anachukua fimbo akafunga mlango na kisha akanigeukia “Leo utaongea na mimi” akanisogelea, “Unanikubali hunikubali? aliongea kwa ghadhabu, “Hapana mwalimu siko tayari” Niliongea kwa sauti ya chini sana. “Utanipa hunipi nilishituka” “Hapana mwalimu siwezi kukupa” “Siwezi kukupa unachotaka naomba niruhusu niondoke” “Huendi popote leo Cathe ama zako ama zangu” Alinishika kwa nguvu na kufanya kile ambacho alitarajia kufanya. Nilihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wangu. Sikutegemea mtu ambaye nilikuwa nikumheshimu kama mwalimu na mlezi wangu katika mazingira kama haya angenitendea kitendo hicho. Maloya alinibaka bila huruma nililia sana, alinizidi nguvu nilishindwa kujiokoa nilijaribu kupiga kelele aliniziba mdomo. Baada ya kutekeleza unyama huo alivaa nguo zake “Vaa uende bwana, unaringa nilijua unajitunza kumbe na wewe hamna kitu ondoka” aliniongea kwa dharau, Moyoni mwangu niliumia sana, “Unajifanya mlokole kumbe huna lolote wajanja washa kuchezea wewe toka bwana” aliongea. Nilivaa nguo zangu kiunyonge sana na kupiga hatua za kinyonge kuelekea mlangoni “Cathe” aliniita, “Ole wako unyanyue mdomo kumwambia mtu yoyote nitakuua” alisema. Niliondoka kinyonge kuelekea bwenini nilifunga mlango na kuanza kulia Nililia sana “kwanini matukio haya yote yananitokea mimi tu ina maana hamna mtu mwingine wa kushea na mimi shida hizi kwa nini mimi peke yangu” Nililia sana “kwanini haya yote” nililia, Nililia mpaka nilipopitiwa na usingizi nilikuja kushtuka ilikuwa jioni sana. Sikusikia hamu ya kula wala kutoka kwenda sehemu yoyote . Nilibaki hapo kitandani hadi siku ya pili yake. Sikujisikia kuingia darasani, nilobaki tu nimelala sikuwa na hamu ya kula nilikula tu pale nilipohisi njaa, hali hiyo iliendelea kwa wiki nzima. Martin alikuwa akinitafta kila kona huku walimu wakiulizia ni wapi nilipo. Nikiwa bwenini niliwaza haya yote yatakwisha lini ndani ya nafsi yangu niligundua Ni lazima niyachukulie kama sehemu ya maisha yangu. Lazima niwe na amani sasa. Kujua kwamba nimezaliwa ili niteseke, nilizaliwa ili nipate uchungu, kamwe haikuniumiza katika maisha yangu. Nilijitia moyo sana kwamba hayo yote ni maisha yangu ambayo nimeletwa nije niishi. Hakika nilipata faraja kubwa sana na kwa wakati huo niliapa sitolia tena, kwa sababu hayo ni maisha yangu Mungu amenileta ili niyaishi. Nilitoka bwenini na kisha kuelekea nyuma ya shule Martin aliniona na kunifuata, alikuja Cathe kwanini huingii darasani wiki nzima , una nini? Una unaumwa? Kwanini uko hivyo Cathe kwanini lakini? Aliuliza maswali mfululizo ambayo nilishindwa kujibu. “Aaah Martin uwe na amani niko sawa kabisa” “Nakujua vizuri kama una tatizo ni bora uniambie ili nijue ni nini naweza kukusaidia.” Sikutaka kumwambia sikutaka ajue, ningewezaje kwanza kumwambia. Hapana hakuna kitu nilihisi machozi yanaanza kunitoka nilinyanyuka pole pole na kumwacha Martin peke yake pale. Niliondoka na kuelekea bwenini jioni ya siku hiyo niliamua kuingia darasani. Nikiwa na furaha kwa kujua kwamba matatizo ni sehemu ya maisha yangu nilingia darasani kwa bashasha zote. Nilikutana na Martin tukasalimiana kwa uchangamfu tukaketi, “Nilikumis sana Cathe, ingawa hutaki kuniambia tatizo lilikuwa ni nini” nilicheka, “Martin sina tatizo lolote uwezi kuniamini mimi mpenzi wako” alitabasamu. “Nakuamini mke wangu wangu mtarajiwa” alisema, nilicheka, tukacheka kwa pamoja kisha tukaendelea kusoma. Siku hiyo ilipita kana kwamba hakuna kilichotokea, maisha yaliendelea. Watu walihisi uhusiano wangu mimi na Maloya na hiyo ikawa habari mpya shuleni, kwakuwa Maloya alikuwa akihofu kitendo chake alikuwa akiniuliza mara kwa mara nimwambie kuhusu mahali nilipo na maendeleo yangu. Candy alichukia sana hivyo nilipokea ujumbe wa vitisho nilipoamka kitandani kwangu “We Malaya naona sasa unataka kuniingilia katika anga zisizofaa, nakuhakikishia ama zangu ama zako hii wiki haitopita lazima nikufanyie kitu cha kihistoria.” Yalikuwa ni maneno mafupi na mazito, niliogopa sana “huyu anataka kunifanyia nini?” Niliishi kwa uwoga mno nilipoteza furaha tangu asubuhi ya siku hiyo, ilikuwa ni jumatatu, niliingia darasani kiunyonge, Martin aliweza kugundua kuwa sipo sawa, “Cathe uniamini, umuamini mme wako mtarajiwa?” Aliniambia “namuamini sana” niliongea ingawa sio kiuchangamfu. “Kwanini hutaki kuniambia tatizo linalokusibu?” Nilijitahidi kuonesha kwamba niko kawaida ingawa najuwa kuwa nilishindwa “Martin niko kawaida” niliongea huku nikitazama pembeni, “Hauko kawaida” Niliamua kunyanyuka na kuondoka ili kumkwepa “Unaenda wapi?” “Aaah” nilishikwa na kigugumizi. “Naenda toilet mara moja” Aliachia tabasamu na kisha akaniambia nenda. Niliondoka na kuelekea chooni, vyoo vilivyokuwa bwenini kwetu, niliingia kule nikabaki nimesimama sikuwa najua ni nini nifanye. “Nimwabie nini Marti ili aelewe sitaki kukosana naye wala sitaki kumkosesha amani” niliwaza. “Nilikwambia leo ni ama zangu ama zako” sauti ya candy ilipenya kwenye masikio yangu. <<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA

at 11:06 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top