Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA MBILI.
Nilishituka na kujikuta nimelala katika zahanati ya shule, dripu zikichuruzisha maji mwilini mwangu, nilihisi maumivu makali sana ya kichwa na macho pia yaliniwia mazito, uchovu ulinitawala, na mwili mzima ulikuwa ukiuma, sikufahamu ni kitu gani kimetokea hata nikafika hapo.
Kumbukumbu zangu ziliniwia vigumu sana kunirejea nilibaki nikiwa nimelala hapo kitandani sikuweza kujiinua, nilipogeuka upande wa pili nilikutana na nesi akiwa anaongea na wanafunzi wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.
Nilipata shida sana kuwatambua kuwa alikuwa ni Martin na Martha.
Baada ya maongezi mafupi Martin aliyekuwa amebeba hotpot na Martha waliongozana kuja kitandani kwangu walipofika walinipa pole na kisha kukaa kwenye kitanda cha pembeni.
Martin alinishika kichwani akiushusha mkono wake usoni mwangu kisha akaniambia “pole Cathe” aliongea kwa sauti yake nzuri ya kiume.
“Asante Martin”
“Nesi amesema unaendelea vizuri unaweza kuruhusiwa kuanzia leo”
“kwani nimelazwa hapa tokea lini?” niliuliza.
“Tokea juzi huko hapa”
“Ninaumwa nini?!” Niliuliza kwa mshangao,
“Ulipatwa tu na mshituko kidogo baada ya kutoka polisi”
Alipotaja polisi kumbukumu zilianza kunirejea,
“Mungu wangu”
“Candy anaendeleaje?” Niliuliza kwa kiherehere ,
“Candy anaendelea vizuri hali yake imetengemaa sasa”
“Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha”
Niliwaza “Candy akipona nimekufa, Candy akipona tu ndio mwisho wa maisha yangu”
“Mbona umeshituka sana?”
“Hapana” niliongea kwa kigugumizi,
“Namwombea Candy apone” nilisema,
“Kila mtu anamwombea kwa kweli hatujui amepatwa na nini, kupona kwake ndipo kutakapojibu maswali yetu yote”, akili ilizidi kwenda kasi,
“nifanye nini mimi?”, nilijiuliza.
“Ndio”
Mwishowe nilijibu, huku nikionesha kunyong’onyea.
Martin alifungua hptpot na kuanza kunilisha chakula, kilikuwa ni chakula kizuri sana tofauti na ambacho tunakula hapo shuleni.
Martha aliniangalia kwa huruma sana,
“pole wifi” alisema.
Niligeuka na kumwangalia Martha,
“Asante” nilijibu.
“Cathe” Martin aliniita,
“Bee” niliitika.
“Sikuwahi kukwambia kwamba Martha ni mdogo wangu” aliniuliza,
“Whaat?”
“Ndio, Martha ni mtoto wa baba yangu mkubwa”
“Tangu nilipopoteza ufahamu ni kitu cha kwanza kilichonipa faraja,
“Nafurahi sana kukufahamu Martha”
“Usijali”
Nilikula nikiwa katikati ya watu hao walionionesha upendo, nilijisikia amani sana kuwa katikati yao.
Baada ya muda alikuja nesi,
“Martha inabidi ukakae na Cathe ili umwangalie, tunamruhusu leo kwa sababu hali yake inaendelea vizuri, tutakupa dawa za kutumia ukisikia maumivu yoyote urudi hapa, Sawa Cathe” nesi alisema kwa sauti yake ya upole.
“sawa asante” nilishukuru kwa sababu sikupenda kuendelea kuwepo hapo.
Walinisaidia kukusanya vitu vyangu na kisha nikarejea bwenini.
Martin alinibusu mdomoni kisha akaniacha nikiwa na Martha.
“Martha, naomba uniangalizie mke wangu” alisema Martin.
Niliachia tabasamu, nilipenda alivyoniita.
“Mchumba tutaonana baadae” alisema kisha akatoka.
Nilitamani aendelee kuwepo karibu yangu ingawa ilikuwa kinyume cha sheria za shule kuwepo katika mabweni ya wasichana.
Aliniacha na Martha
Martha alikuwa akinitunza vizuri sana hakika nilifurahi.
Baada ya muda kupita hali yangu iliweza kutengemaa kabisa na nikaweza kuingia darasani, nilijitahidi kujiamini mbele ya kila mtu ili nisihisiwe kwa tukio lolote. Nilijitahidi sana kuomba mungu aniepushe na tatizo hili
“ee mungu ingawa sio vizuri lakini naomba uichukue roho ya Candy, kumwacha Candy hai ni kuniingiza mimi mkwenye matatizo, mbona umesha nitesa sana hebu saa hizi tu basi unionee huruma na mimi, na mimi niishi kwa amani, Mungu naomba usikie maombi yangu”
Niliomba maombi hayo huku nikiwa sina imani ya kujibiwa.
Nilikata tamaa kabisa.
“Candy usipokufa nitakufa mimi kwa namna yoyote ile”, nilisema.
Niliendelea kusoma kwa bidii huku nikisali.
Kila siku mwalimu alipoingia darasani hasa mwalimu Maloya alitusisitiza tuendelee kumwombea Candy kwasababu hali yake ilikuwa ikitengemaa.
Maneno hayo yalizidi kunikera, kila mara alipotangaza kuhusu hali ya Candy moyo wangu ulikosa amani kabisa.
Ilikuwa ni alfajiri siku ya jumamosi, ni siku ambayo huwa hatuamshwi mapema tunaamka pale utakapojisikia wewe kwa maana shuleni kwetu tulikuwa hatufanyi usafi hiyo siku nilitaka kulala sana.
Ilipofika saa moja kasoro kengele iligongwa, nilikerekwa sana kuamshwa asubuhi siku hiyo nilitamani kuendelea kulala, wakati kengele ikizidi kugongwa nilivuta shuka na kujifunika.
“Hawa vipi bwana ahaaa, fyuuu”, nikasonya
Martha aliniamsha “Cathe amka ni kengele ya tahadhari huwezi kujua pengine kuna tukio baya amka usikute mabweni yanaungua amka haraka”,
nilishuka haraka na kutoka nje huku nikiwa nimevaa night dress.
Martha alicheka “wewe hebu rudi uvae nguo wewe vipi?”, aliongea kwa utani.
Moyo wangu ulikuwa hauna amani kabisa,
niliwaza “sijui polisi wamekuja kunifata tena, mungu wangu kama hali ya Candy ikitengemaa inamaanisha anaweza kuongea na angewasimulia polisi kila kitu, kwa maana mara zote walikuwa wakimsubiria apate unafuu ili aelezee tukio zima, ameelezea na sasa hivi nakuja kufatwa na polisi, ee mungu wa majeshi sijui nikimbie” niliwaza.
“Mi siendi” nilimwambia Martha,
“amna usiogope hamna tukio la ajabu”
“Hapana moyo wangu unasita kabisa kwenda”
“Twende tu Cathe hakuna jinsi”
“Mi nabaki naomba uende utaniambia”
“Unaogopa nini?” Aliingiwa na ghadhabu,
niliogopa anaweza kunishitukia huyu,
“Sawa twende, Ila nilikuwa na woga kweli kwenda huko”
“Hamna usiogope wifi yangu we twende tu”
Tuliongozana hadi kufika mstarini, tulikuwa watu wa mwisho mwisho kufika kwa maana watu wengi walikuwa washafika.
Walimu wote walikuwa katika eneo hilo, niliingiwa na uwoga sikuwa najiamini hata kidogo mwili mzima ulikuwa ukitetemeka,
“unatetemeka nini Cathe” sauti ya Martha ilinishitua.
“Hapana, ila nahisi kuna kitu hakipo sawa, sijui ni nini” niliongea.
“usijali kila kitu kitakuwa sawa”
Tulijongea mstarini.
Walimu walisubiri hadi kelele zote ziishe, baada ya wanafunzi kunyamaza kimya na kuonyesha kuwa tayari kwa kusikiliza tulichoitiwa mapema asubuhi hiyo, mwalimu mkuu Mr. Maige alisogea mbele kututangazia kitu ambacho walikusudia kwa asubuhi hiyo.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: