RIWAYA: HIGH SCHOOL SEHEMU YA KUMI NA TATU. Shule nzima ilikuwa kimya kusikiliza ni kitu gani ambacho tungetangaziwa. Baada ya ukimya wa mda mfupi Mr. Maige alisimama mbele ya wanafunzi wote, alikohoa kidogo kurekebisha koo lake na kisha kuanza kusema kwa sauti iliyonyong’onyea, “Hamjambo wanafunzi” “Hatujambo” tuliitikia na kisha ukimya mzito ukafatia. “Poleni kwa masomo natumaini mko salama wote, lakini kuna jambo moja ningependa kuwaambia wanafunzi, shule imepata msiba mzito,tumempoteza mwanafunzi mwenzetu Candy Carry” Vilio vilianza watu walilia, sio wanafunzi peke yake hata walimu pia. Nilishusha pumzi nzito kisha machozi yalianza kunitoka, ingawa mara zote nimekuwa katika maombi nikiomba mungu amuondoe Candy duniani, lakini kifo cha Candy kiliniuma sana. “Uwepo wangu hapa shuleni umesababisha kifo cha Candy, nisamehe Candy, Mungu naomba unisamehe pia”, Mwalimu Maloya alilia sana, Nikama vile hakuwa akijua chochote hadi wakati huo tulipotangaziwa. Alionekana akiwa na huzuni wakati wote, baadhi ya walimu walimfariji Maloya alikuwa akilia kuliko kawaida, wanafunzi wengi walikuwa wakinitupia macho kujua ningezipokeaje taarifa hizo sikupenda jinsi walivyokuwa wakinitazama. Nikajifanya nimezimia. Nilibebwa na kupelekwa hospitalini, nikawekewa drip za maji ingawa kiukweli sikuwa nimezimia sikutaka kuamka wakati huo, nilitaka kufikiria upya kuhusu hilo swala na jinsi maisha ambavyo yangeenda. Nililala hapo siku nzima, huku taratibu za kuuaga mwili wa Candy hapo shuleni zikiendelea kufanyika. Vipindi vilihairishwa kila mtu alikuwa na huzuni sana kuhusu kifo cha Candy. Ulipofika wakati wa jioni hali bado nikiwa nimefumba macho yangu nilihisi mtu akiingia. Nilifumbua jicho kwa mbali ili kuweza kutazama ni nani kwa maana huo haukuwa wakati wa kuona wagonjwa, nilitamani awe Martin ili kunifariji kwa wakati huo. Hakuwa Marti alikuwa Maloya, alipofika nesi aliingia, “bado hajarudiwa na fahamu, anahitaji muda mwingi wa kupumzika akili yake haiko sawa.” “Sawa” Maloya alijibu, “nimekuja tu kumwangalia, nitaondoka muda si mrefu hauna haja ya kuhofu nesi.” “Sawa” nesi aliitikia na kuondoka. Alituacha mimi na Maloya. “Wewe mshenzi ninajua kuwa unahusika na kifo cha Candy, utakapoamka hapo utanieleza. Nitapambana na wewe na kuhakikisha kwamba unapata adhabu stahiki, lazima uhukumiwe kwa kosa la kumuondoa kipenzi changu. Unajua mimi na Candy tumetoka wapi? Wewe kidudu mtu ama zako ama zangu” aliongea kwa hasira kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka. Alinisonya na kisha kuondoka kwa ghadhabu. Nilipata kujua kwamba Maloya amefahamu kila kitu kilichotokea. Moyo uliniuma sana nilijua nimeimaliza kesi kumbe ndio nimeianza. Jela ilikuwa ikiniita. Nilikata tamaa ya kuendelea kuishi. Kitu pekee cha kufanya ni kuondoka tu hapa. “Sijui nitoroke sasa hivi, nikitoroka saa hizi itajulikana kwamba ninahusika kwa namna Fulani, kwanini niondoke.” Mwili wa Candy uliagwa nikiwa hospitali na ulisafirishwa kuelekea Arusha kwa maziko, kila mtu alikuwa na huzuni sana, Maloya akiambatana na wanafunzi wawili akiwemo Naima waliondoka na mwili wa Candy kuelekea Arusha. Ilichukua muda watu kurejea katika hali ya kawaida kisha maisha yaliendelea. Maisha ya shida yalianza hapo shuleni nilikuwa nikipokea vipigo mara kwa mara kutoka kwa Maloya, nilikuwa nikipigwa sana,adhabu za mara kwa mara hazikuniisha. Martin alikuwa akinionea huruma sana, wakati mwingine alikuwa akijitahidi kunisaidia baadhi adhabu nyingine nilizokuwa nikipewa. “Cathe una una nini na maloya? siku moja aliniuliza nilishindwa cha kumjibu, “kwanini akutese hivi umemfanyia nini yeye? Mimi siwezi kuendelea kuvumilia nitamfata” Nilimshika mkono na kumzuia, “Unaenda wapi” niliongea kwa upole. “Namfata Maloya kwanini anakupiga na anakupa adhabu kila siku nimechoka hata mimi siwezi kuendelea kuvumilia namfata.” “Hapana subiri” niliongea. “Siwezi kuendelea kusubiri” nilimzuia. “Martin sitaki kukwambia siri ya Maloya kunichukia, utaumia sana.” Kwa muda mchache aliweza kutuliza hasira aliyokuwa nayo. “Naomba uniambia, sitachukia” “Najua” “hujui kitu Martin” nilimwambia. “Hapana Cathe niambie” “Nitakwambia, ngoja nipate wakati mzuri nitakwambia kila kitu” nilimwambia. Alitulia na kisha kuendelea na mambo yake. Baba Candy, Mr. Carry alikuwa mbogo hakutaka kuamini kwamba Candy alikufa kwa kudondoka mwenyewe bafuni, alitaka uchunguzi ufanyike ili kujua chanzo cha kifo cha Candy. “Lazima nimjue mtu aliye husika na kifo cha mwanangu na nitampoteza” alisema. Mara moja uchunguzi ulianza kufanyika, nijikuta naishiwa nguvu. Kilichoniogopesha zaidi ni kugundua kuwa…………… <<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA

at 11:08 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top