Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA NNE.
Niliogopa sana kujua kuwa nilikuwa nina ujauzito, sikuwa najua kama ujauzito ni wa Maloya au wa Martin.
Nililia sana, nafsi iliniuma mno, kila ninapojitahidi kutoka kwenye tatizo moja linakuja jingine,
“ eee Mungu wangu kwanini umeniacha mimi? Nimezaliwa kwa ajili ya kuteseka tu, ee Mungu wangu, bora basi ungeichukua roho yangu na mimi nipumzike” nilijikuta nikimkufuru Mungu.
Nilishindwa kufanya kitu chochote kile nilishindwa kula vizuri nilishindwa kusoma hata usingizi uliniwia shida sana kupata. Nilianza kukonda tena.
Ujauzito wangu ulikuwa ukinilazimisha kulala usingizi kila wakati, nilikuwa nasinzia sana, nilihisi unaweza ukawa mkubwa kwasababu hata sikuwa najua una miezi mingapi.
Nafsi iliniuma kuona kwamba sitaweza kuendelea na shule. Tumbo langu lilianza kuonekana, nilijitahidi sana kujizuia lisionekane. Nilimkumbuka sana Candy,
“nilikuwa namsema Candy sasa ni zamu yangu” nilijiwazia,
“nitamwambia nini baba yangu siku akigundua kuwa nina ujauzito?” niliwaza.
“Eee Mungu wangu najikabidhi mikononi mwako”, nilimalizia maombi yangu.
Hesabu zangu ziliniambia kuwa ujauzito huo ni wa Maloya, kwasababu yeye ndio aliyekuwa mtu wa mwisho kukutana na mimi kimwili. Hivyo basi ujauzito huu ulikuwa na takribani miezi minne, kwa hesabu zangu ningeweza kujifungua wakati uliokaribia sana na mtihani, aidha mwezi wa nne ambapo tulitegemea kuanza mitihani mwezi wa tano mwanzoni, mitihani ya kumaliza shule. Hivyo basi endapo nisingeitoa hiyo mimba nisingeweza kufanya mtihani.
“Niitoe” niliwaza
“hapana siwezi kuitoa hii mimba, nimuue kiumbe asiye na hatia siwezi kujua mungu amempangia nini kiumbe wake, siwezi kuitoa hii mimba” nilisita sita sita katika mawazo mawili. Nafsi nyingine ikiniambia unahitaji kusoma, zaidi ya sana unamuhitaji Martin endapo Martin akigundua kwamba una ujauzito wa Maloya mapenzi yenu yatakuwa yameishia hapo, potelea mbali lolote na liwe.
Uchunguzi kuhusu kifo cha Candy ulianza mara moja, Mzee Carry baba yake Candy hakutaka masihara katika hilo, alitoka Arusha na kuja Mwanza kusimamia kesi hiyo, alitaka kuona kwamba aliyehusika na kifo cha mwanae anakamatwa na kuhukumiwa.
Kwa kuanzia mwalimu mkuu aliitwa polisi kutoa maelezo, alieleza kila kitu ambacho alikijua kuhusiana na tukio hilo.
Alirejea shuleni kwa upole sana, kisha akagonga kengele na kutuita wanafunzi wote mstarini, tulienda, alituambia mambo yote ambayo yalitokea hako polisi, maneno yake yalinitikisa sana,
“Cathe” alisema, nilitetemeka
“polisi wamesema endapo watakuhitaji watakuita tena ila kwa sasa hawakuhitaji kwasababu ulishatoa maelezo mara ya kwanza” alisema,
“ee mungu wangu naomba unifanyie miujiza” nilisali kimoyomoyo
Baada ya hapo wanafunzi wengi walisogea kunipa pole akiwemo Martin.
Nafsi yangu ilikosa amani kabisa Martin aliligundua hili ingawa akuniuliza.
Mtu wa pili kuitwa kwaajili ya kutoa maelezo ni Maloya. Nafikiri polisi waligundua uhusiano wa karibu kati ya Maloya na marehemu Candy, aliitwa kutoa maelezo, nilijua mwisho wangu umekaribia .
Maloya alianza kujieleza “mimi ni mtu wa karibu sana na Candy na pia ni mwalimu wake”
“ukaribu wenu uko vipi?” aliulizwa,
Maloya alishindwa kutoa maelezo mazuri, mara nyingi alikuwa akijing’atang’ata, nafikiri alikuwa akihofia kuweka wazi uhusiano wake na Candy ukizingatia baba yake na Candy alikuwepo hapo na hakuwa akipenda utani kabisa.
Siku Candy anafariki Maloya alikuwepo, polisi walitaka kumuhoji kwasababu alikuwa akiendelea vizuri. Walipoingia walikutana na Maloya akiwa ameketi kitandani pembeni ya Candy tunataka kumhoji Candy
“sawa na mimi naomba niwepo”
“we kama nani?” polisi waliuliza,
“mimi ni mpenzi wake” alijibu.
“Sawa”
Candy alianza kujieleza, aliongea kwa shida sana kutokana na hali yake ilivyokuwa, alikuwa akijitahidi sana kuongea ingawa alionekana kushindwa, askari aliyekuja kumhoji, alishindwa kuelewa nini cha kufanya aidha ahairishe mahojiano hayo au aendelee kumtia moyo Candy aongee mara simu yake iliita, alinyanyuka na kuelekea nje Candy aliweza kuongea neno moja, alitaja jina langu na kisha kukata roho.
Na hii ndio sababu aliyofanya Maloya ahisi na ajue kwamba ninahusika kwa namna moja au nyingine na kifo cha Candy.
Pamoja na hayo yote maloya alishindwa kujieleza. Baba yake na Candy alikasirika sana,
“wewe ni mwalimu una taaluma ya ualimu nimemleta mwanangu kumfundisha unamfanya mkeo, nitadili na wewe kwanza, aliongea mzee Carry,
“huyu afunguliwe mashitaka ya kutembea na mwanafunzi”, alisema.
Maloya alilia sana alishindwa kujitetea, aliwekwa mahabusu kusubiria kesi yake ianze.
Ripoti ya daktari ilisaidia kummaliza Maloya, Candy alikufa baada ya kugongwa na kitu kizito kichwani, hivyo damu kuvijia katika ubongo, lakini pia alikuwa na ujauzito mkubwa.
Mzee Carry alikasirika sana alisahau kabisa kuhusu swala kifo cha binti yake aliamua moja kwa moja kuhusika na Maloya ambaye moja kwa moja alionekana kuwa ndiye aliyekuwa akihusika na mimba ya Candy, ilikuwa ni afuheni kwangu.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: