Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA TANO.
Nilikuwa na tabia ya kurekodi matukio yote yaliyokuwa yakinitokea kwenye kitabu change cha kumbukumbu, mimba yangu ilizidi kuwa kubwa hata hivyo nilishindwa kumueleza Martin, sikuwa najua wapi nianzie.
Nilipanga kutoroka ili nisije kushitukiwa kwa ujauzito niliokuwa nao, lakini nisingeweza kuondoka bila kumwaga Martin, niliwaza nitamwambiaje?
Nilivuta pumzi ya nguvu na kisha kuishusha,
“nitafute uongo gani? Nitamwambia Martin kuwa hii mimba ni yakwake na hivyo napenda yeye aendelee kusoma hivyo basi naondoka ili asije akatafutwa kwa kosa la kunipa mimba, tutaonana uraiani” nilipanga kumwambia hivyo, hali nikijua kabisa ujauzito huo sio wa kwake.
Nilimwita Martin, baada ya kutoka prepo usiku,
“Martin nataka nikwambie kitu”
“nakusikiliza mke wangu mtarajiwa” niliachia tabasamu hafifu, ingawa niliumizwa na maneno yake nilijua kwamba hakuna ndoa kati yangu mimi na yeye hasa akijua kwamba nina ujauzito ambao sio wa kwake.
“Martin napenda sana tutimize ndoto zetu ingawa kwa upande wangu naona ni vigumu sana kutimiza” niliongea.
“Unamaanisha nini Cathe”
“nakupenda sana Martin, sana zaidi ya unavyofikiria napenda usome, utimize zile ndoto ambazo hata baba yako pia anapenda kukuona siku moja unafikia, upate shahada yako, upate kazi nzuri, uitunze familia yako ya sasa hivi na baadae”, niliongea kwa uchungu sana.
“Naelewa, naelewa baba yangu anatamani sana nifike sehemu ambayo natamani kufika na ndio maana kila mara nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii”
Maneno yake yalinichoma sana.
“Martin nina ujauzito” sikutaka kusema ni wa nani.
Nafsi yangu iliniwia vigumu sana kumdanganya, hakika alishituka,
“Cathe una uhakika?” aliniuliza kwa sauti ya utulivu na upole,
“ndio” nilisema, alinitazama kisha akashusha sura yake kwa huzuni, alibaki amejiinamia tu pale.
“Nimeamua kuacha shule ili nikupe nafasi wewe uendelee kusoma”, nilisema
Alinyanyua uso wake na kunitazama, tayari uso wake ulishakuwa umelowa machozi, moyo uliumia sana, alishindwa kuongea neno lolote.
“Martin usijali kuhusu mimi, nakupa nafasi hii ya kusoma, usome kwa ajili yako na usome kwa ajili yangu, naenda kuanza kumtunza mtoto” niliongea.
Alinivutia kifuani kwake akanikumbatia,
“nitakapo ondoka naomba usome kwa bidii zote sahau kama nilishawahi kuwepo hapa, Soma sana, Sali sana, kula sana, uwe na nidhamu, tunza mapenzi yangu moyoni mwako” niliongea kwa huzuni huku machozi yakinitiririka.
“Ombi langu la mwisho kwako Martin, naomba unisaidie kuondoka hapa shuleni”, alishindwa kuongea lolote alinikumbatia kwa nguvu huku akilia, nilishukuru Mungu tu kwa hilo sikuwa na jinsi.
Alfajiri na mapema ya siku iliyofuata tulikutana na Martin darasani, alikuwa ameniletea begi lake la madaftari, weka humu nguo zako na kila kitu ambacho unahitaji kuondoka nacho nitatangulia kwenda mjini tutakutana huko.
Tukutane stendi usiondoke na begi lako la nguo ilkiwezekana nikabidhi, nilifanya kama alivyosema, nilimkabidhi begi langu kubwa la nguo nilibeba vitu vyangu vichache nilivyovihifadhi katika begi lake la madaftari, niliomba ruhusa shuleni, kana kwamba naelekea mjini, nikiwa na yunifomu zangu.
Nilipotoka nilienda moja kwa moja dukani kununua nguo ambazo ningezitumia kwa ajili ya kusafiria nilipofika stendi nilikutana na Martin, alikuwa akinisubiria hapo, alionekana mwenye huzuni kuliko siku zote. Alishanikatia tiketi alinikabidhi tiketi yangu muda ulipofika nilipanda kwenye gari kwa ajili ya kurejea nyumbani Dar.
Ulikuwa ni wakati wa huzuni kuliko wote kupata kutokea katika maisha yangu niliachana na Martin siku hiyo, njia nzima nilikuwa nikilia tu.
Nilifika Dar usiku sana, sikuweza kuelekea nyumbani wakati huo hivyo nililala hotelini.
Asubuhi ya siku iliyofuata nilibeba begi langu kuelekea nyumbani, nilitembea kiunyonge sana nilipokaribia kufika nyumbani. Niliwaza naenda kumwambia nini baba na nimerudi kabla shule haijafungwa.
Niliingia nyumbani kwetu, hali niliyoikuta ilinipa afuheni kidogo nyumba haikuwa chafu ilikuwa imetunzwa vizuri. Niliingia ndani nikitetemeka sana. Nilimkuta baba akiwa amekaa sebuleni alishangaa sana kuniona,
“Cathe umerudi mama”,
“ndio”
“karibu tena nyumbani” alisema
“Asante baba”
Nilishangazwa baba hakuwa na maneno mengi.
Nilielekea chumbani kwangu kisha nikalala usingizi mzito. Na kuamka jioni ya siku hiyo nikiwa nimechoka sana.
Baba yangu alikuwa amedhoofu sana, lakini hakuwa tena akinywa pombe wala akivuta sigara, muda mwingi alikuwa akiutumia kuwepo nyumbani akifanya mazoezi, akijitahidi kula vizuri, afya yake haikuwa kama mwanzo.
Nilifurahi kujua kwamba baba sasa amejitambua na ameelewa umuhimu wa afya yake.
Niliendelea kukaa na baba, hakuniuliza hata siku moja kuhusu kurejea kwangu kabla ya muda sikuwa najua baba amepanga nini kuhusu hilo na mimi niliendelea kunyamaza kimya.
Takribani mwezi ulipita.
Asubuhi ya siku hiyo baba alijiandaa mapema sana.
Kisha alikuja chumbani kwangu na akanigongea mlango niliamka na kutoka nje nikiwa na uchovu sana.
“Cathe mimi naelekea kliniki, hatuwezi kwenda wote?” alisema
“Aaah, Baba unaenda kiliniki ya nini?”
“Aaah, Mwanangu nahudhuria kliniki ya kansa kwa ajili ya matatizo ya ini langu” alisema
“Aaah, Ngoja nijiandae basi tuongozane”
“Sawa maana nimeona ujauzito wako unazidi kukua na hujawahi kuhudhuria kliniki hata siku moja.”
Moyo ulinipasuka paaaa…….!!!!!
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
>>>>>>>>>>>>>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: