Home → simulizi
→ HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA SITA.
Sikutegemea kujua kwamba baba anafahamu kuhusu ujauzito niliokuwa nao, uso ulinishuka kwa ashuo, niliinama kwa aibu huku nikiwa nimepwaya, nilishindwa kuongea chochote wala kumtazama baba alikuwa amesimama mbele yangu
“Catherine” baba aliniita.
“Bee” niliitika bila kunyanyua uso wangu.
“Tutakaporudi kutoka hospitali tutaongea, jiandae kwa ajili ya kuelekea hospitali”
Aliongea baba na kisha kuondoka, sikupata hata nafasi ya kumjibu.
Niliingia chumbani kwangu na kuketi kitandani,
“Mungu wangu baba akiniuliza kuhusu ujauzito nimtaje nani?”
“Nitamwambia nini mimi?”
Nilishusha pumzi ndefu.
“Eee Mungu naomba uniongoze katika hili” niliendelea kusema.
Nilijiandaa kwa unyonge nilivaa gauni pana pana ambalo lilificha tumbo langu na kisha tukatoka na baba kwa ajili ya kwenda hospitalini.
Niliingia kwenye gari nikiwa na uoga sana niliketi siti ya nyuma wakati baba akiwa dereva.
Tuliongozana mpaka hospitalini muhimbili, tulianza kwa baba ambapo alihudhuria katika kitengo chake alichotakiwa kwenda na baada ya hapo alinipeleka kliniki.
“Baba wa huyo mtoto wako mtarajiwa yuko wapi?” swali la kwanza kwa nesi.
“Na kwanini umechelewa kuhudhuria?”
Baba alimtazama nesi,
“Amekuja na mimi hapa baba yake” aliongea, nilijisikia aibu sana nilishindwa hata kumtazama nesi usoni, nesi aliishiwa pozi wala neno la kuongea alinihudumia,
“umechelewa sana kuanza kliniki mimba kubwa ya miezi mitano” alisema.
Sikujali.
Nilihudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na maendelea ya mtoto wangu yalikuwa mazuri nilirejea nyumbani.
Tulipofika nyumbani nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwangu, wakati nafungua mlango kuingia chumbani kwangu baba aliniita,
“Catherine njoo tuongee”
mwili mzima ulikuwa ukitetemeka nilishindwa cha kufanya, nilirudi sebuleni kiunyonge nikakaa.
“Mwanangu naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea katika maisha yako, najua kama sio sisi wazazi wako yote yasingekupata.”
Nilishindwa kuelewa namaanisha nini hata hivyo niliogopa kuuliza kwa sababu hapo mimi ndiye niliokuwa na makosa.
“Mwanangu, laiti kama nisingesababisha kifo cha mama yako, mama ako angekuwa anakuhudumia na akikufundisha. Mimi na mama yako tulikuwa na migogoro mingi hapa nyumbani na nafikiri ilikuathiri kwa kiwango kikubwa, kama mtoto wetu ulipaswa upate malezi bora, tukutunze, tukujenge katika hali ya kujiamini ambayo ingekuwezesha wewe kupambana na kila aina ya matukio unayokutana nayo katika maisha yako lakini hatukuweza kuyafanya hayo yote na ndio mana hata sasa uko hapa. Sikushituka sana siku ya kwanza tu uliporudi niligundua kuna tatizo haliko sawa, sikutaka kukuliza kwa sababu najua mimi ndio chanzo cha haya yote, nilikuja kugundua kuwa una ujauzito hata hivyo nilishachelewa nisingeweza kukufanya jambo lolote ningeweza kukupiga, sio kwamba sikukasirika, nilikuwa na hasira sana lakini isingesaidia kitu chochote, ila ukae ulee ujauzito, ujifungue, utapata second chance sawa mwanangu uwe tu na amani.”
Nililia sana.
Baba aliongea maneno mazito kiasi yaliniumiza moyo wangu pia ilikuwa ni ukweli mtupu, nilishusha pumzi ya faraja maisha yaliendelea.
Huko Mwanza kesi dhidi ya Maloya ilizidi kuendeshwa, alikutwa na hatia kutembea na mwanafunzi na kumpa mimba na kisha akahukumiwa jela miaka thelathini.
Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kuwasiliana na Martin tena nilijua kufanya hivyo ni kujiumiza tu, ipo siku angegundua huu ujauzito sio wa kwake na angeniacha, nilikuwa sitaki kuachwa ni bora nimwache mwenyewe.
Niliamua kubadilisha laini, niliitupa laini niliyokuwa naitumia ambayo Martin alikuwa akiifahamu niliivunja na kuitupa mbali na kisha nikasajili laini mpya, na huo ulikuwa mwisho wa mawasiliano kati yangu na Martin.
Baada ya baba yake na Candy kuridhika na hukumu ambayo Maloya alipewa sasa aligeukia kuhusu kesi ya kifo cha mwanaye.
Taarifa mbalimbali zilianza kukusanywa ili kumbaini mtu ambaye alihusika na kifo hiko.
Nilifatwa shuleni kwa ajili ya kutoa ushahidi na ikagundulika kuwa sipo.
Mwalimu alishikwa na fadhaa sana kupata taarifa kwamba nimeondoka shuleni, alishindwa kuelewa ni kwasababu gani, inawezekana huyu mtoto anahusika na kifo cha Candy kwanini atoroke.
Martin alitamani kunitetea lakini alishindwa angesema mimi nina ujauzito si angehusishwa na huo ujauzito wangu kwa maana hakuna mtu ambaye hafahamu mahusiano yetu pale shuleni.
Alijaribu kunitafuta kwa kutumia simu hakunipata tena, alikuwa amenipoteza milele.
Niliendelea kuutunza ujauzito wangu chini ya uangalizi wa baba na baadhi ya ndugu wachache ambao waliguswa na matatizo ya familia yetu.
Shangazi yangu alihamia pale nyumbani kwa ajili ya kutuhudumia mimi na baba ukizingatia hali zetu hazikuwa nzuri
Nashukuru mungu kila kitu kilienda sawa, mimba yangu ilikuwa vizuri na wala sikupatwa na matatizo yoyote.
Nilifanya mazoezi, nilikula vizurui na kuhudhuria kliniki kila mara.
Asubuhi moja nikiwa bado nina usingizi mzito nilisikia hodi ikibishwa nyumbani kwetu, sikutaka kuamka hata hivyo sikuona kama huyo mtu ana dalili ya kuacha kugonga mlango, hodi zilipozidi niliona zinanisumbua nikatoka kiuchovu na kiunyonge huku nikiwa na hasira sana,
“kwanini shangazi hajaamka kwenda kufungua mlango mtu anagongaa.” Nilijiongelesha mwenyewe.
Nilitembea mpaka getini moyo ulinisita,
“au nirudi tu nikalale utakuta jimtu la ajabu ajabu sijui nini nini, aaaah nishafika getini ngoja tu nifungue”
nilifungua geti,
“Mungu wangu nimekwisha” nilisema.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: