Home → simulizi
→ RIWAYA: HIGH SCHOOL
SEHEMU YA KUMI NA MOJA.
Dakika chache baadae jopo la walimu liliingia, kila mtu alionekana akiwa na mshituko sana, nilizidi kutetemeka.
Jasho lilinichuruzika kwa wingi nilishindwa kusema chochote, walimu waliingiwa na mshangao baadhi ya walimu wa kike walishindwa kujizuia na kuangua kilio, eneo zima ilishikwa na taharuki. Wanafunzi madarasani hawakuelewa nini kinaendelea ingawa walihisi kuna kitu hakipo sawa pilikapilika zilizidi.
Mwalimu mkuu mr. Maige alikuwa akipiga simu kila wakati. Dakika chache baadaye polisi waliwasili eneo la shule, ving’ora vyao vikali vilinishitua nilijua kabisa mwisho wangu umekaribia, waliingia wakiwa wameongozana na madaktari pamoja na wandishi wa habari. Nilijua tukio lililokuwa mbele yangu sio dogo.
“Nini kimetokea?” polisi walianza kumhoji mkuu wa shule.
Mkuu wa shule alinyoosha kidole kwangu nilishituka sana,
Nilijua angeweza kujielezea yeye mwenyewe, Mungu wangu nitawambia nini mimi hawa Mungu nisaidie mimi niondoe katika mzigo huu, nilisali kimoyo moyo.
Polisi walinikata jicho na kisha wakanisogelea, wakanishika kama mtuhumiwa rasmi na kisha kunikokota nje kwa nguvu,
mkuu wa operesheni ile aliamrisha “piga picha za tukio na rekodi hali nzima ya tukio mimi nampeleka huyu polisi kuhojiwa na baada ya hapo mwili huo upelekwe hospitali kwaajili ya uchunguzi” aliongea na kuondoka.
Nilikokotwa na kupitishwa katika korido za madarasa watu wote walinishangaa Martin alishindwa kujizuia na kuuliza nini kinaendelea, polisi walimsukuma pembeni na kupita hakuna aliyejali, Martin alilia sana nilimtizama Martin huku machozi yakinitiririka.
Nilimwonesha kwa ishara kuwa kila kitu kipo sawa awe na amani.
Niliondoka na polisi hadi kituo cha polisi cha kati mkoni mwanza, niliogopa sana ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika polisi hakika nilitetemeka ee mungu wangu, eee yesu wa majeshi uliyewavusha wana wa Israeli katika bahari ya shamu naomba unitetee ukinitoa katika kifungo hiki jehova nitakutumika wewe siku zote,
siku hiyo nilikumbuka kusali tena kusali kwa kumaanisha huku nikibeba vifungu vya biblia ambavyo hata sikujua vinatoka sehemu gani.
Na wala sikuwa nafahamu mara ya mwisho nilivisoma lini.
Kweli shida hutufanya tumkumbuke Mungu.
Niliingizwa katika chumba ambacho nilihisi moja kwa moja ni chuma cha mahojiano.
Hakika kilinitisha sana,
Walinikagua hawakunikuta na kitu chochote kile.
“Mwanafunzi” sauti kali ya polisi wa kike iliinita,
niligeuka huku nikitetemeka jasho na machozi vikinitoka kwa pamoja.
Mkuu wa upelelezi alikaa mbele yangu alikuwa ni mbaba mtu mzima mwenye umri kati ya miaka 42-43 alikuwa na sura ya upole wala hakuendana na cheo alichokuwa nacho alinitazama.
“Jina lako ni nani?”
Polisi wa kike alikuwa pembeni yangu aliniuliza, mwanadada huyu alionekana kuwa katili sana na mwenye dharau tena alikuwa jeuri.
Alikuwa akiongea na mimi kama mtuhumiwa ambaye alikuwa akitafutwa muda mrefu sana na hatimaye siku hiyo alinasa katika mtego
“Jina lako ni nani wewe kahaba” aliniuliza kwa dharau na kwa kejeri,
Nilishindwa kuongea midomo ilinitetemeka.
Hatimaye mkuu wa upelelzi ambaye nilikuja kujua kwamba alikuwa akiitwa afande Lodrick aliniuliza alimwambia askari yule wa kike samahani naomba utupishe ingawa hakuridhia na uamuzi huo yule askari hakuwa na jinsi ni amri kutoka kwa bosi wake alipiga saluti na kuondoka tulibaki wawili tu.
Kwa kiasi fulani nilipatwa na ujasiri wa kuongea nilimwamini huyu mbaba kuliko yule mwanamke.
“Unaitwa nani?” aliniuliza,
“Naitwa Catherine kindamba”
“Catherine unaweza kutuambia ni nini kimetoke hata tukamkuta msichana yule akiwa katika hali ile?”
Nilisita nimwambie ukweli , nikimwambia ukweli nimejimaliza, kanisani tumefundishwa kuongea ukweli na sio uongo sijawahi kudanganya.
Upande mwingine uliniambia Cathe bado una nafasi ya kuishi kama utatumia ulimi wako vizuri na ukijiamini.
Ni kweli nimefundishwa kutodanganya lakini siku moja tu haitokuwa vibaya kumbuka unatetea nafsi yako.
Nilishikwa na ujasiri wa ajabu.
“Nilikuwa nimeenda chooni kwa ajili ya kujisaidia nilimkuta Candy amedodoka na anavuja damu.”
“Ina maana hujui nini kimemtokea Candy?”
“Hapana sijui”
“Unaweza kuzungumzia mazingira halisi”
“Niliingia darasani nikaambiwa kwamba natafutwa na Candy na ameelekea chooni nilikokuwa”
“Ikabidi nitoke nimfate Candy huko chooni nikamkuta hivyo.”
“Inamaanisha Candy alikuwa anakutafta kabla hajadondoka”
“Ndio sijui ni nini kimemtokea hata akadondoka niliongea kwa upole.”
“Sawa binti tunashukuru kwa ushirikiano wako tukikuhitaji tutakuita tena.”
Nilitolewa nje nikapandishwa kwenye gari nikarudishwa shuleni.
Kurejea kwangu kuliamsha kelele zisizo na mpangilio kila mtu alitamani kujua ni nini kimetokea, nilikuja kujua kwamba wanafunzi walipewa taarifa juu ya tukio lilitokea na kuhusu kukamatwa kwangu.
Niliporejea niliitwa moja kwa moja kwa mwalimu.
“Cathe ni nini kimetokea?” mwalimu maige aliuliza.
“Mwalimu nimemkuta Candy akiwa ameanguka kule chooni”
“Mungu wangu amepatwa na nini huyu binti?”
“Sijui mwalimu ni tukio la kuogofya sana nimelishuhudia”
“Sijawahi kuona tukio la hivi niliongea nikiwa nalia”
“Pole Cathe ni sehemu ya maisha jipe moyo Candy atapona na atarejea”
“Usijali hiyo ni mipango ya Mungu Candy atapona na atarudi”
nilishikwa na mshangao.
Inamaana Candy hajafa, nilijiuliza, mungu wangu kupona kwa Candy ni kifo changu Mungu wangu nifanye nini mimi nilibaki nimeduwaa,
sauti ya maige ilinishitua.
“Nenda bwenini ukapumzike”
Niliamka kiunyonge nikitetemeka nilishindwa kutembea nilijikuta nimedondoka ghafla nikaona giza mbele yangu sikujua nini kimeendelea tena.
<<<<<<<<<<<<<<<< ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: