NDOA YANGU.... EPISODE 7. Maongezi yangu na Tony yalinifanya nitambue kuwa Tony hanithamini tena kama mke wake hivyo basi nikafanya maamuzi ya kumpa nafasi. Nikampigia simu mama yangu na kumwambia narudi nyumbani kuwasilimia na nitakaa kwa wiki moja. Nilimshawishi kwa kumdanganya kuwa Tony amekubaliana na mimi. Mama alikubali na nikapaki begi langu vizuri tayari kwa safari ya kwenda kwetu. Asubuhi yake nikamwambia Tony kuhusiana na safari yangu. "Nilikusikiliza yote uliyoniambia jana Tony na nimeonelea wote tupeane nafasi kwanza. Nachukua break naenda kwetu kwa wazazi wangu" nilimweleza Tony. Tony akatikisa kichwa chake na kusema, "unatakiwa ujionee hata aibu Vicky. In fact hata wakisema wanawake bora wasimame inatakiwa ufiche uso wako kabisa kwa aibu. Umeshindwa kutunza nyumba yako, umeshindwa kumridhisha mume wako na baada ya kutatua hayo matatizo umeonelea bora uyakimbie?" Tony, nimekataa wewe kunidhihaki na kunitukana. Nilikaa kimya wakati unanitukana jana na sio kwamba mimi nitaendelea kukaa kimya tu uendelee kunitukana. Umesema uwepo wangu unakupa huzuni, sasa hivi nataka nikupe nafasi. Naenda kuchukua muda wangu kuomba kwa ajili yetu." "I don’t freaking need your prayers madam. In fact hata Mungu hatajibu hayo maombi yako kwa sababu Mungu ameshakueleza kila kitu cha kufanya kwa mume wako katika Biblia. Sitaki uniombee mimi." "Eee kwahiyo ile siku nimenunua lingarie na mafuta ya massage na ukaniacha nikining'inia tu usiku kucha usitokee nyumbani nayo utasemaje? Sikuwa natimiza majukumu yangu? Umechanganyikiwa Tony. Hujui ni nini unataka!" "Unataka kuondoka? Sawa! Get the hell out but you just might not meet this marriage when you come back...nakwambia hutaiona tena hii ndoa ukirudi" "Kama nilivyokwambia Tony, nachukua muda mbali na wewe naenda kuiombea hii ndoa, hayo maneno yako yakashindwe. Mungu ata-sustain nyumba yetu" nikamwambia Tony. Akatingisha tena kichwa chake, akafumba macho, akavuta shuka akimaanisha amemaliza maongezi na mimi. Nikachukua mabegi yangu na kuelekea Airport. Nikaenda ofisi za wakala wa usafiri wa anga na kununua tiketi ya ndege ya Fastjet ya kuelekea kwetu Mwanza iliyokua ikiondoka saa nne asubuhi. PASIANSI, MWANZA, TANZANIA. Usiku wake nikiwa nimeshafika nyumbani mapema tu mchana, nikiwa nimekaa na wazazi wangu sebuleni mama alikuwa akijaribu kunipigisha story za hapa na pale. "Ehee kwaio kwanini Tony amekupa ruhusa ya kuja huku mama angu?" "Mama, Tony yuko busy na kazi, hata baba nimemwambia hapo kabla" "Kwaio ameshindwa hata kuja kutusalimia mara moja pamoja na wewe halafu ageuze hata kesho. Hatujamuona tokea ile siku ya harusi." "Si ndio maana nipo hapa mama? Atleast umeona hata mmoja wetu, ukiniona mimi umemuona Tony..si unajua tu mwili mmoja hahaaa." Nikamwambia na kucheka. "Ahaa, hamna tatizo. Nimejaribu kumpigia baada ya wewe kufika kumwambia kwamba nimempokea mke wake lakini hajapokea simu" mama aliongea. "Nina uhakika atakupigia kesho, atakuwa amepumzika mapema leo ukizingatia ni weekenda halafu mimi sipo." Nilimwambia mama. ”Sawa mwanangu, ila Vicky vipi maisha ya ndoa? Ninaimani unamtii mume wako na kumjali vya kutosha." Mama aliongea. "Mama, kwani Tony amelalamika kwako? Najitahidi kadiri ya uwezo wangu." "Mbona unajishuku Vicky? Kila kitu kipo sawa kweli huko ulikotoka? Ninajua kuchelewa kupata ujauzito hakukupi pressure." "Hapana mama, tuko sawa kabisa. Kila kitu kipo vizuri." "Usiwe na pressure ya mtoto. Hata mwaka haujaisha bado. Mimi na baba yako tulisubiri miaka mitatu kabla hatujampata kaka yako wa kwanza na baada ya hapo mambo yakatuendea vizuri. Hivyo usijali kila kitu kitakuwa sawa." Mama alimaliza. "Nafahamu mama...." Mara tukasikia mtu akigonga mlango. "Mama unategemea mgeni yeyote usiku huu. Ni saa tano na nusu sasa na baba ameshaenda kulala." "Hapana mwanangu sina ugeni wowote, inaweza kuwa mmoja wa majirani zetu anahitaji kitu nenda na ufungue mlango." Nikiwa ninaosogelea mlango ili kuufungua, niliangushwa chini kwa nguvu na mlango uliofunguliwa kwa nguvu. Macho yalinitoka na kupiga kelele, walikuwa watu wanne waliovalia kofia zilizoziba uso mzima na kubakiza mdomo, macho na pua wakiwa wameshika mapanga. Nilifunga macho yangu na kuanza kusali. "Sawasawa sali kwa bidii mtoto mzuri, unaweza ukakipata unachokiomba" sauti nzito na mbovu ilisikika kutoka kwa mmoja wapo wa wale watu watatu. Mara wakaanza kunivuta nywele zangu na kunipeleka mpaka sebuleni. Nikamuona mama yangu akiwa amejibanza kwenye kona ya sebule akilia mno, bila shaka alisikia zile purukushani. Tulikuwa tumevamiwa na majambazi! SIKU TANO BAADAE. Niliamka tena huku nikiwa napiga kelele kama kichaa. Imekua ni kawaida yangu kushtuka na kupiga kelele kama mwendawazimu tokea ule usiku mbaya kabisa katika maisha yangu. Usiku tuliovamiwa na majambazi. Baba yangu alikuwa pembeni yangu, akinifuta machozi yaliyokuwa yakinitoka kwa wingi. "Usijali Vicky. Upo sawa na salama kabisa. Baba yako nipo hapa." "Baba naogopa, Tony bado hajaja." "Nafahamu mwanangu, Tony hajaja. Nitampigia simu tena. Jitahidi uwe na nguvu kwanza, sawa mwanangu?" "Hapokei simu zangu baba, tokea umemwambia like tukio hajapokea tena simu yangu baba!!" "Usijali mwanangu atakupigua tu, labda alipatwa na mshtuko baada ya mimi kumsimulia lile tukio. Tusubiri atulie atakupigia tu" Baba alipotoka chumbani kwangu na kuniacha peke yangu nikaanza kukumbuka lile tukio. Usiku mbaya kabisa katika maisha yangu...naweza kuuita 'evil night'. SIKU TANO NYUMA. Nakumbuka baba yangu alifuatwa chumbani na wale majambazi na wakamtaka awape pesa. Nakumbuka walimpiga na ubapa wa panga na kusachi chumba kizima. Aliwapa shilingi laki tano hivyo wakadhani anazo pesa nyingine kwani asubuhi yake alikuwa ametoka kuuza ng'ombe zake 88 huko wilayani Magu. Baba hakuwa na Cash, pesa zote aliweka benki. Nakumbuka niliwaongezea shilingi laki moja niliyokuwa nayo na mwanaume mmoja kati yao akaniambia ninamtukana kwa kuwapa shilingi laki moja tu. Nikiwa ninawaomba msamaha, yule jambazi aliniangalia kwa macho fulani ambayo nilijua anataka kufanya nini kabla hajaniambia. "Tafadhali jamani, mimi nimeolewa. Ninawaombeni msinifanye mnachotaka.kunifanya. Nawaomba for christ sake! "Kwaio kama umeolewa unafanya nini nyumbani kwa baba na mama. Mume wako hakuridhishi ee mama? Ngoja nimsaidie hilo suala. Anahitaji msaada." Yule jambazi aliongea. Niliomboleza na kuwaomba wasinibake, mama na baba nao wakaomboleza kwa kuwapigia magoti wale watu wabaya na jawabu walilowapa ni kwamba wamesikia ombi lao na kitu pekee watachokifanya sio kunibaka mbele yao. Majambazi wawili wakabaki sebuleni wakiwalinda baba na mama na wengine wawili wakanivuta mimi mpaka chumbani. Nilipigana kadiri ninavyoweza lakini walinizidi nguvu. Mmoja akanishikilia na mwingine akafanya mambo yake, maumivu niliyoyapata sijawahi kukumbana nayo. Nilimkumbuka mume wangu Tony, nikajilaumu kwanini niliondoka kwa mume wangu, kwanini niliwadanganya wazazi wangu... Nikakumbuka jinsi Tony alivyonizuia nisiondoke na kumwacha. Nililia mno, yule jambazi aliendelea kunifanyia kitendo cha kinyama na dakika 30 baadae akawa amemaliza. Baada ya yuke jambazi kumaliza, wakaambizana waondoke haraka...wakaondoka na kutokomea kabisa! Niliumia mno, kwa mara ya pili tena nikamlaumu Mungu na kumuuliza maswali mengi. Ukimya wake ulinipa simanzi na nikajidharau mno! MUDA HUU. Zimepita siku tano tokea nifanyiwe like tukio la kinyama ule usiku, siku tano baada ya baba kumpigia simu Tony na kumtaarifu na siku tatu tokea nitoke hospitali ya Bugando, bado Tony hajaja na hapokei simu tena.... Sina nilichobakiza kusema nitaiishi kesho, nipo radhi nife hata sasa hivi...... ITAENDELEA.......... TUKUTANE JUMATATU KWA MWISHO WA SIMULIZI HII. Weekend njema!! Share Jumaa Mmak

at 12:18 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top