Home → simulizi
→ NDOA YANGU...
EPISODE 6.
Baadhi yenu mnalalamika hamjaziona episode zilizopita, pitia timeline yangu mtazikuta nyuma.
Haya songa nayo....
Kama masaa nane hivi nilikuwa nimekaa ofisini kwa daktari nikisubiri kupewa maelezo ya kina kuhusiana na hali ya Tony. Nilichoambiwa wakati nikisubiri ni kwamba Tony yuko hai na ameingizwa kupigwa 'ultrasound' na baadae afanyiwe upasuaji.
Manesi hawakutaka kuniambia ukubwa wa ajali aliyoipata Tony, nilikuwa nikilia tu nakupiga kelele kama nimechanganyikiwa. Baadae nikampigia simu wifi yangu ambae alikuja haraka kusubiri nami huku akinibembeleza.
Nilitoka hospitali mara moja na kwenda Myfair plaza kwenye mashine ya ATM ili kutoa pesa maana sikuwa hata na mia, ilikuwa tayari saa kumi na moja kasoro jioni na sikuwa nimekula wala kunywa kitu tokea jana yake jioni.
Baada ya kurudi hospitalini, nikaonana na daktari mwenye asili ya kihindi na akaanza kunieleza kilichojiri.
"Mrs Tony, Asante sana kwa uvumilivu wako" mimi nikamkatisha haraka.
"Mr. Daktari, please just go straight to the point, acha kuanza kuzunguka zunguka. Anaendeleaje? Nini kimetokea? Upasuaji ulikuwa wa nini? Yuko salama? Upasuaji umefanikiwa?
"Madam, nitakujibu maswali yako yote, ila nataka utulie kwanza acha papara"
"Okay, samahani, endelea nakusikiliza"
"Mume wako yuko salama, na upasuaji ulikuwa wa mafanikio. Alipatwa na kitu kwa kitaalamu kinaitwa 'testicular trauma' ni injury inayotokea kwenye korodani za mwanaume.
"Kwa wanaume korodani au testicles zinakaa nje ya kitu kama kipochi hivi kinachoitwa kwa lugha ya kitaalam scrotum. Kutokana na location yake, aina nyingi za ajali zinazotokea husababisha kuumia kwa korodani.
"Mfano wa ajali hizo ni kama vile kupigwa kwa mpira au kitu chochote ktk maeneo nyeti, ajali ya pikipiki na ajali ya baiskeli ambayo kwayo ndio mume wako alikumbana nayo.
"Mungu wanguu!!!!! unaona matatizo haya..unamaanisha nini daktari? Kwamba mmezitoa, mume wangu hana korodani tena? Mamaaa tutapataje mtoto sasa uwiiii nafwaa mie...Tony ataniuaaaa woiii!!!" Nilichanganyikiwa!
"Tafadhali binti hebu relax basi, mbona unadandia treni kwa mbele. Mimi sijakueleza kwamba mume wako hana korodani hapa. Ni rapture tu ndogo ilitokea na kuhama kwa testicles na ndio maana ikatubidi kumfanyia upasuaji haraka"
"Upasuaji kama nilivyokwambia ulikuwa wa mafanikio na tumeweza kuzirudisha mahala pake na tuna uhakika haitasababisha asiwe na uwezo wa kuzaa hapo baadae"
"Ofcourse ninashauri akae mbali na Sex kwa muda kama wiki tatu hivi mpaka apone vizuri kabisa ili asiweze kupata kitu kinaitwa 'hernia'. Vinginevyo kila kitu kipo sawa sasa, tumshukuru Mungu.
"Asante sana daktari, kwaio lini tutaruhusiwa kurudi nyumbani?"
"Nataka nimtizame usiku huu kuhakikisha yuko sawa. Akiamka kesho vizuri nitaruhusu muondoke"
Usiku ule dada yake aliondoka baada ya kuhakikishiwa Tony yuko salama.
Mimi nilikaa hospitali chumba alicholazwa Tony nikiwa pembeni ya kitanda chake, huku machozi yakinitoka usiku kucha, nilikumbuka mambo mengi sana enzi za uchumba wetu jinsi tulivyopendana na kuona ulimwengu wote ni wangu.
Asubuhi yake baada ya kufanya malipo tuliruhusiwa kutoka, Tony alikuwa mkimya asiongee hata neno moja. Nikiwa na-drive nikawa kichwani nawaza kama Tony hataamsha tena hasira zake juu yangu.
Nikawa nikimuomba Mungu kimya kimya Tony asianze masuala yake tena.
"Darling uko sawa?" Nilimuuliza baada ya kufika nyumbani na kumlaza chumbani.
"Vicky, siko sawa. Unajua nini? Ninajuta kukuoa wewe. Sidhani kama kweli mwanaume apatae mke amepata kitu chema na kupata kibali kutoka kwa Mungu kwa sababu wewe ndio chanzo cha mimi kutokuwa na furaha na kujawa na huzuni.
Nikamshangaa Tony, sikumuelewa!!!
"Unajua nini, nilipoamua kukuoa wewe nilikuwa na mipango mingi. Nilifahamu ni nini ninataka. Nilitaka mwanamke ambae atanipenda na kunifanya niwe na furaha. Nilitaka maisha ya furaha, faraja na amani.
"Nilitaka kujenga nyakati nzuri zenye ubora wa hali ya juu katika ndoa yetu wawili tu mimi na wewe kabla hata hatujaanza kuzaa.
"Ila sijafanikiwa kupata lolote kati ya hayo, ikawa ni matatizo tu hili baadae linakuja hili. Tupo kwenye ndoa kwa miezi tisa tu na tayari nimeshachoka"
"Tony, kwanini unanilaumu mimi kwa hayo? Kwanini? Kipi cha msingi ambacho mimi nimekifanya ambacho kimeharibu hiyo unayosema furaha yako?"
"Nisikilize Vicky, baada ya ndoa tu ilinichukua wiki mbili nzima wewe kuniruhusu kufanya tendo la ndoa na kuiondoa bikira yako. Honeymoon yetu hata sikuifurahia kwakuwa ulikuwa ukinizuia kufanya tendo la ndoa.
Baadae sana Baada ya kuniruhusu kutoa bikira yako kwa mbinde kweli ukaanza wenge lako la kutaka mtoto na kufanya tendo la ndoa liwe linaboa kila mara.
"Kila nikikueleza kwamba tusubiri kwanza tufurahie ndoa yetu kabla hatujaanza kuzaa na kulea wewe unakua mbogo. Kila nikitaka kufanya tendo la ndoa kwa style tofauti wewe hutaki unataka missionary style kwa madai kwamba ndio style nzuri ya kupata ujauzito.
Kwa wenge lako la kutaka mtoto mapema baada ya miezi mitano tu ukaanza huo mfungo wako na kwa sababu ya mawazo na frustration ulizonipa nikawa sina furaha na stress juu.
"Jana asubuhi nikaenda kufanya mazoezi na baiskeli yangu na kutokana na stress na mawazo uliyonisababishia wewe nikapata ajali.
"Unafahamu wewe ndio umenisababishia haya? Nilikuwa nikikufikiria wewe mpaka nikapoteza concentration na shetani alivyo mpumbavu was trying to crack a joke, testicular trauma? I am tired madam"
Nilikaa kimya nisijue lipi la kuongea, zaidi zaidi hasira zikawa zikinipanda.
"Unathubutuje kuniambia hayo Tony? Kwanini unanilaumu mimi kwa kuwa na huzuni na kukosa hiyo furaha yako! Kila siku naamka kukuombea na hii ndio namna unavyonilipa?
"Sio wewe ambae wakati unanioa mtaji wa kampuni yako ulikua na kufikia kutengeneza faida kubwa? Unathubutuje kunitukana na kunilaumu mimi sasa hivi!! Sitaruhusu shetani aendelee kukutumia tena Tony, amekutumia vya kutosha!
"Haya maongezi yameisha Tony, sasa hivi fanya lolote unalotaka. Nikasimama pale kitandani na kutoka nje huku nikiwa nimeghafirika mno. Na kwa mara ya kwanza tena nikaona bora ningekuwa single tu.......
ITAENDELEA.........
Lunch njema!
Share
Jumaa mmaka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: