Home → simulizi
→ NDOA YANGU.....
EPISODE 5
Jumamosi asubuhi Tony aliporudi nyumbani asubuhi nikaamua imetosha sasa liwalo na liwe. Hakuwa na haki ya kuendelea kulala nje ya nyumba yetu eti kwa sababu ya hasira.
Nilikuwa tayari ninamsubiri afike na alipoingia tu nikasimama nikamzuia mlangoni na kumuuliza kwa jazba.."Eheee unafikiri ulikuwa wapi Mr. Tony?"
Akanitizama kwa mshangao kama nimeota mapembe na kwa mshangao akanijibu kwa mkato.."Bahari Beach Hotel."
"Kwaio ndio huko unakolala siku zote?" Nikamuuliza huku nikiwa na uhakika hatanijibu palepale.
"Yes nilichukua chumba pale" akanijibu huku akinitizama. "Ni hayo tu?" Tony akaniuliza
"Hapana Tony, sio hayo tu na usinifanye mimi mpumbavu. Umekuwa ukilala nje takribani wiki tatu sasa na ninakuuliza unanijibu kwa dharau" niliongea huku nikiwa nimejawa na hasira!
"Madam, umeniuliza nilikokuwa na nimekujibu vizuri tu, ni kivipi nimekuonesha dharau?"
"Tony, kwa mara nyingine nakuomba unisamehe"
"Okay nimekusikia. Kuwa muwazi basi unaomba msamaha wa nini?
"Well, nisamehe kwa kukunyima tendo la ndoa na kufunga bila makubaliano na wewe. Samahani kwa kutokujali hisia zako. Please tunaweza tukarudi kuwa kama zamani tulivyopendana?"
"Okay, nimekusikia" akanijibu huku akitizama saa yake.
"Tony sasa hivi please. Unataka niseme au nifanye nini unisamehe?"
"Vicky nimesema nimekusikia. Please don't stress me. Nataka nikafanye mazoezi na baiskeli yangu kidogo, umenielewa?"
”Okay that is fine. Nataka unipe ahadi kwamba kuanzia leo utabaki nyumbani"
"Yes nakuahidi nitabaki, kwahiyo unaniruhusu niende nikabadili na kwenda kufanya mazoezi?"
Nikatikisa kichwa na kumpisha njia na akaenda chumba cha wageni na kuvaa nguo za mazoezi. Siku zote alikuwa akivutia na kuonekana handsome akivaa nguo za mazoezi zilizokuwa zikimbana na kuonesha misuli yake iliyotuna sawasawa.
Nikaenda kumkumbatia nikitegemea atanikatalia lakini akanikumbatia vizuri tu na kuondoka na baiskeli yake ya mazoezi. Asubuhi ile nilifurahi mno na nikaamua nimpikie breakfast nzuri ale akirudi kutoka mazoezini.
Baada kama ya dakika 30 hivi nikapigiwa simu iliyobadili maisha yangu kabisa. Huku machozi yakinitoka nisijue kwanini, nilichukua funguo za gari yangu na kuwahi Hospitali ya TMJ nilikoelekezwa.
Nilikua bado siamini kama kweli nimeambiwa Tony amepata ajali!! Ni dakika 30 tu zimepita tokea aondoke nyumbani, alienipigia simu hakuweza kuniambia ajali ilikuaje na ukubwa wake.
Nikakutana na foleni kubwa. Nikajaribu kupiga simu ya Tony ili kupata details lakini simu yake ilikuwa imezimwa. Nikataka kuwapigia ndugu na marafiki lakini nikajiambia natakiwa nijue hali yake na ukubwa wa ajali aliyoipata kwanza kabla sijamwambia yeyote.
"Oh Mungu wangu nisaidie mwanao. Wewe mwenyewe ulisema hatutakufa bali tutaishi. Tafadhali Mungu mponye mume wangu, sitakuwa mjane nikiwa kijana hivi oh Mungu"
Maneno ya kusali yakaniishia, sikujua hata namna ya kuomba. Baada ya saa moja hatimaye nikafika hospitali ya TMJ. Nikapaki gari Myfair plaza na kuvuka upande iliko hospitali ya TMJ.
Nikatembea haraka haraka kuwahi mapokezi huku nikiwa nina hofu na uoga mkuu nisijue ni nini naenda kukikuta huko......
ITAENDELEA.......
Share
Jumaa Mmaka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: