NDOA YANGU... EPISODE 4. Ni wiki moja imepita tokea nimalize mfungo, Tony hajawahi kulala hata usiku mmoja nyumbani. Ilikuwa akirudi asubuhi sana anabadili nguo na kwenda kazini. Kila asubuhi nilikuwa nikimuomba arudi nyumbani lakini sikufanikiwa. Alikuwa akirudi tu anapitiliza moja kwa moja chumba cha wageni anabadili nguo na kuondoka asiniongeleshe hata neno moja. Nilianza kufikiri kwanini nisingemkubalia tu kipindi kile. Sikufikiri kama ingefikia hatua hii. Na sikufahamu nitumie njia gani kumaliza hili tatizo. Nilifahamu Sex ni jambo la muhimu kwa wanaume, lakini kwangu sijui ni nini sikuwahi kufurahia hata siku moja. Siku ambapo Tony aliondoa bikira yangu nilifikiri maumivu yataishia siku ile ile kwamba siku nyingine nitakuwa nikifurahia tendo. Lakini ile miezi mitano kabla sijaanza mfungo, kila tulipokua tukifanya tendo la ndoa yale maumivu niliendelea kuyapata. Ukweli ni kwamba nilitamani tuishi tu bila ya kufanya tendo la ndoa. Ila kwa kuwa ni ndoa sikua na jinsi. Mwishoe nikaona labda nahitaji ufumbuzi wa kimwili zaidi kwani ufumbuzi wa Kiroho haukuwa ukileta matunda yeyote kwa Tony. Nilichukua simu yangu mchana ule baada ya kutoka kazini nikaingia 'google' na kutafuta "jinsi gani ya kuzuia maumivu wakati wa tendo la ndoa?". Yalikuja majibu mbalimbali nikasoma baadhi na baada ya kumaliza kusoma mikao mbalimbali ya tendo la ndoa ili kutoumia wakati wa tendo, nikaazimia kufanya maamuzi ambayo yatanifanya nifurahie tendo. Baada ya hapo nikatafuta tena katika 'google' "Jinsi gani ya kumshawishi mumeo ashiriki tendo na wewe" yakaja mambo ambayo kwangu niliyaona hayana upako. Ila nikaamua kuyasoma baadhi ili niweze kuyatumia kuhakikisha Tony analala na mimi. Nikapata texts kadhaa kutoka 'google' na kuamua kuzi-copy na kumtumia Tony kwa interval ya lisaa limoja. Text ya kwanza nikamtumia ikisema; "Nakuhitaji mme wangu, mwili wangu unakutamani mno" Baada ya saa moja bila kupata jibu lolote, nikamtumia text nyingine ya kingereza niliyoipata hukohuko 'google' iliyokua ikisema; "I can’t focus, all I can think about is what you will do to me if you were here with me" Ila napo sikupata majibu yoyote, baada ya dakika 39 za ukimya nikaamua kumtumia text nyingine ya kiingereza niliyotunga mwenyewe iliyosema; "You taught me how to make love, tonight I will show you how much I have learnt" Nikapata majibu text yake ikisema, "please niko kwenye kikao na bodi" Nilifurahi mno, nikaruka juu kwa furaha kutoka kwenye kochi nililokuwa nimekaa. Nilifurahi kwa kuwa ndio maneno pekee Tony aliyoongea na mimi. Hajaongea na mimi kwa wiki sasa. Nikaamua kumtumia na nyingine tena; "Okey mume wangu, nakufikiria kweli nakusubiri kwa hamu" akaijibu mapema kwa kuniambia; "Acha upumbavu Vicky" Nikamtumia nyingine iliyosema "please njoo nyumbani ulale na mimi leo. Nimekubali nilikosea. Nahitaji kurekebisha na wewe. Tafadhali nipe nafasi nyingine. Nakupenda my baby" Akanijibu "Okay" Nilifurahi sana nikaondoka haraka na ku-drive mpaka Game supermarket mlimani City nakununua matching lingerie (nguo ya usiku yenye mvuto wa kimahaba). Nikanunua foot massage kit na body massage oil. Nilisoma kwenye google kwamba kumfanyia mwanaume massage ya miguu na mwili kunaweza kufanya maajabu na mume akashawishika kushiriki tendo na wewe. Pia nikanunua lubricator. Google ilinifundisha vingi mno. Baada ya kumaliza manunuzi nika-drive haraka kupitia barabara ya sam Nujoma, nikanyosha barabara inayoelekea Coca cola Mwenge na kukatisha kulia kuelekea barabara inayoelekea clouds media group. Nikafika nyumbani mida ya saa moja usiku, nikaandaa chakula ambapo nilimpikia Tony fried rice na kuku. Mpaka kufikia mida ya saa mbili usiku nilikuwa nimeshamaliza kila kitu na nimejiandaa kumpokea Tony. Nilikaa kwenye sofa nikiangalia Movie iitwayo 'Me before you' huku nikiwa nimevaa lingarie ambayo kwa hakika ilikua inavutia kwani ilikua imenichora vizuri umbo langu namba nane ambalo Tony alikuwa akisema linamvutia mno. Nikajaribu kumpigia Tony lakini akawa hapatikani kwenye simu. Nikasubiri! Lakini hakutokea..nikaendelea kumpigia lakini sikuweza kumfikia... Usingizi nao haukuniacha salama, nikaanza kusinzia na kuona watu wawili wawili kwenye TV...mwishoe nikapitiwa na usingizi kabisa kwenye kochi. Nikaamshwa na mlio wa mlango ukifunguliwa, nikatizama saa na kukuta ni saa moja asubuhi. Tony hakurudi ule usiku, instead alirudi asubuhi. Akaingia, akanitizama kwa sekunde kadhaa na kupitiliza moja kwa moja kwenye chumba cha wageni kubadili nguo kama kawaida yake bila kunisemesha lolote. Nikainamisha kichwa changu, nikalia mno, nikaomboleza zaidi pale alipojifungia ndani. Nilipatwa na uchungu mwingi....kwa mara ya kwanza nikamlaumu Mungu... ITAENDELEA..... Jumaa Mmaka

at 12:17 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top