NDOA YANGU.... EPISODE 3 Ilipoishia.. Jibu lake lilinifanya nilie kilio kikubwa na uchungu mwingi.....oh ndoa yangu, masikini mimi kumbe sikujua!!!!... Endelea... Alinitumia text ikisema, "please muulize roho mtakatifu atakwambia nilipo na kwa nini sirudi nyumbani." Nikasema sasa imetosha, nimechoka na tabia ya Tony nikajiambia kwamba sasa tunahitaji councelling. Nilimsubiri asubuhi yake arudi lakini hakuonekana. Nikampigia simu mchana baada ya kujawa na wasiwasi mwingi lakini hakupokea simu yangu. Baadae kidogo nikapata text yake aliyoiandika kwa kingereza akisema; ”I am quite surprised you are looking for me. Don’t worry, I am fine. Don’t let me distract you from God”. Akimaanisha anashangaa kwanini ninamtafuta, kwamba yuko mzima hataki anisumbue juu ya suala langu la kufunga na kuomba. Nikaamua ni muda sasa wa kuomba ushauri kwa mama mchungaji. Jioni ike nikaenda nyumbani kwa mama mchungaji na baada ya sala ya jioni tukaanza kuongea kuhusiana na changamoto za kufunga tokea tuanze mfungo. Nikamuelezea kuhusiana na uhusiano wangu na Tony ulivyo kua na matatizo. Nilijua nitapata ushauri wa namna ya kufanya kutoka kwa mama mchungaji. Mama mchungaji akasikitika sana kwa kutingisha kichwa nilipomuonesha texts za Tony. Dada Vicky, Biblia inasema nini juu ya kuheshimu wazazi wako?" "Waheshimu baba na mama yako, ili siku zako za kuishi zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA" nikamjibu haraka huku nikimshangaa kwanini anaongelewa wazazi wakati mimi nahitaji ndoa yangu iponywe. "Unakumbuka kipindi ulipokuja kwangu na kuniambia umeamua uolewe na huyo kijana Tony ambae ndio kwanza alikuwa mbichi katika imani? Nilikuasa uolewe na waliobobea katika imani. Kama ungeyasikiliza maneno yangu huenda haya yasingetokea" aliongea huku akionekana amekasirika. "Samahaniama, nampenda mume wangu na ninafikiri anampenda Mungu pia" "Anampenda Mungu?, Bado unatetea matendo yake? Mume ambae hataki kukubaliana na wewe katika maombi atawezaje kumruhusu roho mtakatifu aingie mwilini mwake? Aliniuliza! "Samahani mama" mama alikuwa akijulikana kwa hasira na sikutaka kuendelea kumuudhi. "Hata hivyo agano limeshafanyika, ni mume wako. Inabidi tutafute way forward. Unaona shetani hapumziki. Yupo kazini kuharibu ndoa yako. Kumbuka maandiko Waraka wa paulo mtume kwa Waefeso 6:12 inasema, "kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" "Hii vita sio dhidi ya mume wako bali ni vita dhidi ya roho na pepo wabaya" "Sawa mama" nikajibu. "Shetani anafahamu kabisa kwamba mfungo huu utaiokoa ndoa yako na anataka kuhakikisha anazuia hilo. Endelea kuhakikisha unasugua goti kwa Mungu" "Sawa mama. Nifanye nini sasa kuhusu Tony kukataa kurudi nyumbani?" "Usijali Vicky, Tony atarudi nyumbani, ni kama mtoto wa Prodigal kwenye kile kisa cha wana wawili wa baba tajiri katika kitabu cha Luka 15:11-32. Ninao uhakika utarudi. Tumuombe Mungu mpendwa". Niliondoka nyumbani kwa mchungaji baada ya masaa mawili ya kuomba. Nilijihisi nina nguvu mpya. Nilitakiwa nijikite katka kuomba na nisiache imani yangu iyumbishwe. Nilipofika nyumbani nilimkuta Tony akiwa ame-relax sebuleni, nilithibitisba kauli ya mama mchungaji kwamba Tony atarudi tu nyumbani kama alivyotabiri. Siku zilivyozidi kwenda na ndivyo mambo yalivyozidi kuparanganyika. Tony akaacha kwenda kanisani kwetu na kunitaka nihamie kanisa alilohamia yeye. Nilipingana nae idea yake. Sikutaka kukubaliana na uamuzi wake. Nikawa napokea text za kunipa moyo na kunifariji kutoka kwa mama mchungaji. Mwishowe siku 100 ziliisha. Ikatangazwa kanisani kuwa wanandoa tuhudhurie pamoja katika mkesha wa ibada ya maombi. Nikambembeleza kweli Tony twende pamoja lakini akanikatalia kata kata. Sikuwa na jinsi nikaenda kwenye maombi peke yangu. Usiku ule niliomba kila aina ya maombi. Furaha yangu ilikua juu ya kwamba sasa ugomvi na Tony utakua umeisha. Nilijihakikishia tutafanya tendo la ndoa kadiri atakavyotaka yeye. Kumbe nilikua najiongopea..... ITAENDELEA.... Lengo langu story hii iishe mapema, hivyo kila nitakapokuwa napata muda nje ya majukumu yangu nitakuwa nawawekea hapa bila kuzingatia ni lini na muda gani. Nia ni wote tujifunze, tuwe makini na maamuzi yetu na kung'amua mambo ya msingi ili kudumisha mahusiano na ndoa ambako kwayo tunajenga taifa lenye nidhamu na maadili mema. Read and share, it will definetly bless others. God bless you! Jumaa Mmaka Kipusa

at 12:16 AM

Bagikan ke

1 comments:

avatar

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma

Kwaheri Gerd Ulrich

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top