NDOA YANGU..... EPISODE 2 Ilipoishia jana; Nilijua kabisa nipo kwenye jaribio kubwa sana la ndoa yangu, nilitakiwa kuomba sana juu ya mume wangu...labda sikujua ni nini natakiwa kufanya kama mke! kwa kweli nilichoka.......... Sasa endelea.... Baada ya Tony kuondoka, niliazimia hili jambo nilifikishe kwa Mungu wangu kupitia maombi. Niliingia ndani na kuanza kusali. Nilisali kwa takribani masaa mawili nikimlilia Mungu juu ya ndoa yangu. . "Baba nilinde juu ya ndoa yangu, ondoa kila aina ya ushetani unaomnyemelea mume wangu. Mithali 21:1 inasema, "Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote aendapo." . Oh Mungu wangu geuza moyo wa mume wangu Tony asipende Sex mpaka siku hizi 100 za kufunga ziishe..Amen. Baada ya sala ya muda mrefu nikajihisi kupata moyo upya na nikapata namna ya kufanya. . Nilikuwa sina sababu yeyote tena ya kuweza kumshawishi Tony asifanye mapenzi na mimi, hivyo nilitakiwa nitumie busara tu kuzuia kwa kufanya mambo ambayo yatamfanya Tony asitamani kufanya tendo la ndoa na mimi. . Hivyo nikaamua nisioge siku nzima. Nilifahamu fika ni jinsi gani Tony alivyokua akipenda kuniona nikiwa naoga na kuwa msafi nikinukia muda wote. . Alirudi nyumbani mishale ya saa moja jioni, nilihakikisha chakula cha usiku nimeshakiandaa. Nilijua tu lazima malumbano yataanza tena. Na kwa kweli sikukosea maana baada tu ya kuingia ndani akaanza; . "Madam, umeshaweka mambo yako sawa?" "Mambo gani Tony?" Njoo ule chakula nilichokuandalia" "Ulifikiri ninakutania? Unafikiri kwa kutokuoga kwako kutasaidia kunibadilisha maamuzi yangu? Au unafikiri mimi ni mpumbavu nisijue kwamba kutokuoga kwako leo ni trick ya kujaribu kunizuia nisishiriki na wewe sex?" . Kwa kweli nilipata mshtuko na kigugumizi nisijue niongee nini baada ya yeye kugundua plan yangu ilikua ni nini. "Tony please naomba unielewe. Natakiwa nijikite kwa Mungu." Nikaanza kumuomba Tony. . . "Vicky, get it straight, mimi sikulazimishi usifunge. Kuna ubaya gani kama tukishiriki tendo kati ya saa kumi na mbili jioni unapofungua funga yako mpaka saa sita usiku unapoanza funga yako tena? Hicho ndicho ninachokuomba Vicky mke wangu." . "Samahani Tony, siamini kama hivyo ndio vizuri zaid. Natakiwa niwe msafi bila kushiriki tendo siku zote 100. Kushiriki tendo katikati ya hizo siku nitajisikia si msafi." Nikamuelezea hayo Tony. . "Upi si usafi katika tendo la ndoa kati ya mume na mke waliohalalishwa? Tunaruhusiwa kabisa!!" . "Nisikilize Tony, unatakiwa uwe mvumilivu. Nimebakiwa na siku 85 tu baada ya hapo tutafanya mpaka mwenyewe uchoke" . "Ngoja nikwambie kitu Vicky, hii ni mara ya mwisho kwangu kuongelea hili suala. Kama umeshindwa namna ya ku-balance ndoa yako na kufunga, basi utakua huna tena hiyo ndoa baada ya kumaliza hizo siku zako 100 za kufunga_ . "Nini unamaanisha Tony? Mungu aingilie kati kuzuia hayo maneno mabaya ya mkosi yatokayo kinywani mwako." . Tony akaniacha nimesimama pale na akaelekea chumbani. Nikapata mshangao baadae usiku pale Tony alipoanza kuhamishia vitu vyake chumba cha kulala wageni. Nilitaka niende nikamuombe asifanye vile lakini baadae nikaamua ni bora akae huko kwa hizo siku 85 zilizobaki. . Labda huu ulikua mpango wa Mungu kunitafutia ufumbuzi. Nikamshukuru Mungu kwa kunipa ile njia ya kukaa chumba tofauti na Tony na hivyo kutosumbuliwa tena juu ya tendo la ndoa. . . Siku ya 60 ya kufunga na kuomba, nikazidi kuchangangikiwa. Furaha na amani ya kufunga na kuomba ikapotea. Tony na mimi tukawa kama wageni ndani ya nyumba. . Hakula chakula nilichompikia kwa takribani wiki 6 sasa, nikajawa na hofu na uoga. Akawa ameanza kurudi nyumbani kwa kuchelewa na tukawa hatuongei tena. Kila nilipojaribu kumuongelesha aliniambia nifunge mdomo wangu hataki kunisikia. . Wote tulikuwa tukienda kazini na kurudi nyumbani lakini kila mtu alielekea chumbani kwake. Nilikuwa sijui hata nianzie wapi. Nilifahamu fika hakuna jambo baya nililolifanya, nilichokua nafanya ni chema kwa ajili ya ndoa yetu na nikashangaa kwanini Tony halioni hilo. . . Siku moja jioni nikiwa nimetangulia kufika nyumbani mida ya saa moja usiku nilipata text toka kwa Tony iliyoniumiza sana, text hiyo ilisema "Usinisubiri mimi, sitarudi nyumbani leo" Sikuamini macho yangu, na haraka haraka nikamjibu text iliyosema "Uko wapi? Kwanini hutarudi nyumbani?" . . Jibu lake lilinifanya nilie kilio kikubwa na uchungu mwingi.....oh ndoa yangu, masikini mimi kumbe sikujua!!!!... ITAENDELEA....... Share Jumaa mmaka Kipusa

at 12:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top