Home → simulizi
→ Nimeona ni vema ku-share na ninyi story hii ambayo itakua katika episode chache, songa nayo kuna mambo ya kujifunza.....
NDOA YANGU, NANI WA KUMLAUMU?
Episode 1
Kawe, Dar es salaam.
Baada ya kufuta meza ya chakula na kuosha vyombo, nilienda chumbani, sikujisumbua kusema usiku mwema kwa Antony ambae alikuwa sebuleni akiangalia fainali ya ligi ya mpira wa kikapu (NBA) kati ya Golden Warriors na Cleveland Cavaliers.
Nikijua lazima atakuja chumbani si muda mrefu, hivyo nlitaka akifika tu afikiri mimi nimeshalala muda mrefu. Haraka haraka nikaingia bafuni na kuoga kabla sijapanda kitandani. Nikahakikisha navaa suruali ndefu ili kusiwe na namna yeyote ya yeye ku-'access' mwili wangu.
Baada ya saa moja nikamsikia akipanda juu ya kitanda na kugeukia upande mwingine, kidogo nikashusha pumzi nliyoibana kwa muda mrefu. Nikafurahi kwa kuwa niliweza kukwepa kufanya tendo la ndoa usiku ule.
Asubuhi ile nilijua lazima tutakuwa na ugomvi tena, nikamuomba Mungu kimya kimya aniepushe na ugomvi. Mara nikahisi mikono yake ikinipapasa papasa mwili wangu. Nikawa sina shaka kabisa nini kinachohitajika na ni kipi kitatokea.
Nikafungua macho yangu na kutizama saa iliyopo ukutani. Ilikuwa saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi. Nikageuka na kuondoa mikono yake na kujaribu kuamka lakini akanivuta nisiamke. Kama mara tatu kila nikitaka kuamka ananivuta nibaki kitandani.
Mwishowe akasema; "Baby leo unayo sababu gani ya kuninyima haki yangu ya ndoa? Ni wiki mbili sasa for Christ sake. Unafikiri mimi nitakuwa na furaha kivipi kama unaninyima haki yangu ya ndoa?" Akasema hayo huku akionekana ameghafirika mno!!
"Unataka kuniambia furaha yako ni kufanya mapenzi tu? Kwa hiyo bado hujanielewa mwenzako? Nafanya hivi kwa ajili yetu. Kwa ajili ya ndoa yetu na kwa ajili ya kesho yetu.
Nilikwambia kabla sijaanza hivi kwamba haya yatakuja kutokea na tukakubaliana hutafanya hivyo na sasa hivi umenigeuka nionekane nina hatia. Seriously mimi unanichanganya!!" Nikamweleza hayo huku nami nikiwa nimekasirika!
Victoria, mimi sipingi wewe kufunga na kuomba. Nampenda Mungu pia na ninaenda kanisani lakini hauwezi ukategemea mimi nikae siku 100 bila haki yangu ya ndoa eti kwa vile upo kwenye maombi ya kufunga, hiyo haipo!!" Tony aliongea.
Nilikasirika mno baada ya kunieleza hayo, "seriously Tony? Unanitania? Hauwezi kujizuia? Hii inaonesha ni jinsi gani mume wangu umeanguka kiimani.
Sio wewe uliyekuwa ukifunga na kuomba na mimi kila mara kabla hatujaoana? Kwahiyo kipindi kile ulikua ukijifanyisha tu! Sio sisi tuliokaa kwenye uchumba miaka miwili bila ya kufanya ngono? Kwaio inamaanisha ulikua unanisaliti?
Nini? Unawezaje kusema hayo? Umechanganyikiwa ee? Unaweza vipi kufananisha kipindi kile na sasa hivi? Kipindi kile nilikuwa single sasa hivo nimeoa. Kuna maana gani ya mimi kuoa kama siwezi kupata haki yangu ya ndoa?
"Ahaa kwaio mimi ni sex machine? Ulinioa kwa sababu ya sex?" Nilimuuliza.
"Unajua nini, siwezi kupoteza muda wangu katika maongezi na wewe yasiyo na tija. Ninakuonya mara ya mwisho. Sitaki kusikia mambo yako ya kufunga na you will learn to respect me katika hii nyumba. Kama huu ndio upuuzi mnaofundishana huko kanisani, nitakuzuia kwenda tena shabàash"
"You wont dare Tony, usijaribu nakwambia. Kama ningeambiwa kuchagua wewe na Mungu wangu, wewe ungepoteza. Mungu kwanza wewe unafuata. Huyo shetani anaejaribu kukutumia..hatanikamata na mimi"
"Try me Vicky, nijaribu uone Vicky" akaongea huku akielekea bafuni na kufunga mlango. Nikatoka chumbani na kuelekea jikoni nikiwa nimeumia mno moyoni. Nikiwa ninaandaa kifungua kinywa nilikuwa nimejawa na huzuni mno, sikuelewa kwanini Tony alikuwa na hasira juu ya uhusiano wangu na Mungu. Sikutarajia kama mambo kama haya yangetokea ndani ya miezi 6 tu ya ndoa yetu.
Anafahamu fika ni jinsi gani ninavyompenda Mungu na ni kiasi gani uhusiano na Mungu una maana kwangu lakini hakuwa akinielewa. Na tuliongea haya wakati wa uchumba na alikuwa akiniambia ni kwa namna gani ananipenda kutokana na nilivyojitoa kumpenda Mungu.
Tumejaribu kutafuta mtoto kwa kwa miezi mitano sasa, na hakuna lolote lililotokea. Na ninafahamu fika inanibidi nikazane kumuomba Mungu kabla hiyo miezi mitano bila ya ujauzito isije kuwa miaka 15 bila ya mtoto. Na nikamwambia kabisa nataka kujiunga na maombi ya kufunga ya siku 100.
Mwanzoni alikubali kujiunga na mimi kwenye maombi ila baada ya siku tatu akaacha. Sikuhisi amenitenga mimi niliendelea mwenyewe, sikufikiri kama atakuwa mchungu kwangu katika jambo jema kama hili.
Baada ya kumaliza kuandaa kifungua kinywa ikiwa ni kama nusu saa tokea tuzozane alitoka chumbani akiwa ameshavaa vizuri suti iliyompendeza na akapitiliza moja kwa moja nje huju akinipita bila kunisemesha lolote.
Nikamkimbilia na kumshika mkono, kabla hajaingia kwenye gari yake. " Haujala kifungua kinywa nilichokuandalia" Nikamwambia..
"Nitolee upuuzi wako hapa, kifungua kinywa my foot!! Sitaki chakula chako sasa na mpaka utakapojifunza kuniheshimu kama mume wako na kichwa cha nyumba na pale utakapoona kipi ni cha muhimu kwako" akasema hayo huku akiingia ndani ya gari na kufunga mlango kwa nguvu, akawasha gari na kuondoka haraka, nikasimama pale huku nimepigwa na butwaa.
Tumekuwa na kutoelewana juu ya tendo la ndoa wiki ya pili sasa ila sijawahi kumuona Tony akiwa amekasirika kama leo hii. Nilijua kabisa nipo kwenye jaribio kubwa sana la ndoa yangu, nilitakiwa kuomba sana juu ya mume wangu...labda sikujua ni nini natakiwa kufanya kama mke! kwa kweli nilichoka..........
ITAENDELEA KESHO.........
Share series hii na wengine wafuatilie na kujifunza.
Crdts: Tund Onp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: