Home → simulizi
→ JAMANI BABA
Sehemu 02
ILIPOISHIA
“Asante , shikamoo, ” alisalimia Mwaija huku
akikaa kwenye kochi kwa adabu .
“Marahaba, za safari?”
“Nzuri .”
“Karibu sana, karibu mwanangu, ” alisema
Masalanda huku akimkazia macho Mwaija na
kumshangaza mkewe kwani uchangamfu
ulikuwa mkubwa tofauti na alivyofikiria.
SASA ENDELEA ...
“Asante sana . Naamini wewe ndiyo baba
mdogo?” aliuliza Mwaija .
“Hapana! Huyo ni baba yako , mambo ya baba
mdogo yanatoka wapi saa hizi hapa ?” alikuja juu
mama Mwaija .
“Sawa , baba!”
“Ni mimi mwanangu .”
Mwaija alifurahia mapokezi hayo kiasi kwamba
alijikuta akifurahi sana tofauti na alivyotaka
kuamini hasa baada ya kushuka stendi Ubungo.
Mwaija alioneshwa chumba chake cha kulala.
Akaingiza mizigo yake ndani , akakiangalia
chumba hicho kisha akakipenda sana.
***
Ilikuwa usiku wa manane, Masalanda aliamka na
kuanza kumuwaza Mwaija . Aliwaza tangu
alipomwona jioni ile akitoka Tanga ...
“Asante , shikamoo. ”
“Marahaba , za safari?”
“Nzuri .”
“Karibu sana, karibu mwanangu. ”
“Asante sana . Naamini wewe ndiyo baba
mdogo?”
Masalanda akazinduka kutoka kwenye mawazo
ya jioni, akasema mwenyewe moyoni . ..
“Anaonekana binti mchangamfu halafu ana akili
kichwani. Ana heshima zake f’ lani. Yale mavazi
ndiyo ya watoto wetu wa siku hizi. ”
Wakati Masalanda akiwaza hayo , mkewe
alishtuka na kugundua kuwa mumewe hakuwa
amelala. Akajua ana mawazo kwani anamjua
vizuri ...
“Baba Mwaija ,” aliita mama Mwaija kwa kutumia
jina la binti yake.
“Naam.”
“Nahisi kama una mawazo sana ?”
“Hapana. Sina mawazo .”
“Kama unayo niambie tu. Unajua binti yetu kaja
kama ulivyomuona mavazi yake , nilimwambia
yale si mavazi ya kuvaa humu ndani , akasema
atajirekebisha kwa hiyo tumvumilie kidogo mume
wangu.”
“Sijayashangaa mavazi mimi , mabinti wetu mjini
siku hizi ndivyo wanavyovaa , sidhani kama kuna
namna.”
“Sasa mawazo ni ya nini ?”
“Nawaza biashara zangu naona kama haziendi
sawasawa kama zamani .”
“Mungu atakusaidia mume wangu, biashara
ndivyo zilivyo , leo nzuri kesho ni mbaya sana .”
“Sawa , nashukuru pia kwa dua zako .”
***
Kule chumbani, Mwaija alikuwa akichati na jamaa
yake wa Tanga mjini anaitwa Seif Mabanda ya
Papa. Licha ya kwamba ilikuwa usiku lakini yeye
hakuona tabu ...
“Mwenzio nimekuja kwa mama Dar , sipo Tanga ,
hajakwambia Mwanakombo?”
“Sijasikia. Unarudi lini ?”
“Mh ! Sijui kama nitarudi tena huko . Mama
hataki.”
“Kwa hiyo ina maana umenimwaga?”
“Jamani sijakumwaga , siku mojamoja we njoo
huku Dar . ”
“Mi sijawahi kufika Dar itakuaje?”
“Mi nitakuelekeza.”
***
Asubuhi Masalanda aliomba kupikiwa chai ili
anywe kabla ya kwenda kwenye biashara zake. ..
“We Mwaija ,” aliita mama.
“Abee mama. ”
“Hebu mpikie chai baba yako sasa hivi .”
Chai ilipikwa ingawa mama Mwaija alishangaa
sana kwani haikuwa kawaida kwa mumewe
kunywa chai asubuhi pale nyumbani.
Baada ya dakika kumi na tano tu, chai ilipelekwa
mezani. Mwaija alibeba kwenye sinia akiwa
ndani ya kanga moja. ..
“Loo !” alihamaki moyoni Masalanda lakini
Mwaija hakusikia.
“Shikamoo baba.”
“Marhaba Mwaija , hujambo mwanangu ?”
“Sijambo baba sijui wewe umeamkaje?”
“Mimi mzima wa afya, nakuhofia wewe na
uchovu wa safari.”
“Nimeamka sawa baba .”
“Haya tumshukuru Mungu wetu. ”
“Ni kweli baba.”
Wakati Mwaija anaondoka, ‘mzigo’ nyuma
ulionekana unavyosumbuliwa na kutembea hasa
ikizingatiwa ile kanga moja tu na umbo la Mwaija
sasa!
“Hivi huyu binti ndiyo nini hivi ?” alijiuliza
Masalanda huku macho yake yakimtoka pima
wakati Mwaija anafuata maji ya kunawa .
“Chai tayari wewe?” mama mtu aliuliza kutokea
uani ambako alikuwa akifagia.. .
“Tayari mama.”
“Weka na maji kama nilivyokuelekeza kila kitu
jana usiku .”
“Sawa mama .”
Baada ya mumewe kuondoka ndipo mama
Mwaija alibaini kuwa , mumewe alikuwa
akihudumiwa huku binti yake akiwa ndani ya
kanga moko , ilimuuma sana!
“We Mwaija .”
“Abee .”
“Wakati unamhudumia baba yako chai ulivaa
hivyo?”
“Ndiyo mama .”
“Ha ! Ha ! Haaa ! Yaani kweli unavaa hivyo mbele
ya baba yako Mwaija ? Hebu jiangalie kwanza.
Ona! Hii mikalio yako ulitaka aione siyo?”
“Hapana mama , ila ... ”
“Ila nini ? Au unataka baba yako aingiwe na ibilisi
juu yako siyo ?” ITAENDELEAAA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: