JAMANI BABA Sehemu 03 ILIPOISHIA : “We Mwaija .” “Abee .” “Wakati unamhudumia baba yako chai ulivaa hivyo?” “Ndiyo mama .” “Ha ! Ha ! Haaa! Yaani kweli unavaa hivyo mbele ya baba yako Mwaija ? Hebu jiangalie kwanza. Ona! Hii mikalio yako ulitaka aione siyo?” “Hapana mama , ila .. .” “Ila nini ? Au unataka baba yako aingiwe na ibilisi juu yako siyo ?” TAMBAA NAYO ... “Hapana mama , mimi sikujua kama kwa kuvaa hivi baba anaweza kuingiwa na ibilisi .” “We hivyo ulivyovaa unaona ni sawa siyo?” “Ulivyoniambia ndiyo nimegundua si sawa sasa .” Mama alimwangalia bintiye kwa macho makali kwa karibu dakika moja nzima huku Mwaija naye akishindwa kuondoka na kusimama palepale.. . “Nisamehe mama.” “Usirudie tena, sawa ?” “Sawa mama .” “Haya , kaendelee na kazi zako .” *** Shughuli zilikuwa haziendi sawa kwa Masilinde. Kila baada ta muda alivuta picha ya Mwaija. .. “Yule binti, daa ! Ni shida kwelikweli. Au kuishi mbali na mama ndiyo kawa vile ? Sasa ni kuvaa gani vile mbele ya baba ’ake ?” *** Jioni Masilinde aliporudi nyumbani alimkuta Mwaija, mama yake alikwenda kudai pesa zake kwa watu aliowakopesha vitenge .. . “Shikamoo baba.” “Marhaba Mwaija , mzima ?” “Mi mzima baba, pole sana kwa kazi.” “Nimepoa . Mama yuko wapi?” aliuliza baba mtu huyo huku akikaa kwenye sofa... “Alisema anakwenda kudai madeni ya vitenge sijui.” “Ooo! Ni ile biashara yake.” “Nikupikie chakula baba?” “Hapana, kama kuna juisi naombeni. ” “Ipo ,” alisema Mwaija huku akienda kuifuata hiyo juisi... “Mh !” aliguna Masilinde akimwangalia Mwaija alivyovaa jioni hiyo. Alivaa gauni fupi , magoti yote yalikuwa nje huku miguu yenye umbile la chupa za bia ikionekana vizuri sana na kumfanya baba’ake azidi kung’ata ulimi . “Karibu juisi baba .” “Asante sana mama. ” Wakati Mwaija anaondoka kwenda kuendelea na shughuli zake , Masilinde alimtolea macho pima huku akitingisha kichwa . .. “We Mwaija .” “Abee baba .” “Njoo hapa. ” Mwaija alirudi haraka ... “Hebu kaa hapo .” Mwaija alikaa... “Hivi hizo nguo zako za ajabuajabu unazovaa hapa kwangu una maanisha nini? Nani kakwambia hapa ni hosteli ?” “Samahani baba, sikujua kama nitakukwaza .” Mara mama yake aliingia ... “Afadhali umekuja mama Mwaija ... ” “Nini tena ? Halafu wee Mwaija ...” Kabla mama’ake hajamaliza kusema, Masilinde aliendelea... “Nilikuwa namuonya mwanao na hivi viguo vyake... ” “Na ndiyo nilichotaka kumwambia na mimi . Asubuhi nimemsema sana, akabadili . Nashangaa saa hizi namkuta hivi tena. ” “Nisameheni sana.” “Tukusamehe kwani we mwenyewe huoni ? Kama utaendelea hivyo hapa nyumbani kwangu utahama haraka sana ,” alikuja juu Masilinde. “Na kweli utahama hapa. Nilishakwambia tangu unakuja kwamba hayo mavazi yako mimi sikubaliani nayo lakini nahisi kama hunielewi vile. ” “Nimewaelewa. ” “Haya kabadili haraka sana ,” alisema Masilinde. Mwaija alisimama kwenda kubadili nguo . Wakati anatembea macho ya Masilinde yalikuwa kwake huku akisema .. . “Unavaa viguo vya ajabuajabu kama hosteli !” Mwaija alianza kukata tamaa ya kuendelea kuishi kwenye nyumba ile kwani mavazi ya ajabu yanayopigwa vita ndiyo zake . Hakuwa na nguo ye heshima hata moja. “Sasa itabidi kila gauni nivae na kanga juu ,” alisema moyoni huku akilitungua gauni jingine na kulivaa, akatupia na kanga moja juu yake, akatoka... “Si hivyo sasa, ulikuwa unashindiwa nini tangu mwanzo?” alihoji Masilinde huku akiachia tabasamu pana ! Mwaija alipoona baba huyo anatabasamu na yeye akaachia la kwake, wakatabasamu wote ... “Hapo sasa unaonekana binti mzuri, uliyelelewa kwa maadili ya wazazi wako , si kama saa zile . “Asante baba .” Mwaija aliondoka kwenda nje . Wakati anakwenda macho ya Masilinde yakamsindikiza , akashtuka ... “Mamaaaa. ..kumbe ishu si viguo vifupi , ishu ni kwamba amejaaliwa makalio. Ona. ..eee . ..laaa!” alisema moyoni huku akisimama kumwangalia vizuri binti huyo . Japokuwa alivaa kanga juu ya gauni lakini wowowo lake lilionekana wazi na kutingisha kwa kadiri mguu mmoja ulipokuwa unakwenda mbele na kuacha mwingine nyuma. .. “Haiwezekani ! Hivi kweli mama yake ni huyu mke wangu au alipewa mwingine siku anajifungua?” Hapo mama Mwaija alikuwa chumbani kwake ... “We Mwaija ,” aliita Masilinde lakini kwa sauti ambayo kama hakutaka mkewe asikie kule chumbani. “Abee baba .” itaendeleaaa..

at 12:29 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top