Home → simulizi
→ RIWAYA:ROHO YA GIZA
🅱
SEHEMU YA TISA(09)
*****ILIPOISHIA******
hatimae akafanikiwa kutoka ndani ya shimo hilo,,, punde si punde akajitokeza yule kiongozi mkuu muwakilishi wa wafuasi wa Lucifer hapa duniani...
hakuna aliyeweza kumuona kwa macho ya kawaida!! akagusa kichwa cha mwanaume huyo... ghafla akili ya mwanaume huyo ikabadilika,,, akaingiwa na roho ya kikatiri.. akasimama haraka kisha akamtazama mke wa Fundikira kwa macho ya msisitizo kufanya jambo fulani..akazipiga hatua kadhaa akaifungua ile kamba pale kwenye mti,, akaifunga kitanzi akaishikilia kikakamavu.. . kisha akazipiga hatua kumfuata mke wa Fundikira!!
****ENDELEA****
mke wa Fundikira akaingiwa na hofu kupita kiasi,, akaona kuwa mtu huyo hana nia nzuri,, mtu huyo alipomkaribia mke wa Fundikira akamnasa na kumfunga kamba shingoni na kuanza kumnyonga!
wakati huo huo Fundikira katika pitapita zake kumtafuta mkewe akawa amefika eneo hilo akasikia sauti ya mwanamke akikoroma,,, aliposikiliza kwa makini sauti hiyo akahisi kuwa mwanamke huyo anahitaji msaada,, ingawa kwa wakati huo hakuweza kuitambua sauti hiyo,, akatimua mbio kuelekea kule inapotokeq sauti hiyo,,, alipoyltazama kwa makini akamuona mkewe akiwa anatapatapa kupigania pumzi huku akifanya jitihada za kujiokoa mwenyewe kwa nguvu zake zote... Fundikira akaokota jiwe na kumpiga kichwani yule mtu anayemnyonga mkewe kwa kamba!!
mtu huyo akadondoka chini na kupoteza fahamu, Fundikira akaifungua kamba hiyo shingoni kwa mkewe.. akafanikiwa kuokoa uhai wa mkewe,,
*************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa Fundikira,, alionekana mtoto wao akiwa amelala usingizi mzito pale juu ya kitanda... ajitokeza Lucifer ndani ya chumba hicho,, akazipiga hatua kukifuata kitanda hicho!! alipokikaribia,, akasita kufanya jambo lolote,, kwa sababu kulikuwa na biblia aliyoiacha Fundikira pale juu ya kitanda! Lucifer akakasirika kupita kiasi,, ni baada ya mpango wake kushindikana ,kumchukua mtoto huyo kumpeleka kuzimu! akatoweka kimiujiza.
wakati huohuo alionekana Fundikira na mkewe wakizipiga hatua kurudi nyumbani!
baada ya dakika kadhaa wakawa wamefika,, wakaingia ndani ya nyumba,, wakaelekea chumbani.. walipofika wakaanza kusali kisha wakapanda kitandani na kuutafuta usingizi.
************************
Asubuhi palipokucha walidamka salama lakini,, Fundikira akamwambia mkewe kuwa waende kwa mchungaji! mkewe hakuwa na kipingamizi akakubali wazo la mumewe! wakajiandaa kisha wakaelekea kwa mchungaji.. huku wakiwa na mtoto wao wa pekee!
walipofika Fundikira akasema ukweli wa mambo yote aliyoyafanya wakati anamtumikia Lucifer! mkewe akaanza kumuogopa Fundikira baada ya kumsikia akisema kuwa amefanya mauwaji ya watu wengi wasiokuwa na hatia,, akasema,,"hata mabucha mengi ya kuuza nyama huwa wanauza nyama za binadamu pasipo wao kujua,, hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kuona jambo hilo,,
mchungaji akaanzisha maombi maalumu kwa Toba,, Fundikira akatubu kwa imani..
kisha mchungaji akasema jumapili mje kanisani!.
siku zilizidi kusonga hatimae jumapili ikawadia,, wakajiandaa kwenda kanisani!!! wakati mke wa Fundikira yumo bafuni anaoga,, ghafla bomba likaanza kutoa damu badala ya maji! mke wa Fundikira akapiga kelele akatimua mbio kutoka bafuni! Fundikira akashtuka kumuona mkewe anapiga kelele! akauliza kwa mshangao mbona mwili wako umetapakaa damu? umepetwa na nini?
mkewe akashindwa kujibu kitu chochote akabaki anatetemeka kwa hofu iliyokuw imetanda juu yake!
Fundikira akaamua kwenda kule bafuni kushuhudia nini kimetokea... alipofungua mlango wa bafu akashtuka kuona damu nyingi zimetapakaa kwenye marumaru!! alipotazama kwa makini akaona matone ya damu yakitokea ndani ya bomba!! punde si punde ikasikika sauti ya mkewe akilia kwa sauti kali,,
Fundikira akatimua mbio kurudi chumbani..akastaajabu hakumkuta mkewe,, alipoangaza angaza macho yake akaona alama za nyayo za miguu iliyokanyaga damu ikitokea chumbani akazifuata nyayo hizo huku macho yake yakitazama kwa tahadhari! akaona alama za nyayo hizo zimeelekea kwenye kile chumba chake cha siri alichokuwa akikitumia kuwasiliana na Lucifer kuomba chochote anachokitaka! akausukuma ulenukuta ambao ni mlango wa kuingia ndani ya chumba hicho!! alipoingia upande wa ndani akakuta mkewe kapoteza fahamu huku kazungukwa na jopo la watu tisa waliovalia majoho marefu yenye rangi nyeusi,, Fundikira akapaza sauti akasema,, "muacheni mke wangu! mimi sihitaji tena kuendelea kuwa mwanachama wenu!
punde si punde akaonekana mmoja kati ya watu hao tisa akichomoa kisu na kuchuchumaa pale alipokuwa amelala mke wa Fundikira!
macho yakamtoka Fundikira!!! wazo likamjia kuwa arudi chumbani akachukue biblia akatimua mbio kukifuata chumba chake cha kulala,, ghafla akatereza na kudondoka chini akaangukia kisogo!! akatulia tuli!
wakati huo huo kule ndani ya kile chumba cha siri walionekana wale wafuasi wa Lucifer wakifanya ishara ya mikono yao.... kwa ajili ya kumchinja mke wa Fundikira!
ITAENDELEA.........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: