RIWAYA:ROHO YA GIZA SEHEMU YA KUMI(10) *****ILIPOISHIA****** "muacheni mke wangu! mimi sihitaji tena kuendelea kuwa mwanachama wenu! punde si punde akaonekana mmoja kati ya watu hao tisa akichomoa kisu na kuchuchumaa pale alipokuwa amelala mke wa Fundikira! macho yakamtoka Fundikira!!! wazo likamjia kuwa arudi chumbani akachukue biblia akatimua mbio kukifuata chumba chake cha kulala,, ghafla akatereza na kudondoka chini akaangukia kisogo!! akatulia tuli! wakati huo huo kule ndani ya kile chumba cha siri walionekana wale wafuasi wa Lucifer wakifanya ishara ya mikono yao.... kwa ajili ya kumchinja mke wa Fundikira! ****ENDELEA**** Wakati huo huo akaonekana Fundikira akinyanyuka kutoka pale chini alipokuwa amedondoka! akahisi maumivu makali kisogoni mwake,, akajaribu kukumbika nini kilimtokea mpaka yeye kudondoka chini,,kumbukumbu zikajia,,akakumbuka kuwa mkewe yupo kweny hatari lakini hana uwezo wa kuwazuia wale wafuasi wa lucifer zaidi ya kusali kwa imani,, Fundikira akatimua mbio kuelekea kwenye chumba chake,,akachukua biblia haraka,kisha akatimua mbio kukifuata kile chumba alichokuwemo mkewe,,akaingi akakuta yule mfuasi mmojawapo kati ya wale wafuasi wa Lucifer akiwa ameshikiria kile kisu kikiwa shingoni mwa mkewe! Fundikira akaanza kusali kwa kukemea huku kashikilia biblia,,punde si punde wale wafuasi wa Lucifer wakaanza kupiga mayowe,,wakiashilia maumivu makali kwenye miili yao,,yani wanaunguzwa kwa moto,,Fundikira hakusita kuendelea kusali kwa imani,,hatimae wakatoweka kimiujiza na kutokomea kusikojulikana! baada ya tukio hilo mke wa Fundikira akazinduka na kupata fahamu,akastaajabu kujikuta ndani ya chumba hicho akiwa uchi wa mnyama,akauliza kwa mshangao!,,"nini kimetokea? Fundikira akajibu,,"walitaka kukuchukua kwa kuchinja shingo yako! mke wa Fundikira akaingiwa na hofu kusikia maneno hayo,,akanyanyuka. kutoka hapo chini,, wakaongozana kuelekea chumbani,, wakamkuta mtoto wao kalala usingizizito pale juu ya kotanda! Fundikira na mkewe wakaanza kusali,,kisha wakapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! baada ya dakika kadhaa kupita wakasinzia,,, ilipofika majira ya saa moja za usiku,, wakashtuka kutoka usingizini,, wakastaajabu kuona wamelaal masaa mengi mfululizo! lakini cha kushangaza hawakumuona mtoto wao pale kitandani!! wakaingiwa na hofu,, Fundikira akatimua mnio kuelekea sebuleni! akamkuta mtoto wake akiwa kaketi kwenye sofa!! Fundikira akasita kumfuata mtoto huyo,, akaanza kusali kwa kukemea akihisi huenda ni mtego wa Lucifar,, kumbe mtoto huyo alidamka akaona wazazi wake bado wamelalal akaamua kutoka ndani ya chumba na kuelekea sebuleni! Baada ya kumaliza kusali,, Fundikira akazipiga hatua kumfuata mtoto wake akamgusa,, akagundua kuwa hakuna jambo lolote baya mbele yao! akaonekana mkewe akizipiga hatua kuja sebuleni,,kisha akaelekea jikoni kuandaa chakula angalau wapate mlo. baada ya nusu saa chakula kikaiva wakaanza kula.. walipomaliza wakarudi chumbani hukunwameongozana na mtoto wao,,,wakapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi! ************************* Asubuhi palipokucha,, Fundikira akadamka mapema akamuamsha mkewe, kisha akasema,,"yatupasa twende kule kanisani kwa mchungaji,,Mke wa Fundikira akadamka na kuandaa chai haraka.. kisha akamuandaa myoto wake kwa kumuogesha! baada ya dakika kadhaa kupita wakanywa chai na kuondoka zao. iliwalazimu kutembea kwa miguu kwa sababu,, gari alilokuwa analitumoa Fundikira katika matembezi yake lilichukuliwa na Lucifer kimiujiza kwa mara ya pili,, walitembea mwendo wa dakika nyinginkiasi,, wakawa wamefika kanisani kwa mchungaji, alex,, wakaingia ndani ya kanisa wakamkuta mchungaji akiendelea kupanga vitu vilivyomo ndani ya kanisa vikae katika mpangilio.... mchungaji akafurahi sana kumuona Fundikira pamoja na familia yake kuja kanisani hapo,, akawakaribisha kisha wakaanzisha maombi ya muda mfupi,, baada ya kumaliza maombi, mchungaji akasema,, "mbona jana hamkuja kanisani kwenye misa takatifu! Fundikira akaanza kueleza kilichotokea siku ya jana! mchungaji akaingiwa na roho ya huruma kisha akasema,, "yawapasa mumrudie Mungu,, atawaonyesha njia sahihi pia atawaondolea mateso na misukosuko,, Fundikira na mkewe wakakubali kumchamungu kwa imani na matendo,, ****BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA*** maisha ya Fundikira yakabadilika,, familia yake ikaishi kwa amani pasipo misukosuko,,Fundikira akawa mmoja kati ya viongozi wa kanisa hilo,, hatimae akawa mchungaji na kuanzisha kanisa lake,,, akapata waumini wengi sana,, kwa sababu,, alisimaam kiimani. kitendo hicho kilimchukiza sana Lucifer akaamua kuandaa mpango wa Fundikira kumtumikia yeye kwa namna nyingine... siku moja majira ya mchana Fundikira akiwa njianinkuelekea kwenye kanisa lake kwa ajili ya ibaada takatifu,, ghafla simu yake ikaita,, alipoitazama akaona namba ngeni ambazo sizo za kawaida,, namba hizo zilisomeka 666, Fundikira akashtuka kuona namba hizo akakata simu hiyo kisha akaanza kusali kwa kukemea,, punde si punde simu ikaita tena! akaamua kuika kisha akazima simu yake,, akaendelea na safari yake ya kuelekea kanisani kwake,, baada ya mwendo wa dakika kadhaa simu yake ikaita tena!! akashtuka! akajisemea moyoni,, "mbona simu yangu nimeizima!? yawezekanaje inaita? akaamua kuizima kwa mara nyingine tena, akaendelea na safari yake, ************************ Upande mwingine kule kuzimu alionekana Lucifer,, akiandaa mpango kabambe wa kumrudisha Fundikira awe mfuasi wake,,,akaandaliwa mwanamke ambaye atakuwa maalu kumteka Kifikr la Fundikira! mwanamke huyo akatumwa duniani siku ya leo kwenda kufunya jitihada za kumnasa Fundikira kiimani na kimatendo ilimradi airudie kazi ya kumtumikia Lucifer ,,kwa, kuwasha wayu waache kumuabudu Mungu wamuabudu Lucifer. ************************* wakati huohuo,, alionekana Fundikira akiingia ndani ya kanisa lake,, baada ya sekunde kadhaa akaonekana mwanamke mrembo kupita kiasi! wanamke huyo alikuwa na tumbo dogo,, na nyonga pana, kavalia gauni lililokuwa limeshikilia vyema mwili wake na kuonyesha umbo lwke la kuvutia,, mwanamke huyo akaingia ndani ya kanisa huku kashikilia kitabu kilichoonekana kuwa na kurasa nyingi,, kikafanana na biblia, akizipiga hatua mpaka kule mbele alipokuwepo Fundikira,, Fundikira akastaajabu kumuona mwanamke huyo,, akamkaribisha kisha akamuuliza kwa ukarimu,, "nikusaidie nini dada? mwanamke huyo akasema,, "nimekuja kwa ajili ya maombezi,, mimi jina langu naitwa SEVE ninatatizo la kushika mimba,, mpaka sasa sijawai kushika ujauzito kwa kipindi cha miaka tisa..naomba msaada wako,, Fundikira akamtazama mwanamke huyo kwa macho ya huruma,, kisha akasema,, imani yako ndiyo itakayokuponya,, yakupasa umtumainie Mungu pekee,, atakuponya,, hakuna kinachoshindikana mbele yake kwa yeyote atakaye muita,, naye ataitika kwa kujibu maombi yako!. Fundikira akastaajabu kumuona mwanamke huyo akirudi nyuma hatua chache,, ni baada ya kutaja jini MUNGU!(GOD). Fundikira hakujali akahisi huenda mwanamke huyo anajiandaa kupiga magoti kwa ajili ya maombi! bila kuchelewa maomni yakaanza! Fundikira akafumba mqcho huku akisali kwa imani,, akimuomba Mungu afungue uzazi wa mwanamke huyo,,, akiwa katikati ya maombezi,, ghafla mwanamke huyo akaanza kuvua nguo,, akabaki uchi wa mnyama kama alivyozaliwa! akazipiga hatua kumeogelea Fundikira! akaanza kumpapasa nyeti zake! Fundikira hakusita kuendelea kusali! lakini kila akimtaja Mungu mwanamke huyo anatetemeka huku akirudi nyuma!! lakini hakukoma,, akaendelea kufanya kazi aliyotumwa na Lucifer!.. punde si punde Fundikira akajikuta anaingiwa na tamaa,, mwili wa Fundikira ukaingiwa na hisia za kutaka kujaamiana na mwanamke huyo! pasipokujitambua kuwa ni mtego wa Lucifer! akaacha kusali akaiweka biblia kando,, alipofumbua macho akamuona mwanamke huyo yupo uchi wa mnyama! TAHARUKI!!!! ITAENDELEA.........

at 3:32 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top