Home → simulizi
→ RIWAYA:ROHO YA GIZA
👺👺👺👺👺👺👺👺
SEHEMU YA (11)
*****ILIPOISHIA******
akiwa katikati ya maombezi,, ghafla mwanamke huyo akaanza kuvua nguo,, akabaki uchi wa mnyama kama alivyozaliwa! akazipiga hatua kumeogelea Fundikira! akaanza kumpapasa nyeti zake! Fundikira hakusita kuendelea kusali! lakini kila akimtaja Mungu mwanamke huyo anatetemeka huku akirudi nyuma!! lakini hakukoma,, akaendelea kufanya kazi aliyotumwa na Lucifer!.. punde si punde Fundikira akajikuta anaingiwa na tamaa,, mwili wa Fundikira ukaingiwa na hisia za kutaka kujaamiana na mwanamke huyo! pasipokujitambua kuwa ni mtego wa Lucifer! akaacha kusali akaiweka biblia kando,, alipofumbua macho akamuona mwanamke huyo yupo uchi wa mnyama!
TAHARUKI!!!!
******TAENDELEA*****
Fundikira akaanza kuingiwa na hisia za kuibanjua amri ya sita..akaanza kumpapasa mwanamke huyo,,akambeba na kumlaza juu ya meza anayoitumia kuwekea baadhi ya vitu vidogo vidogo, Fundikira akaanza kuvua suruali yake,,punde si punde zikasikika sauti za nafsi mbili...nafsi moja ikimwambia asisite aendelee kufanya kitendo hicho...wakati huohuo nafsi nyingine ikimkataza asifanye kitendo hicho,,nafwi hiyo ikamwambia,, "huyu si binadamu wa kawaida bali ni pepo,, mshinde shetani.
Fundikira akabaki mdomo wazi pasipokujijua nini anafanya...akaacha kuvua suruali yake..akaivaa haraka na kufunga mkanda...kisha akazipiga hatua kurudi nyuma huku akimtazama mwanamke huyo kwa macho ya mshangao!
mwanamke huyo akashtuka! akanyanyuka kutoka juu ya meza akazipiga hatua za taratibu,,huku akijipapasa maziwa yake kwa kuyabinyabinya! Fundikira aliendelea kumtazama mwanamke huyo,,, kuanzia kwenye kiuno kushuka chini,,
mwanamke huyo aliendelea kuzipiga hatua kwa madaha,,huku akipinda nyonga zake, kutokqna na umbile lenye mvuto alilokuwanalo mwanamke huyo.
Fundikira akajikuta anameza mafundo ya mate huku akijiramba midomo yake!
wakati mwanamke huyo anazipiga hatua,,,ghafla akaikanyaga ile biblia iliyokuwa pale chini kwenye sakafu! punde si punde akaanza kupiga kelele,,kwa kihisi maumivu makali ya moto ukichoma mwili wake,
macho yakamtoka Fundikira,,akamtazama mwanamke huyo kwa makini,,,alipotazama miguu ya mwanamke huyo,,akaona mguu mmoja wa mwanamke huyo umekanyaga biblia! Fundikira akashtuka! akajisemea moyoni,,"bila shaka huyu ni pepo..
bilq kuchelewa Fundikira akajisafisha kwanza mwili wake kwa kutubu dhambi aliyoitenda pasipokukusudia,,,akamuomba Mungu kwa imani amuondolee majaribu hayo..kishaakaanza kusali kwa kukemea, mwanamke huyo akaanza kupiga kelele mfululizo,ghafla akaanza kuwaka moto kama kamwagiwa mafuta!
akaungua na kuteketea papohapo , ukawa ndio mwisho wa mwanamke huyo.
*************************
Upande mwingine kule kuzimu,, alionekana Lucifer akitazama tukio zima linaloendelea ndani ya kanisa la Fundikira....kitendo hiyo lilimkasirisha sana Lucifer...akaamua kuandaa mpango mwingine kabambe.....akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer...kisha akasema,,"nakupa kazi na uifanye siku ya leo kabla mwezi haujaandama..... mke wa Fundikira auwawe kisha niletee kichwa chake.
Kiongozi mkuu akatii amri ya Lucifer..akasujudu miguuji mwa Lucifer....punde si punde Lucifer akatoweka kimiujiza kurudi kuzimu.
ilipofika saa moja za usiku...kiongozi mkuu akaitisha mkutano wa dharura,,akateuwa wafuasi wawili,,waende kupandikiza chuki,,kwa raisi wa nchi,,aamuru makanisa yote yaliyofunguliwa na watu binafsi yachomwe moto. na atakayekiuka auwawe.
bila kuchelewa wafuasi hao wawili wakatoweka kimiujiza.
***************************
Upande mwingine,,alionekana Raisi akiwa katika,jengo kubwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akilihutubia taifa kupitia vyombo vya habari... pumde si pumde wakajitokeza kimiujiza wale wafuasi wawili....mmoja kati ya wafuasi hao akagusa kichwa cha raisi..ghafla raisi akasita kuongea,, akabaki kimya kwa sekunde kadhaa,,,akapoteza kumbukumbu kichani mwake,,akawa hakumbuki alikuwa anaongea kuhusu jambo gani! akawatazama waandishi wa habari kwa macho ya msisitizo,,uso wa raisi ukabadilika,,hata ule muonekano wa tabasamu ukatoweka,,akaweka sura ya kusisitiza jambo fulani!! kisha akasema,,"natoa tamko na lifanyiwe kazi kabla hapajakucha,,makanisa yote yaliyofunguliwa na watu binafsi yachomwe moto,,na atakayejaribu kupiga au kuzuia agizo hili auwawe kwa kukatwa kichwa papohapo....
alipomaliza kuongea maneno hayo,,akasema,,"mkutano umekwisha mwaweza kwenda.
waandishi wa habari wakabaki na mshangao, huku wakitazamana nyuso zao....
wakati huohuo...huko mitaani,, kauli ya raisi ilileta gumzo kwa wananchi..wakabaki wakijiuliza raisi kapatwa na nini!? kwa nini katoa maamuzi magumu kiasi hiyo...vikiwemo vitisho vya mauwaji!
bila kuchelewa maaskari wakavamia mitaa kutafuta makanisa ya watu binafsi....makanisa mengi yakachomwa moto.
*************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa Fundikira,alionekana Fundikira akizipiga hatua za haraka kutoka nje ya nyumba yake...ni baada ya kusikia agizo la raisi kupitia Runinga yake.
taarifa hiyo ilimfanya Fundikira achanganyikiwe,,,alitembea huku akiongea peke yake na kumlaumu raisi kwa maamuzi hayo!
Mke wa Fundikira akaamua kumfuata mumewe kwa sababu alijua kuwa Fundikira hawezi kukubali..kanisa lake lichomwe moto....hivyo atauwawa na maaskari walioagizwa na raisi...kanisa halikuwa mbali kutoka nyumbani kwa Fundikira.. baada ya dakika kadhaa akawa amefika kwenye kanisa hilo..akawakuta maaskari wakilimwagia kanisa hilo mafuta aina ya petroli.
Fundikira akapaza sauti akiwasisitiza wasichome nyumba ya kumuabudu Mungu.. lakini maaskari hao hawakumsikiliza Fundikira hatimae wakamaliza kulimwagia mafuta kanisa hilo..akaonekana askari mmoja akiwa ameshikilia kiberiti..akilisogelea kanisa hilo alichome moto...Fundikira akaruka kama kipa.....kujirusha ule upande alipokuwepo askari huyo,,wakadodoka chini,,maaskari wakaanza kumshushia Fundikira kipigo kikali!
mke wa Fundikira akatimua mbio kuja kuwazuia maaskari hao wasiendelee kumpiga mumewe...ghafla mkuu wa maaskari hao akachukua bunduki kutoka mikononi mwa askari mwingine...akachomoa singe iliyokuwa mbele ya bunduki hiyo...kisha akamsogelea mke wa Fundikira! kutekeleza amri ya raisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: