RIWAYA:ROHO YA GIZA SEHEMU YA NANE(08) *****ILIPOISHIA****** wakati huo huo sauti nyingine inamwambia aendelee kusali,,kuwa huyo si mtoto bali ni pepo! Fundikira akahisi kuchanganyikiwa!! akajisemea moyoni,,"haa!! inamaana nikiendelea kusali nitamuuwa mwanangu?? mbona sielewi!!kutokana na upendo kwa mtoto wake wa pekee Fundikira akajikuta anaanza kupoteza imani!!! akaacha kusali ilimradi mwanae asije kifa kwa maombi!!! akaitoa mikono yake kifuani,, iliyokuwa imekumbatia biblia,,,,huku akimtazama mwanae kwa macho ya uwoga wa hali ya juu.. kwa sababu mtoto huyo alibadilika akawa anasura ya kutisha pia ngozi yake ilikuwa inatisha!!!! fundikira akajikuta anaitupa biblia kando!!! PATASHIKA! *****ENDELEA**** Jasho likamtoka mfululizo hofu ikazidi kuongezeka juu yake,,akazipiga hatua za uwoga kurudi nyuma,,,punde si punde ikasikika sauti ya roho ya giza ikimwambia safi umefanya kazi nzuri,,,usiogope wala usikimbie,,sauti hiyo ilisikika ikijirudia rudia kwenye masikio ya Fundikira ,,,akaufungua mlango na kutimua mbio kutoka ndani ya chumba hicho,,mtoto wa Fundikira aliendea kuzipiga hatua kuufuata mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho...akaikanyaga biblia,punde si punde ukazuka moto mkali,,ukaanza kumuunguza mtoto huyo,,akapiga kelele lakini sauti ya mtoto huyo ilikuwa inatisha, punde si punde akaonekana kiumbe wa ajabu akitokea ndani ya mwili wa mtoto huyo,,kiumbe huyo alikuwa na vichwa tisa na mikono tisa...akatoweka kimiujiza !! mtoto wa Fundikira akanyanyuka na kujishangaa,,, ************************** kule sebuleni alionekana Fundikira akiwa anataka kutoka nje ya mlango,,,ikasikika sauti ya mtoto wake ikiita kutokea kule chumbani,,Fundikira akasita kutoka nje ya nyumba yake,, akajisemea moyoni,, "mbona sielewi,, hivi hiyo ni sauti ya mtoto wangu!!? akazipiga tua kukifuata chumba chake huku macho yake yakitazama kwa tahadhari... akaingia ndani ya chumba chake akamkuta mtoto wake kasimama kando ya kitanda! alipoangaza angaza macho yake akaona ile biblia iko chini akaichukua haraka kisha akamsogelea mtoto wake huku akimtazama kwa macho ya mshangao! Baada ya dakika kadhaa kupita,, Fundikira akaanza kusali kwa imani!! akimuomba Mungu amlinde yeye na familia yake,, *********************** Upande mwingine alionekana Lucifer,,, akiwa kule kumzimu,,, akamuita kiongozi mkuu muwakilishi wa wafuasi wake duniani!! akasema,,,huyu mtu ni tatizo,, na kama akiendelea kubaki hai,, tutapoteza wanachama,, sass basi natoa amri,, lazima auwawe na endapo itashindikana basi uhai wako ni halali yangu! kiongozi mkuu akatii amri ya Lucifer akatoweka kimiujiza kurudi duniani! **************************** Upande mwingine alionekana mke wa Fundikira akiendelea kutimua mbio pasipokujua ni wapi anaelekea, alikimbia umbali,giza lilikuwa totoro,,,akajikuta anatumbukia ndani ya shimo lililokuwa wazi,,shimo hilo lilikuwa refu na maji yenye kina kirefu kiasi,,, akapiga kelele kuomba msaada lakini hapakuwa na mtu yeyote eneo hilo,,, akajitahidi kufanya jitihada za kuokoa uhai wake,, punde si punde akahisi ameshikwa mguu wake mmoja anavutwa kuelekea chini ya maji hayo! hofu ikazidi kuongezeka,, akaanza kupiga kelele,, wazo likamjia kuwa asali kwa imani,, bila kuchelewa akaanza kumtaja Mungu bila kuchoka huku akisali,, mara ghafla akahisi kaachiliwa mguu wake... Upande mwingine alione manaume mmoja akiwa anaendesha pikipiki akapita kwenye lile eneo ambalo,,lipo lile shimo alilodumbukia mke wa Fundikira akasikia sauti ya mwanamke akipiga kelele za kuomba msaada,, mwanaume huyo akaingiwa na roho ya huruma akaamua kusimamisha pikipiki yake,, akashuka na lil fuata shimo hilo! akamulika kwa kutumia tochi ya simu yake! akamuona mwanamke yumo ndani ya shimo hilo! akasema,, "ondoa wasiwasi dada yangu.. wacha niangalie uwezekano wa kukutoa ndani ya shimo hili.. ********************* Kule nyumbani kwa Fundikira alionekana akimaliza. kusali... kisha akamsogelea mtoto wake na kumkumbatia.... ghafla wazo likamjia kuwa mkewe alikimbia,, akajisemea moyoni,, "sijui yuhali gani huko aliko!!? wacha nikamtafute usiku huu huu asije kupatwa na tatizo!!! Fundikira akamlaza mtot wake kitandani.. alipohakikisha kuwa kalala usingizi.. akatoka nje ya nyumba yake kwenda kumtafuta mkewe.. huko. mitaani. wakati huo huo kule katika lile eneo alilokuwepo mke wa Fundikira alionekana mwanaume huyo akitafakari jinsi ya kumsaidia mwanamke huyo kumtoa ndani ya shimo hilo... akakumbuka kuwa nyuma ya kiti cha pikipiki yake,,, kuna kamba ndefu ambazo alizinunu mchana wa leo kwa ajili ya mifugo yake kadhaa kule nyumbani kwake....akachukua kamba hizo akaziunganisha kwa kuzifunga... ikapatikana kamba moja yenye urefu wa kutosha kufika ndani kabisa ya shimo hilo... mke wa Fundikira akaishika kamba hiyo na kujifunga kiunoni,,, pia akaishikilia kwa nguvu.. yule mwanaume akaifunga kamba hiyo kwenye mti uliokuwa kando ya shimo hilo akaanza kuvuta kamba huku mke wa Fundikira akikanyaga kingo za shimo hilo... hatimae akafanikiwa kutoka ndani ya shimo hilo,,, punde si punde akajitokeza yule kiongozi mkuu muwakilishi wa wafuasi wa Lucifer hapa duniani... hakuna aliyeweza kumuona kwa macho ya kawaida!! akagusa kichwa cha mwanaume huyo... ghafla akili ya mwanaume huyo ikabadilika,,, akaingiwa na roho ya kikatiri.. akasimama haraka kisha akamtazama mke wa Fundikira kwa macho ya msisitizo kufanya jambo fulani..akazipiga hatua kadhaa akaifungua ile kamba pale kwenye mti,, akaifunga kitanzi akaishikilia kikakamavu.. . kisha akazipiga hatua kumfuata mke wa Fundikira!! ITAENDELEA.........

at 3:32 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top