Home → simulizi
→ RIWAYA:ROHO YA GIZA
SEHEMU YA SABA(07)
*****ILIPOISHIA******
wakati huo Fundikila alikuwa sebuleni,,ameshikilia kitabu kitakatifu anasali kwa imani.... akiwa katikati ya maombi,,,, punde si punde ikasikika sauti ya mkewe akipiga kelele kule chumbani.... wakati huohuo mtoto pia akaanza kulia kwa sauti kali!
TAHARUKI!!!!!
*****ENDELEA*****
Fundikira akashtuka,, akasita kuendelea kusali akanyanyuka,,akatimua mbio,, kielekea chumbani,, akamkuta mkewe anatokwa na damu puani masikioni na mdomoni!! punde si punde mtoto akafumba macho,,akatulia tuli! Fundikila akaanza kusali kwa imani huku,,amegusa mwili wa mke wake!!! Kumbe Fundikira aliondolewa ngivu za kimiujiza na Lucifer baada ya kujitoa kwenye chama cha kumuabudu Lucifer!
Hivyo Fundikira hakuweza kuwaona wale wanachama watano waliotumwa na Lucifer kuja kuiangamiza familia yake!
Fundikira akaendelea kusali kwa imani,, punde si punde wale wanachama wa Lucifer wakaanza kuhisi wanaungua miili yao!! wakaanza kupiga kelele na kujionyesha mbele ya macho ya fundikira!
Fundikira akashtuka kuona mmoja kati yao ameshikilia bakuli kubwa likiwa na damu ndani yake! kumbe damu iliyokuwa inatoka puani masikioni na mdomoni mwa mke wa Fundikira,, ilitolewa kimiujiza kwa lengo la kuchukua damu hiyo kwa ajili ya kitoweo cha siku hiyo.. ilimradi mke wa Fundikira apoteze maisha?
Fundikira hakusita kuendelea kusali,, alizidi kisali kwa kukemea nguvu za giza?!
hatimae wale wanachama wakawaka moto na kuteketea,, ukawa ndio mwisho wa ihai wao... ghafla lile bakuli lililokuwa na damu ndani yake... likapasuka vipande vipande! na damu iliyokuwa ndani ya bakuli hilo ikatoweka kimiujiza na kurudi mwini mwa mke wa Fundikira!
*****************************************
Upande mwingine kule kuzimu,, alionekana Lucifer,, akiwa anapiga kelele kwa sauti lali!! kelele hizo ziliambatana na mngurumo mkubwa... pamoja na radi za mfululizo!
akiashiria kuwa kakasilishwa na kitendo cha Fundikila kusababisha wafuasi wake watano kuadhibiwa na Mungu! kwa imani yake kali?
Lucifer akaandaa mpango wa kuangamiza watu mia tano, usiku huo
iwe kama fidia ya wale wafuasi wake watano walioangamia kwa moto!
Akamuamuru kiongozi mkuu wa wafuasi wake,, hapa duniani.. ateuwe baadhi ya wanachama waende kuangamiza watu mia tano!
nila kuchelewa kiomgozi mkuu akateuwa wanachama kumi.. wasambae sehemu mbalimbali za mitaa kuangamiza watu!
wanachama hao kumi wakatoweka kimiujiza kila mmoja akaelekea upande wake!
**********************************
Wakati huohuo! kule nyumnani kwa fundikira alionekana,, mkewe akizinduka na kupata fahamu!!! akauliza kwa mshangao,, "mbona nipo hapa chini!!? nini kimetokea!?
Fundikira akasita kuongea jambo lolote, akavuta pumzi kwa sekunde kadhaa kisha akasema,,"ulidondoka chini! ukapoteza fahamu!!! lakini ukweli ni kwamba walikuja!
Fundikira Aliongea hivyo kisha akabaki kimya!
mkewe akauliza,, "umesema walikuja? akina nani hao?
Fundikira akaanza kueleza ukweli wa mamno yaliyotokea,,.
Kabla hajamaliza kusimulia,, ghafla mtoto akashtuka kutoka usingizini,, akafumbua macho!! kosha ikasikika sauti ikitoka kwenye kinywa cha mtoto huyo!
Haya yote umesababisha wewe!! na siwezi kukuacha ukiwa hai!
Fundikira pamoja na mkewe wakaingiwa na hofu!! macho yakawatoka! wakabaki wanatazamama! ghafla ikasikika sauti ya kicheko chenye sauti ya kutisha ikitokea kinywani mwa mtoto wao!
kisha mtoto huyo akaanza kubadilika rangi ya ngozi yake,,, akawa mweusi kama mkaa!! akaota meno marefu yenye ncha kali! akanyanyuka kutoka kitandani ma kuwafuata wazazi wake!! mke wa Fundikira akanyanyuka haraka akatimua mbio kutoka ndani ya chumba na kuelekea sebuleni! Fundikira akabaki chumbani akaikumbatia biblia na kuanza kusali kwa imani!
wakati anasali,,Lucifer akajitokeza kimiujiza kuja kumdhuru fundikira,, punde si punde akajitokeza malaika akiwa kashikilia upanga,, kumlinda Fundikira!! Lucifer akasita kufanya jambo alilokuwa amelusudia!!! wakati huo Fundikila hakuweza kuona chochote kinachoendelea,, zaidi ya kumuona mtoto wake akizipiga hatua za taratibu kumfuata hapo aliposimama!!! ghafla zikasikika sauti mbili tofauti.. masikioni mwake,, zikimgombania Sauti moja ikimshawishi atupe biblia kando kuwa asipofanya hivyo atamuangamiza mtoto wake wa damu kwa maombi!!! wakati huo huo sauti nyingine inamwambia aendelee kusali,,kuwa huyo si mtoto bali ni pepo!
Fundikira akahisi kuchanganyikiwa!! akajisemea moyoni,,"haa!! inamaana nikiendelea kusali nitamuuwa mwanangu??
mbona sielewi!!kutokana na upendo kwa mtoto wake wa pekee Fundikira akajikuta anaanza kupoteza imani!!! akaacha kusali ilimradi mwanae asije kifa kwa maombi!!! akaitoa mikono yake kifuani,, iliyokuwa imekumbatia biblia,,,,huku akimtazama mwanae kwa macho ya uwoga wa hali ya juu.. kwa sababu mtoto huyo alibadilika akawa anasura ya kutisha pia ngozi yake ilikuwa inatisha!!!! fundikira akajikuta anaitupa biblia kando!!!
PATASHIKA!
ITAENDELEA.........
wingi wa like zenu ndizo zitasababisha niirushe hadithi hii mapema kwa sababu ni ya bure.. zawadi kwa mashabiki wa riwaya zangu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: