Home → simulizi
→ RIWAYA:ROHO YA GIZA
🅱 professional love
SEHEMU YA TANO(05)
*****ILIPOISHIA******
baada ya Lucifer kuongea maneno hayo akatoweka kimiujiza na wale wafuasi wake wakatoweka muda huohuo..
mke wa Fundikila hakuwa na uwendo wa kuona yale yote yaliyotendeka muda mchache uliopita!
.sasahivi ile hali ya joto kali mwilini mwake ilitoweka!
Fundikila akatimua mbio kumfuata mkewe akaanza kumkagua kama kaumizwa na wale wafuasi wa Lucifer!
alipogusa mwili wa mke wake,, Fundikila akaanza kutokwa na damu kwenye kucha za mikono yake! wakati anatahamaki...akahisi maumivu makali kwenye paji la uso..punde si punde akadondoka chini akapoteza fahamu!!
******ENDELEA*******
mkewe akaingiwa na hofu kupita kiasi akaingiwa na hofu baada ya kumuona Fundikila kadondoka chini huku anatokwa na damu kwenye vidole sehemu ya kucha zote za mikononi!
akamsogelea mumewe huku akionekana kuwa katika hali ya uwoga wa hali ya juu..kabla hajamkaribia..ukasikika mngurumo wa kutisha ukitokea ndani ya nyumba..mke wa Fundikila akaamua kwenda kushuhudia nini kimetokea huko ndani ya nyumba!akazipiga hatua za kunyatia akaufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba,,,macho yakamtoka baada ya kuona kila kitu kimebadilika ndani ya nyumba panaonekana kutisha!
wakati huohuo alionekana mwanaume moja akizipiga hatua kulifuata geti la nyumba ya fundikila akagonga geti hilo kwa mfululizo...mke wa Fundikila akatimua mbio kwenda kufungua mlango,,,akashtuka kumuona mtu ambaye hakuwahi kumuona machoni mwake,,,
punde si punde Fundikila akazinguka fahamu zikarejea!..wakati mke wa Fundikila akiwa bado anamshangaa mgeni aliyegonga geti....ikasikika sauti ya Fundikila akimuita mkewe..mke wa Fundikila akashtuka! akageuza shingo yake kumtazama mumewe,,,akamuona amenyanyuka kutoka pale chini alipokuwa amedondoka na kupoteza fahamu....
wakati huo huo akageuza shingo kumtazama yule mtu aliyekuwa anagonga geti! hakumuona tena wala hakujua mtu huyo kaenda wapi!
akataka kutimua mbio ,,
Fundikila akasema,,usikimbie mke wangu.......maneno hayo ya fundikila yalimfanya mkewe apunguze waasiwasi uliokuwa umeetawala kichwani mwake.
akazipiga hattua kumfuata mumewe huku akimtazama kwa macho ya uwoga!Fundikila akasema twende ndani nitakusimulia kila kitu utajua ukweli wa haya mambo....
wakaongozana kuingia ndani ya nyumba lakini mke wa Fundikila alikuwa na hofu kuhusu yale aliyoyaona ndani ya nyumba...hivyo akatembea nyuma ya Fundikila!
walipoingia ndani ya nyumba mke wa Fundikila akastaajabu kuona muonekano wa ndani umerudi kama kawaida na ule muonekano wa kutisha ukatoweka!
sebule ilibaki tupu pasipokuwa na kitu chochote!, Fundikila akasema,,"kuna jambo nataka nikueleze,,,nilifanya siri hii kwa miaka mingi,,mke wa Fundikila akasema,," siri gani hiyo mbona unanitisha?
Fundikila akasita kuongea akakumbuka kuwa aliambiwa asitoe siri hiyo kwa kipindi cha uhai wake wote!
mkewe akabiki akimkodolea macho mumewe,,alipoona Fundikila kabaki kimya ,akaamua kuuliza,,"mbona upo kimya? pia mbona usemi hilo jambo?
Fundikila akanyanyuka akamtazama mkewe kwa macho yamsisitizo kisha akasema,,"usijali nitakueleza siku nyingine.
aliongea mneno hayo huku akizipiga kukifuata chumba chake cha kulala....
pia mkewe hakutaka kubaki hapo sebuleni peke yake akaamua kumfuata mumewe hukohuko chumbani.
**********************************
siku zilizidi kusonga,,hali ya maisha yao ikawa tete! mali za Fundikila zilitoweka kimiujiza kila kukicha,,
akawa hana pesa ya kumuhudumia mke wake...
siku moja akiwa matembezini,,alitafakari nini cha kufanya,,akajishauri aende kwa Lucifer kuomba msamaha ili arudishiwe mali zake,,
hakutaka kupoteza muda usiku wa siku ya leo...ilipofika saa tisa za usiku akadamka nakuingia ndani ya kile chumba chake cha siri,,akafanya ishara huku akitamka maneno ya lugha isiyoeleweka! punde si punde ukazuka moshi mkubwa akajitokeza Lucifer akasema,,msamaha wako umekubaliwa lakini utalazimika ufanye jambo fulani...baada ya kusema maneno hayo,,,Lucifer akatoweka kimiujiza!
Fundikila akashtuka akabaki anajiuliza,,je?jambo hilo analohitajika alifanye ni jambo gani?
wakati anatahamaki,,,akasikia kisho kikubwa kiasi kule sebuleni....akatoka haraka kwenye hicho chumba cha siri akazipiga hatua kwenda sebuleni,,akawasha taa..akastaajabu kukuta vitu vyote vya sebuleni vimerudi...alipoangaza angaza macho yake akaona kadi yake ya benki juu ya meza ya kioo...akaichukua akaitazama kwa makini,,,kadi hiyo ilikuwa imeandikwa 666....akatabasamu kisha akazipiga hatua kulifuata dirisha akatazama upande wa nje,,akafurahi kuliona gari lake!
asubuhi palipokucha mke wa fundikila alidamka,,akastaajabu kukuta vitu vilivyotoweka sebuleni vimerudi..akaingiwa na hofu akajisemea moyoni,,"mbona nyumba hii inamauzauza,,yawezekana Fundikila anajua ukweli wa haya mambo,,kwa sababu yeye anaona ni mambo ya kawaida hata haonyeshi kushtushwa!
cha kushangaza mke wa Fundikila akitaka kumuuliza mumewe kuhusu ukweli wa mambo hayo,,anajikuta anasahau yani wazo hilo utoweka kichwani mwake....lakini akiwa peke yake wazo hilo humjia..
miezi ilizidi kusonga, hatimaae akatimiza miezi tisa ,,,na muda wa kujifungua ukawadia,,,
akajifungua watoto mapacha watatu(3)
**********************************
baada ya mwaka moja kupita mambo yakaanza upya ,,mapacha hao watatu wakawa wanaishiwa damu mara kwa mara ,,,jambo hilo liliwashangaza madaktari kwa sababu kila ifikapo ijumaa watoto hao huonekana kuzidiwa na mwili kunyong'onyea,,na walipopelekwa hospitali,vipimo vilionyesha kuwa damu imepungua kwenye miili yao!
hali hiyo ilijitokeza kila wiki siku ya ijumaa!hatimae vifo vikaanza,,akafa mtoto mmoja kati ya mapacha hao watatu!
baada wiki moja kupita ,,,hali ikawa tete katika familia ya Fundikila!
siku moja majira ya usiku Fundikila akiwa amelala na mkewe akajitokeza Lucifer,, akaanza kunyonya damu ya watoto wa Fundikila kwa kuwagusa mwilini! punde si punde mapacha hao wawili wakaanza kulia kwa sauti kali huku wakiweweseka..
Fundikila akashtuka kutoka usingizini,,akashtuka kumuona Lucifer kawagusa watoto wake!!!
ITAENDELEA.........
RIWAYA:ROHO YA GIZA
SEHEMU YA SITA(06)
*****ILIPOISHIA******
baada ya mwaka moja kupita mambo yakaanza upya ,,mapacha hao watatu wakawa wanaishiwa damu mara kwa mara ,,,jambo hilo liliwashangaza madaktari kwa sababu kila ifikapo ijumaa watoto hao huonekana kuzidiwa na mwili kunyong'onyea,,na walipopelekwa hospitali,vipimo vilionyesha kuwa damu imepungua kwenye miili yao!
hali hiyo ilijitokeza kila wiki siku ya ijumaa!hatimae vifo vikaanza,,akafa mtoto mmoja kati ya mapacha hao watatu!
baada wiki moja kupita ,,,hali ikawa tete katika familia ya Fundikila!
siku moja majira ya usiku Fundikila akiwa amelala na mkewe akajitokeza Lucifer,, akaanza kunyonya damu ya watoto wa Fundikila kwa kuwagusa mwilini! punde si punde mapacha hao wawili wakaanza kulia kwa sauti kali huku wakiweweseka..
Fundikila akashtuka kutoka usingizini,,akashtuka kumuona Lucifer kawagusa watoto wake!!!
*****ENDELEA******
Watoto hao wakapiga kelele wakilia mfululizo!! Fundikila akapaza sauti akisema ,,"tafadhali naomba usiwadhuru watoto wamgu....Lucifer akamtazama Fundikila kisha akatoweka kimiujiza,,,
wakati huo mke wa Fundikila alikuwa kalala usingizi hakuweza kusikia chochote wala kuona kinachoendelea! watoto hao mapacha wakaendelea kulia mfululizo ,,,mama yao akashtuka kutoka usingizini,,,akastaajabu kumuona mumewe ameketi kwenye kitanda cha watoto! huku akijaribu kuwabembeleza watoto hao mapacha wanyamaze kulia... lakini ikashindikana! pacha mmoja akaanza kunyong'onyea mwili.. akatulia tuli...
Fundikila pamoja na mkewe wakaingiwa na wasiwasi wakamkimbiza haraka hospitali,, usiku huohuo...
walipofika mtoto huyo akafanyiwa vipimo,,, ikagundulika anaupungufu wa damu,,, na imepungua kwa kiwango kikubwa kupita kiasi!! madaktari wakafanya hima,, kuokoa maisha ya mtoto huyo.. wakamtundikia dripu ya kuongeza damu..... lakini wakawa wamechelewa... mtoto huyo akapoteza maisha!!!
****************************
Fundikila pamoja na mkewe wakasikitika sana kumpoteza mtot wao wa pili kati ya wale mapacha watatu!!!
wiku zilizidi kusonga,, Fundikila akaamua kumrudia Mungu Muumba!....akatubu dhambi zake,,akawa anawachukia sana watu wanaomuabudu Lucifer... wakati mwingine alitoa siri,, hadharani!
pia alimueleza mkewe ukweli wa mambo... wakahama kwenye hiyo na kwenda kuishi eneo lingine kabisa....
kitendo hicho kilimchukiza sana Lucifer!... akaandaa mpango wa kumuangamiza Fundikila na kizazi chake.....
ilipofika nyakati za usiku wa leo,, Wafuasi wa Lucifer.. wakiwa katoka mkutano maalumu Lucifer akajitokeza kwenye kikao hicho.. watu walikuwa wengi sana siku hiyo,, kutoka nchi mbalimbali za Africa! kikao hicho ni kwa ajili ya kuandaa mikqkati ya kumuangamiza Fundikila....
Lucifer akasema,, "Mtu huyu amejitoa kwenye chama chetu... na akiendelea kubaki hai.. atatoa siri zote.. hivyo watu wataogopa kujiunga na chama chetu... natoa tamko... mtu huyu auwawe kabla hapajapambazuka,,, baada ya kumaliza kusema maneno hayo,, Lucifer akatoweka kimiujiza! punde si punde kiongozi mkuu ambaye ni wakala wa Lucifer hapa duniani! akaamuru wanachama watano waende kumuangamiza Fundikila...
wakatoweka kimiujiza wakajitokeza nje ya nyumba ya Fundikila!
huku wamevalia majoho meusi yaliyofuka mpaka sehemu ya nyuso zao... wakiwa wameshikilia mishumaa kwenye mikono yao!
wakatoweka kimiujiza wakajitokeza chumbani kwa Fundikila!
wakati huo Fundikila alikuwa sebuleni,,ameshikilia kitabu kitakatifu anasali kwa imani.... akiwa katikati ya maombi,,,, punde si punde ikasikika sauti ya mkewe akipiga kelele kule chumbani.... wakati huohuo mtoto pia akaanza kulia kwa sauti kali!
TAHARUKI!!!!!
ITAENDELEA.........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: