RIWAYA:ROHO YA GIZA SEHEMU YA NNE(04) *****ILIPOISHIA****** yule muhudumu akatazama kwenye kitabu cha orodha.. lakini halikuonekana jina la Fundikila.. Fundikila akasema, "mimi ni mteja wenu na mara ya mwisho kutoa pesa ni jana mchana.... iweje mniambie sina akaunti kwenye benki yenu... ebu acheni utani... wale wahudumu wakatazamana.... wakahisi huenda Fundikila kapatwa na ugonjwa wa akili!!! kisha wakabaki wakimtazama... Fundikila akaamua kutoka nje ya benkk hiyo.. akaingka ndank ya taxi.. akasema,, "nileleke posta ya zamani.. baada ya nusu saa wakawa wamefika.. Fundikila akashuka kutoka ndani ya gari.. akazipiga hatua kuelekea kwenye kampuni yake angalau akachukue pesa amlilpe yule dereva taxi... alipolikaribia jengo la kampuni hiyo... likatoweka mimiujiza!!! *****ENDELEA****** Fundikila akahisi kuchanganyikiwa,,akaamua kurudi kule lilipokuwa limepaki gari(taxi) akafungua mlangto ana kuingia ndania ya gari hilo,, kisha akasema,,"nipeleke nyumbani kwangu. ******************* upande mwingine kule nyumbani kwa fundikila, alionekana mkewe akiwa amejilaza kitandani,,ni baada ya kumaliza shughuli ndogo ndogo za nyumbani...akiwa usingizini akahisi mgongano wa vyombo,, kule jikoni! akashtuka kutoka usingizini akanyanyuka kutoka kitandani akaufuata mlango akaufungua na kutoka chumbani,,,,akaelekea jikoni..alipofika akastaajabu kukuta chumba cha jiko kipo tupu hakuna kitu hata kimoja!!! macho yakamtoka akaingiwaq na hofu. akatoka haraka jikoni akazipiga hatua kuelekea sebuleni,kwa lengo la nkutoka nje ya nyumba....alipoangaza macho yake akastaajabu kuona sebule ipo tupu hakuna kitu hata kimoja! akapikicha macho yake,huku akijisemea moyoni,,"hivi naota au nashuhudia kwa macho yangu? mbona maajabu haya!? hofu ikazidi kuongezeka akatimua mbio kuufuata mlango akatoka nje ya nyumba...akabaki hapo nje akimsubiria mumewe! wakati huohuo alionekana Fundikila akiwa ndani ya taxi,,,akielekea nyumbani huku akimsisitiza dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi... baqada ya nusu saa kupita Fundikila alifika nyumbani...akashuka kutoka ndani ya taxi,,akaparamia geti na kuingia upande wa ndani!akastaajabu kukuta mlango wa kuingilia ndani ya nyumba upo wazi pia mkewe yupo nje kaketi huku machozi yakimtoka! akajisemea moyoni,,"bila shaka hali sio shwari! alijisemea maneno hayo huku akizipiga hatua kumfuata mkewe pale alipokuwa ameketi,akamuuliza,,"mbona umeketi hapa nje? mkewe akajibu,,"nashindwa kuelewa hii nyumba yetu yani nilichokiona siku ya leo!!!!!!!! akasita kuendelea kusimulia kisha nakasema ingia ndani ukajionee mwenyewe. Bila kuchelewa Fundikila akazipiga hatua za harakaharaka akaingia ndani ya nyumba... macho yakamtoka kuona hakuna kitu chochote sebulen! akashtuka akaamua kuifuata korido inayoelekea vyumbani..akasukuma ukuta uliokuwa na mlango wa siri wa kuingia katika kile chumba alichokuwa akikitumia kumuomba Lucifer ampe anachokitaka! akashtuka kukuta watu watatu..wamevalia majoho meusi wakiwa wameketi chini wameizunguka mishumaa mingi iliyokuwa ikiwaka!na upande wa kichwani walikua wamefunika nyuso zao kwa kofia pana zilizokuwa zimeungana na majoho waliyokuwa wamevaa! moshi mkubwa ulikuwa umetanda ndani ya chumba hicho! punde si punde ikasikika sauti ya mke wa Fundikila akipiga kelele kule nje ya nyumba. Fundikila akatimua mbio kuelekea nje kutazama nini kimempata mkewe! kabla hajaufikia mlango wa sebuleni...ukasikika mngurumo wa kutisha na sauti za watu wengi wakiongea kwa kujibishana! Fundikila akaingiwa na hofu kupita kiasi!akapaza sauti kwa uwoga akisema,,"najua hamjaja kwa nia nzuri...lakini ninaombi, nipo tayari kupoteza uhai wangu lakini naomba muache kiumbe aliyomo tumboni mwa mke wangu...sipo taya kumpoteza mwanangu wa pekee... baada ya kuongea maneno hayo akafungua mlango na kutoka nje haraka...akashtuka kukuta mkewe kazungukwa na moto ulio waka kutokea kwenye ardhi,,moto huo uliwaka huku umechora alama ya pembe tatu! mke wa Fundikila akiwa katikati ya moto huo...yeye hakuweza kuona moto huo kwa macho ya kawaida..lakini alikuwa anahisi joto kali kupita kiasi ,,lililosababisha maumivu kwenye mwili wake! Fundikila akajisemea moyoni ,,"bila shaka wanataka kumuangamiza mtoto aliye tumboni mwa mke wangu!!! yanipasa nifaye jambo.wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla...akajitokeza Lucifer akiwa ameongozana na watu wawili wenye mbawa zilizofanana na popo! Lucifer akazipiga hatua kuwafuata wale watu waliokuwa wamemzunguka mke wa Fundikila,,miongoni mwa watu hao alikuwemo kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer duniani... Lucifera akasema,,"muacheni,,muda na wakati bado haujawadia,,hakuna haja ya kumuangamiza kiumbe huyo aliye tumboni mwa mwanamke huyo.. yawapasa muhakikishe Fundikila anapata mateso na fedhea ndipo mauti yamfuate... baada yaLucifer kuongea maneno hayo akatoweka kimiujiza na wale wafuasi wake wakatoweka muda huohuo.. mke wa Fundikila hakuwa na uwendo wa kuona yale yote yaliyotendeka muda mchache uliopita! .sasahivi ile hali ya joto kali mwilini mwake ilitoweka! Fundikila akatimua mbio kumfuata mkewe akaanza kumkagua kama kaumizwa na wale wafuasi wa Lucifer! alipogusa mwili wa mke wake,, Fundikila akaanza kutokwa na damu kwenye kucha za mikono yake! wakati anatahamaki...akahisi maumivu makali kwenye paji la uso..punde si punde akadondoka chini akapoteza fahamu!! PATASHIKA!!!!!! ITAENDELEA......... je? Fundikila atafanikiwa kumuokoa mke wake? #Ukitaka mwendelezo njo whsp 0658247651 By B professional love

at 3:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top